Asalaam Aleiykum,
إِنَّ ٱلۡمُسۡلِمِينَ وَٱلۡمُسۡلِمَـٰتِ
Hakika ya Waislam Wanaume na Wanawake.
(1)Hiyo njia ya kwanza ilotajwa hapo ambayo wengi tunazaliwa mpaka kufikia kuondoka Ulimwengu huu tunabaki hapo hapo, si wengi wenye kupiga hatua ya kuendelea mbele kwenye njia hii.
Nini Uislam? ni (Surrender)kujisalimisha, na hakuna taabu kubwa kama kujisalimisha kwa jambo usoweza kuliona, rahisi kujisalimisha kwa kitu unachoweza kukiona lakini vigumu sana kujisalimisha kwa kitu ambacho hukioni, inataka moyo wenye salama kukipata kitendo kama hicho, ndio maana utaona kujisalimisha kwetu kumekua kidogo kidogo, unaacha hiki, halafu unaacha kengine taratibu kwa kuwa (Surrender)yako sio kamilifu, bado mbishi, bado una afya, unakwenda ukirudi, mambo yakiwa magumu unataraji labda mzimu haujafurahi, pengine shetani kakasirika, labda nina nukusi imeniganda, kujisalamisha kwako jichunguze kukoje, nakupa (Mifano hai)jitizame jee umeingia kikamilifu katika sheria zote za Kiislam, Na kama hujaingia basi wewe ni Muislam kwa sababu moja tu umejikubalisha kujisalimisha, Na kutokana na hilo huenda ukajisalimisha upo njiani,kwa hiyo Waislam wanaume na waislam wanawake(Sote Tumo) ila kwa yule atakae amua kujitenga mwenyewe na vitendo viovu akadumu navyo.
وَٱلۡمُؤۡمِنِينَ وَٱلۡمُؤۡمِنَـٰتِ
Na Waumin Wanaume na Waumin Wanawake
(2)Njia ya pili, Ukipata kujisalimisha kwa ukamilifu nini kinatokezea? Kuna kitu kinatokezea katika Moyo wako (From Beyond)si cha Ulimwengu huu,(Something New)kitu kipya kinatawala Moyo wako unaondoka katika Njia ya Uislam na kuendelea katika Kundi la Waumin, kundi hili matendo yake, maneno yake, na kila kitu chao kimejaa uaminifu, hata ukitaka kumdhuru habadiliki tena, kuna kitu kipya kinaishi ndani ya Moyo wake, Ulimwengu huu anauona kwa njia nyengine kabisa tafauti na yule wa njia ya mwanzo, anaamini yote yanotokezea yupo mpangaji wake na yeye ni mwenye kufata, Kwenye Furaha anafurahi kwenye dhiki anakubali, kwenye huzuni anahuzunika, huku anaamini Mollah wake ni mwenye kusimamia kila jambo, anaamini yeye ni Mwenye kulitoa Jua na kuuleta Usiku, Yeye ni Mwenye kuvilaza viumbe ikisha akavihuuisha, Yeye ni Mwenye Kuleta Nuru na pia kuongoza vyote vilivyomo kwenye Ulimwengu huu, Mwenye Imani hutokwa na Machozi akijua yeye kala jirani yake hajala, hushikwa na huzuni iwapo kama Rafiki yake kafikwa na Maradhi au Misiba humshukuru Mollah wake kila anapoanza jambo au kulimaliza na hudumu na Imani hiyo kwa kipindi chote cha Uhai wake bila ya kutetereka.
وَٱلۡقَـٰنِتِينَ وَٱلۡقَـٰنِتَـٰتِ
Watiifu Wanaume na Watiifu wanawake
(3)Njia ya tatu, Ukishapita katika Njia ya pili moja kwa moja unaingia katika njia ya tatu ambayo ya Utiifu, unakua simwenye kumuasi Mollah wako katika sheria zake zote unazifata, katika njia hii unakuwa safi katika kila jambo lako, unaogopa kuigusa haramu hata iwe chembe ndogo, unazungukwa na Utiifu huo kuenea kila sehemu ya maisha yako, Unawatii wazee wako, unamtii Mumeo au Mkeo, katika mambo yote ya Uhalali.
وَٱلصَّـٰدِقِينَ وَٱلصَّـٰدِقَـٰتِ
Na Wasemao ukweli Wanaume na Wanawake.
Ukweli wenyewe upi? Ukishapita katika Njia hizo tatu za Juu moja kwa moja unageuka kuwa Ukweli, unathibitisha Ukweli wa Mambo ya Kilimwengu na ya Huko ya Upande wa Pili usionekana, kwa sababu unafunguliwa ukweli na Mwenyewe Mwenye Enzi Mungu, huwezi tena kukamata Kitabu chake halafu ukawa unakwenda Kinyume cha Ukweli, Na ukifika kwenye Njia hii basi (Shindano unaita Shindano)Huwezi kuita Msumari tena, Unasimama na msimamo wako bila ya Kuyumba, kwa sababu ushaujua ukweli, Unakuwa Mkweli, Unasema Ukweli, Huna haja ya kwenda kinyume cha huo Ukweli, (Mfano sasa hivi unaona Taa lakini hujui inakuaje hata ikawa Taa)Hujui taa imetokea wapi kwanini ikawaka sababu zake nini kuwaka taa hii, hayo ni katika Ulimwengu huu, ikisha Ghafla Mollah wako anakuonesha Nuru ambayo ni zaidi ya Taa na wewe hujapata kuiona, hapo unakua umeshauona Ukweli, sasa hivi hujaona ukweli wala hujaona hiyo taa, ila unaona vilomurikwa na Taa lakini taa yenyewe huijui, Itafute taa au Nuru ndio utaujua Ukweli.
Endelea part 3
No comments:
Post a Comment