Sunday, February 2, 2014

UCHA MUNGU WA GHAFLA PART 1

Asalaam Aleiykum,

Kuna Baadhi ya watu wanapenda njia za rahisi, namie nimewatafutia hii moja labda kama wataiweza wanaweza kuupata Ucha Mungu kwa wepesi kabisa, Na kuna baadhi ya wengine wanapata shida na kuona mambo mazito katika kuupata Ucha Mungu, na kila wakiwaendea Wanazuoni masharti wanayopewa magumu, inabidi wakimbie wakakae njia panda, Sasa mimi katika wachache ambaye natoa (Cheap Ticket)Nakwambia usipate tabu zipo njia za Rahisi kuupata Ucha Mungu, sina vizuizi wala kuambatanisha shuruti lolote lile, sikwambii Shk fulani kasema hivi wala fulani kasema vile, mie nakupeleka kisimani, nakwambia maji haya unaweza chota unywe, huwezi tena mimi hapo sina msaada, Kwangu mie Waumini wote sawa, wote wako katika njia moja ila kwenye njia kuna mabonde na mashimo na yatakiwa umshike mkono kumuonesha mwenzio njia, na hiyo ndio kazi ninayo fanya mimi, Neno langu ninalo kwambia ni moja (Kama kweli mpenzi wa Mungu chupa ujiunge nami).
Bwana Mtume s.a.w Kabla ya kuondoka katika Ulimwengu huu alitupa ishara moja kubwa sana na inafaa kuzingatiwa, Lau kama sisi wenye kuutaka Uislam na kuitafuta hiyo (Taqwa) na kweli tunampenda Mwenye Enzi Mungu basi ishara hii tuloachiwa ni kigezo cha kutosha kuipata hiyo (Taqwa),na sote mwisho wetu ungekua mzuri wa kupigiwa mfano. Alifanya nini kabla ya kufa kwake kipenzi chetu?.
"Alimwita mkewe Bibi Aisha"Akamuuliza ""Ewe Aisha" Ndani ya Nyumba kuna kiasi gani"Wakati huo Bwana Mtume s.a.w yupo katika (Sakaratul Mauti), Na kapata nafuu kidogo, anakuja juu anamuuliza mkewe ndani ziko kiasi gani""Anajibu Bibi Aisha zimebaki (Dirham 7)""Akasema Bwana Mtume s.a.w basi  zitowe sadaka" ikisha huyo akazama tena kwenye (Sakaratul Mauti) alipokuja juu tena akamuuliza tena Bibi Aisha umeshazitoa zile (Dirham)Bibi Aisha akajibu hapana maradhi yako yamenishughulisha Ewe Mjumbe wa Mwenye Enzi Mungu, Bwana Mtume s.a.w Akatoa sauti ya Ukali, "Akamwambia Ewe Aisha zitoe upesi hizo pesa" zilipotolewa hiyo Roho ya kipenzi cha Umma huu ikarejea kwa Mollah wake.
"Ewe Muumin, Ewe Muislam kuna mafundisho gani katika tukio hili? Na kwanini zikawa Pesa? tunaingia katika maudhui hii ikiwa yatagonga kwenye Moyo wako, basi moja kwa moja, au hapo hapo linaweza kutokea tukio la wewe Kurehemewa na kupata mabadiliko katika mwenendo wako na mtizamo wako wa mambo ya Kidini, Unaweza kububujikwa na machozi ukaona kumbe hivi, siku zote mimi nimeganda kwenye mapesa wakati hayana faida yoyote, kumbe haya mapesa ndio kizuizi kikubwa cha mimi kuupata huo Ucha Mungu.
Sasa Kwanini Bwana Mtume s.a.w akatumia wakati wa kufa kwake ndio atufundishe Darsa hii ya mwisho.?
Endelea Part 2

No comments:

Post a Comment