Asalaam Aleiykum,
Ilikuaje Bwana Mtume s.a.w akaamua na kusisitiza aondoke msafi katika Ulimwengu huu, Hapa kwa Mwenye Akili na yule anayetaka Ucha Mungu kuna mazingatio makubwa na faida isiyo na mwisho,"Ewe Aisha zitoe haraka" Vipi Kipenzi cha Mwenye Enzi Mungu atarejea kwa Mollah wake akiwa na (Dirham 7), Yeye anaelewa kaja katika Ulimwengu huu hana chochote, Na hivi ndio sote tunavokuja katika Ulimwengu huu tukiwa Weupe hata nguo inabidi tusaidiwe, Na tukiondoka pia tunaondoka katika hali kama hiyo, Na huo ni mfano wa hakika wa kila Mmoja wetu.
Sasa tizama leo wangapi wameondoka katika Ulimwengu huu, huku nyuma watu wanapiga hesabu ya pesa zake zilizopo kwenye (Account),wamekusanyana ndugu na watoto wanapanga mipango vipi watazikaanga, Vipi watazidi kukuchoma moto kwa Million zako mwenyewe, huyu anawaza atafungua (Guest house)yule anawaza (Hotel) ya aina gani itamfaa, na hivi ndio wengi tunavoondoka katika Ulimwengu huu (Account)limefurika, na huko uendako unaulizwa vile tulokua tunakuruzuku ulikua unavitoa?
Utajibu nini wakati huo, ndio Maana Mtume s.a.w akatuonesha (Symbol)ya (Dinar)kuzitoa, Toweni msije mkaacha mapesa mnarudi kwa Mollah wenu huku nyuma watu wanayatafuna wanavotaka, na kukutia kero zaidi hata dua hawakuombei, washaitupa maiti hao wanakwenda zao.
Sasa kwa ajili gani ikawa pesa? Sababu nikuwa pesa ni kitu kigumu sana mtu kukiacha, Mtu anaweza kuacha yote lakini pesa ikamshinda, watizame wenye pesa, hata akiwa Hospital mahatuti anauliza Ngapi zimetumika,ngapi zimebakia, hesabu ikoje, na nyinyi mlomzunguka mnamuona tajiri mkubwa, lakini kwa wenye kufahamu, wale wacha Mungu wanamuona maskini mkubwa kalala kwenye kitanda, wanamuona hakuna fukara kama yeye, Lau angejikaza kidogo, akafanya bidii angejua kuwa ndani ya (Body)yake ana (Gas) hajachimba, kuna (Petrol)hajavumbua kuna madini ya kila aina lakini bado hajapata ujuzi wa kuitumia mali (Ghafi)hiyo.
Muulize Tajiri baada ya pesa ana nini chengine cha kutoa , utamkuta hana chochote kile cha kutoa, kama kula kiasi kile kile unachokula wewe na yeye ndio anachokula,umaskini umemshika wa Ucha Mungu, lakini muulize Mcha Mungu aliyegundua Utajiri wa Mollah wake atakwambia, Mie nina mambo mengi yaso na idadi, naweza kutoa kila kitu tuka (Share)nina furaha chukua na wewe kidogo, nina Dua sogea nikuombee, Nina Afya (Alhamdullilah) Nina mapenzi kaa karibu na mimi utayapata, nina Usalama ukiwa na mimi utasalimika, nina Imani ukiwa na karibu na mimi utaihisi, nina hichi na kile lakini huwezi kuvipata mpaka uwe karibu na mimi(Uwe karibu na Mollah wako), au ufate mwenendo wangu hayo na mengi mengine kutoka kwa Mollah wangu simalizi kuyahadithia.
Nakuona hivi na wewe una shauku ya kuyataka hayo, unashangaa vipi yanapatikana, Pengine wewe ni Tajiri au unapata Mshahara wa kutosha,, au Maskini hohe hahe nyote mnataraji kuupata huo utajiri wa kutoka kwa Mollah waenu, Mnatamani (Ghafla Uwe Mcha Mungu) lakini hujui ufanye nini, cha kufanya kipo, lakini jee uko tayari kukifanya?.
Endelea part 3
No comments:
Post a Comment