Sunday, February 23, 2014

NGAZI SABA ZA ROHO PART 2(NGAZI 1)

Asalaam Aleiykum,

عَلَّمَ ٱلۡإِنسَـٰنَ مَا لَمۡ يَعۡلَمۡ
Amemfundisha Mwanaadamu (Chungu)ya Mambo aliyokua hayajui.
Mtizame Mtoto na vimacho vyake anavokuja katika Ulimwengu huu, akizaliwa tu maskini hajui chochote anaangaza huku na kule, kama kusema Akili yangu tupu sasa anzeni kujaza mambo yenu, lakini Mtoto (Hodari)anasikia pande zote mbili, anasikia mafundisho yanotoka kwa Mollah wake, na kusikiliza pia yanotoka kwenu, Na hivi ndio sote tunavofundishwa tokea kuzaliwa mpaka tunaingia kaburini, lakini tunafika pahala, tunasahau kusikiliza upande wa pili(Nyimbo, Ngoma,siasa zinatushughulisha)unakua husikii tena hayo mafundisho japo yanaendelea kuja(stage by stage)hiyo haki yako lazima uletewe lakini hutaki, wewe unashughulika na Elimu ya nje, umeambiwa (Elimu bila ya malipo) na kila mtu anapenda kitu cha bure, hapo tena unaanza kujazwa Mbinu za wizi, vipi utadhulumu, kuna njia ngapi za uongo, hata ukitimia miaka 21 wewe ushakua (Expert)unakabiziwa cheti unakua mtaalamu wa mipango yote, tizama sasa uharibifu unofatia unadumu na elimu hiyo mpaka ukipata kizazi chako unawarithisha ikisha huyo unajifia bila ya faida yoyote ya Uhai huu na ukarimu ulofanyiwa na Mollah wako.
Sasa unapata fundisho hili la kupanda ngazi kama utapenda utaondoka hapo ulipo ili upande hiyo ngazi kwa hiyari yako mwenyewe kumbuka hakuna anokulazimisha, Kwa ukweli wa dhati sote tuna fahamu vipi mahusiano yetu yalivyo na Namba 7 , sina haja ya kuyataja yote, ila nitalieleza hili moja ambalo pengine linaweza kuamsha kitu ndani ya Akili yako, inaweza Taa ikawaka ukapata maarifa kumbe ngazi yenyewe ilokusudiwa ndio hii, Na vile vile kumbuka somo hili hali hitaji Mabuku wala hadith (japo nimeitia moja)ili kukutosheleza fahamu yako iungane na kusudio langu, elewa haina haja ya Sheikh wala Maalim, wewe Mwenyewe ndio unakwenda katika Ngazi hizi na wewe Mwenyewe ndio utagundua sasa upo Ghorofa ya ngapi.
(1)Ngazi ya kwanza: Sote tunafahamu mahusiano yetu na hiyo Namba saba, Ukitizama kwa uangalifu katika upande wa Dini utajua kila baada ya miaka saba kunatokea mabadiliko katika maisha yako lichunguze hilo utalijua,( Wanasayansi wao wamesema kumi 7x10=70)hakuna alokosea)hiyo ndio (Life Span)ya Binaadamu wengi, wapo wanopitiliza na wapo wasofikia lakini dhumuni letu ni kuzungumzia ngazi hii ya Mwanzo na hazina zake.
endelea part 3

No comments:

Post a Comment