Asalaam Aleiykum,
Inatakiwa uanze kuchukua tahadhari sasa ungali mzima bado una hema, inabidi tukukumbushe zile operesheni mbili moja wanakufanyia wanaadamu wenzio kukuponesha maradhi yako, na ya Pili wanakufanyia Malaika kuitoa Roho yako katika hiyo (Body). Sasa Utakua na hali gani kama nikikujulisha kuwa kuna uwezekano wa kukutana na siku hii ukiwa umefurahi, jee uwezekano huo Upo?.
Naam Uwezekano upo, safari hiyo wewe unakwenda kila siku huku umefurahi kwanini siku hiyo iwe hujafurahi, Mwenye Enzi Mungu anasema katika Sura ya Al-Anaam aya ya 60.
"وَهُوَ ٱلَّذِى يَتَوَفَّٮٰڪُم بِٱلَّيۡلِ وَيَعۡلَمُ مَا جَرَحۡتُم بِٱلنَّہَارِ ثُمَّ يَبۡعَثُڪُمۡ فِيهِ لِيُقۡضَىٰٓ أَجَلٌ۬ مُّسَمًّ۬ىۖ "
Naye (Mollah wenu)Ndiye anayekufisheni(Kufa)wakati wa usiku, Na anakijua mlichofanya mchana, ikisha Yeye hukufufueni humo mchana ili muda ulowekwa utimizwe.(Mpaka mwisho wa aya)
Sasa ikiwa pahala hapo hapo kila usiku unakwenda mwenyewe kitandani ili upate kwenda huko ulikotokea leo vipi uwe na mashaka, kwanini usifurahi kama unavofurahi siku zote, na ukiamka tu unatuhadithia jana nimelala vizuri, kwani ile (Final)uwe na woga mkubwa kupita kiasi, (Hufikiri kama lazima kuna kitu hapo)umekichunguza kitu gani. Tunaendelea.
Uwezekano upo na wengi wa Waja wema wameondoka kwenye Ulimwengu huu wanafuraha ya kukutana na Mollah wao, sasa kwanini na wewe usiwe miongoni mwao?
Kuna visa vimetokea itabidi munipe Radhi zenu ili niwahadithie, vipo vingi lakini nakupeni viwili ambavyo mimi nimekua Shahidi wake. Kuna waja wema wanaondoka katika Dunia hii wanapanga mpaka maziko yao yawe vipi, huku kashanunua Sanda yake kwa Pesa za halali, Na ikisha anaagiza fulani na fulani ndio waingie kwenye kaburi langu, na kweli unashuhudia siku ya maziko yake hayo yote yanafanyika, Sasa wao walikua wanajua nini ambacho kimewafikisha katika daraja hiyo, Na kwanini sisi leo ambao wengi wetu tunasema watu wa zamani hawakusoma dini, sisi ndio tulosoma, mbona tunaogopa kununua Sanda, wangapi leo wenye Sanda zao majumbani,(Utakuta Mtu anaandika "Will"(Karatasi ya Urithi)lakini anaogopa kununua Sanda)sasa ndio unafanya nini? vipi leo ukiumwa na Kichwa tu unaanza kutetemeka, Nini kimekukuta?.
Masiku ya karibuni hivi nilikutana na Mzee Mmoja ambaye masiku yake yakuondoka Ulimwenguni yashakaribia, kwa kuwa anafahamu mimi natambua baadhi ya ishara akataka anifahamishe au anifundishe kitu kama nitakua nimesahau, Akanambia Mwanangu sasa mimi niko tayari kwenda, mimi nishajiandaa, kila kitu kiko tayari, (Na huko ndio njia ya kufahamiana kwa lugha ya Mystcism)nikamjibu naelewa, huku machozi yanatoka katika moyo wangu, kwa sababu watu kama hao akikwambia maneno kama hayo basi inakua hamalizi miezi sita, na kweli kabla ya miezi sita kutimia hiyo Roho yake ikarudi kwa Mollah wake, na mimi nikapata bahati ya kuwepo kwenye mazishi yake basi nilmbusu kipaji cha sura yake kwa (Elimu)aliyoniachia kwa njia ya (Communion).
Kwanini usiondoke umefurahi wakati kila usiku unakwenda huko huko ulipotokea, tafauti yake siku ya mwisho unaamshwa ndani ya usingizi, kuna wengine wanapata kwa bahati, (Hunipa habari nikawa nacheka sababu siwezi kuwafahamisha wakafahamu hicho walichokutana nacho ni kitendawili gani)anahadithia mtu ndani ya ndoto yake kaamka na anaiona ile ndoto, umepata kujiuliza nani Mwenye kuiona hiyo Ndoto, unaijua ladha ya kuamka ndani ya usingizi ukawa unaona ndoto yako, basi wako wenye kupata bahati hiyo mtu akakwambia na mimi nimejiona nimo kwenye ndoto, siku zote kumbuka ukiota hujioni kwenye ndoto, au huchunguzi kwanini huoti hapo ulipolala?, kwa hiyo siku ya Mauti, inakua hali kama hiyo ya kuamka kwenye Ndoto yako, unauona usingizi wako, kwanini sasa una woga, kwanini hufurahi kama alivokwambia Mollah wako
Fajr aya ya 27 mpaka 30 "يَـٰٓأَيَّتُہَا ٱلنَّفۡسُ ٱلۡمُطۡمَٮِٕنَّةُ "
Ewe Nafs iliyo tua,
Ipi nafs iliyotua? Unaijua Nafs ilotua, Ushawahi kuyaona maji yalivotulia kwenye (Mtungi) hakuna hata kitone chenye kutingishika, Kutulia huku kunakuwa kuondokewa na yale yote niloyataja hapo mwanzoni yakawa hayamo kwenye Roho yako, kutulia kwenyewe kunakuwa umeshapita daraja zote za matamanio, anaweza kuja Mwanaume au Mwanamke ikawa ndani ya Maumbile yako hakuna chochote chenye kutokea(Jitizame sasa hivi unakuaje wakitokezea), Unaweza kuona mapesa ikawa hushtuki kabisa, unaweza kutaka kupewa cheo ukawa huna hata haja nacho, ndani ya nafs yako hakuna cha kukushtua umetulia makini huna magonvi wala chuki, huna mashaka kabisa ya kilimwengu, umepoa baridi, kinachokujia katika utulivu huo ni kumkumbuka Mollah wako, ukiingia mchana unasubiri usiku ufike ili uwe karibu na Mollah wako, na ukimalizika usiku una hamu uingie mchana ili upate utulivu wa kushuhudia zawadi ya uhai inavotenda kazi zake, haupatikani usemi katika ulimi wako au fikra isipokua maneno ya kumsabahi Mollah wako, hayaaingii tena mawazo ya kipuuzi katika kichwa chako. Hapo tena unakithiri katika Ibada na kuomba mapenzi ya Mollah wako yakushukie, ukidumu katika hali hiyo Mollah wako anakwambia Nini?
Endelea Part 3
No comments:
Post a Comment