Sunday, February 16, 2014

NJIA KUMI ZA KUIPATA PEPO PART 1

Asalaam Aleiykum,

Elewa utakapo kutana na Ukweli shaka itakuondoka, Hapo utagundua Ukweli hautaki Wakili wala Utetezi, Utajua pia Ukweli hauna ubaguzi na unamkaribisha kila Mja kuufikia, Ndio Maana utakuta ukisema uongo mmoja unatakiwa uulinde kwa uongo mengine 99. Na Ukweli huo una njia nyingi kuufikia japo mimi leo nimechagua hizi kumi(10)ili tupate faida zake kwa pamoja, nazingumza hizi ili asije kutokea Mtu na (Fantasy)zake akawa anakwambia shika ukweli wangu ndio utapata mafanikio, kumbuka ukweli utaupata kwa juhudi zako mwenyewe na hakuna juhudi za kumfata yoyote yule ambaye anaweza kuwa hajui njia kama ulivo wewe.
Kumbuka mambo yote ya Dini yanafanyika ndani ya kifua cha Siri, chochote kile ufanyacho kuonesha watu au kujionesha mwenyewe kinakua hakina thamani katika Ulimwengu wa Dini, Ni njia tunazo ziita (Attention seeking) na hilo neno la mwisho ni zuri sana ukilisoma moja moja(See King)(Muone Mfalme) ni mambo ya kujionesha(Showing-Off). Unatakiwa Mja wewe Mawasiliano yako na upande wa Pili uyafanye kwa siri kubwa ndio unaweza kufanikiwa, Hakutakiwi maonesho huko wala watu wakuone, hutakiwi uwajulishe watu uko hivi ama vile, Ni wewe na Mollah wako siri hiyo.
Sasa kwanini nikazichagua njia hizi kumi ambazo kidogo zitakushangaza, Ni kutokana na tafauti tulonazo Binaadamu ndio maana njia zikawekwa tafauti huyu anaweza kupita ile wewe ukapita hii, Yule anaweza kwenda kwa haraka wewe ukenda taratibu lakini la muhimu nyote mtafika kwenye hiyo (Haki)ama huo Ukweli. Kumbuka tatizo sio kuchelewa bali kama jee utafika?,
Hapa natilia mkazo ukiona Mtu yoyote anatilia mkazo lazima ushike au uifate njia yake ndio ufike kwenye (Haki)Basi elewa huyo muongozaji mwenyewe hajui njia na huna haja ya kumfata atakupoteza na unatakiwa umkimbie haraka.
Tunaingia Darsa hii na tunakutana na aya ya 35 sura ya Ahzab ambayo tutaishi katika maneno hayo ili tuzijue hizo njia kumi zilokusudiwa ni zipi ili tupate faida zake. Na uzuri wa njia hizi unaweza kuchagua mwenyewe yoyote ukaifata njia hiyo ili ikupe manufaa yake. Hapa nakutaka uishi ndani neno sio kupita ukakamata neno na ukaacha maana yake. zingatia sana kisemwacho na kitakua na faida kubwa na wewe.
Endelea Part 2

No comments:

Post a Comment