Asalaam Aleiykum,
وَٱلصَّـٰبِرِينَ وَٱلصَّـٰبِرَٲتِ
Na Wanaosubiri Wanaume na Wanawake.
(5)Njia ya tano ni hii ya Subira, Katika Njia hii unatakiwa ujifunge kustahamili yote yatakayo kukuta, Inatakiwa uyabebe mazuri na mabaya,Inatakiwa uwe msubirifu wa hali ya juu kuipita njia hii hususan ukiwa unaishi na viumbe wenzio wenye tabia tafauti, unaishi na Familia wenye mwenendo tafauti, unaishi katika Ulimwengu wenye mabadiliko kila leo, Unaishi kwenye (Body)Mwili wako unabadilika kila siku, Unaishi na Akili yako yenye mabadiliko ya kila wakati, kuna mambo yenye kutokea katika Ulimwengu huu kila saa na dakika, Basi ikiwa yatakugusa wewe unatakiwa uwe mwenye subira katika njia hii nzito.
Nini Subira? Subira ni njia ya (Awareness)ya kufahamu kila linalojiri lina chanzo chake na mimi ninachotakiwa ni kusubiri chanzo hicho kichukue muda wake, na hilo jambo likipita bila ya wewe kuteleza hapo unakua umeshapata subira, Shida zikija unasubiri, mateso yakija unasubiri, Raha zikija unasubiri, Ukikerwa unasubiri, msiba ukikukuta unasubiri hapo tena unakua Mja wa subira.
وَٱلۡخَـٰشِعِينَ وَٱلۡخَـٰشِعَـٰتِ
Na Wanyenyekevu Wanaume na Wanawake.
(6)Njia hii ya sita ni ya Unyenyekevu, Wapi unatokea unyenyekevu, Unyenyekevu unatokea Moyoni.
Nini Unyenyekevu?
Unyenyekevu ni hali ya kufanywa Mtumwa kwa hiari yako, Kumbuka Utumwa ni jambo la kulazimishwa, iwe kwa nguvu au kwa pesa, lakini Utumwa huo ukigeuka ukawa hiyari basi unageuka kuwa unyenyekevu, (Mfano) anatakiwa kiongozi muadilifu kuwanyenyekea walomchagua ili awatumikie, na uongozi ni kokote iwe nyumbani kazini au kwengine kokote na ukiupata huo Unyenyekevu basi jua wewe unavyo vitu viwili muhimu huwezi kuwa na Unyenyekevu ila lazima una subira, na hakuna yoyote mwenye subira ila anakua mwenye kuipata Sala, Na hakuna Mwenye kuipata Sala ila anapata matunda ya Unyenyekevu nayo ni kusamehewa na kukubaliwa dua zake, kuupata unyenyekevu lazima ukubali kuwa(Nothing)ndani ya hiyo(nothing)ndipo inatokea (Something)siwezi kuhadithia haina mfano hali ya unyenyekevu ambayo ikikuingia kwa ukamilifu inakupata (Khofu)na ikikupata khofu unakua ushakwenda (Beyond).
وَٱلۡمُتَصَدِّقِينَ وَٱلۡمُتَصَدِّقَـٰتِ
Na watoao Sadaka Wanaume na Wanawake
Nani Mtoa Sadaka?
(7)Njia ya Saba, Mtoa Sadaka ni yule alosadikisha Ukweli wa kuamini kwamba yeye kapewa zawadi ya Uhai na vyote alivochuma ni zawadi kutoka kwa Mollah wake, Na yeye hana Ujira wala cha kufanya ila atumie zawadi hizo na viumbe wenzie, huyo ndio mtoa Sadaka, Anatoa akijijua yeye sie mwenye kutoa ila Mwenye Enzi Mungu ndie Mwenye kutoa kupitia kwenye chanzo chake yeye, Ametangulia kwenye kheri nyingi yule Mwenye kutoa Sadaka kwa
Wingi.
وَٱلصَّـٰٓٮِٕمِينَ وَٱلصَّـٰٓٮِٕمَـٰتِ
Na Wanaofunga Wanaume na Wanawake
Nini Kufunga?
(8)Njia ya Nane.Wanaofunga ni wale ambao wameamua Kuishi Kiroho, Funga zipo za kila aina, lakini zote ni zenye kuushirikisha Mwili (Body)Kwa sababu Roho Daima inafunga, kwa hiyo Funga yoyote ni (Brain Discipline) ukenda (Deep)utagundua ni (Control) Ya Akili yako, Ndio maana mwanzo unapoanza (Kufunga)unakua unahangaika na njaa, ukiweza ku (Control) Akili inaelekea kwengine unaanza kutamani hiki na kile mpaka wakati wa kufungua kwako, kwa hiyo mwenye kufunga kweli ambao walotajwa hapo ni wale wenye kufunga Mwili(Body) na (Mind)Akili.
وَٱلۡحَـٰفِظِينَ فُرُوجَهُمۡ وَٱلۡحَـٰفِظَـٰتِ
Na Wanao hifadhi Tupu zao Wanaume na Wanawake.
(9)Njia ya Tisa, Tunaizungumza (Most Powerful Energy)(Sex)hapa ndipo anapofeli kila mmoja wetu, Hatari zote zinatokezea hapo, ndio maana mkaambiwa msikurubie, Kuhifadhi tupu ndio mtihani mgumu kupita yote, ukiichezea (Chemical)hii kwa njia ya haramu itakuharibia maisha yako, na ukiweza kuimudu(Control)basi wewe umefaulu, vipi wewe unaweza kushindana na kitu ambacho kutokana na hiyo(Energy)wewe umezaliwa, (Everything)Kimezungukwa na (Sex)jitizame kutwa nzima wewe unaona nini, au mara ngapi yanapita mawazo ya kitu hicho katika Akili yako, kwa hiyo atakaeweza kuhifadhi tupu yake ikawa hachezi na (Energy)hii isipokua kwa njia ya halali, basi njia hii itampa ushindi ulio mkubwa kabisa katika kuisogelea hiyo haki.
وَٱلذَّٲڪِرِينَ ٱللَّهَ كَثِيرً۬ا وَٱلذَّٲڪِرَٲتِ
Na Wanaomtaja Mwenye Enzi Mungu kwa wingi Wanaume na Wanawake.
(10)Njia ya Kumi, Nini Kutaja?
Kutaja ni kukumbuka, Huwezi kutaja ila Umekumbuka, Na huwezi kukumbuka ila ulicho kikumbuka kiko karibu yako, Ima kwenye Akili au Mbele yako, Na hiyo ndio maana ya kumtaja Mollah wako kwa wingi, Na kwanini ikawa kwa wingi sababu Mollah wako yuko (Both)kwenye Akili na (Present), Kila kitu katika Ulimwengu huu kinaonesha uweza wa kuwepo kwake, Kuanzia Miti,Vidudu,Maua,Mbingu,Nyota,Jua,Mwezi na Milima na Vingi vilivyomo katika Ardhi hii, havikutoshi hivyo vyote kukumbusha Mollah kwa Wingi. Basi ukiifata kikamilifu Njia hizo nini Kinatokea.
أَعَدَّ ٱللَّهُ لَهُم مَّغۡفِرَةً۬ وَأَجۡرًا عَظِيمً۬ا
MWENYE ENZI MUNGU AMEWAANDALIA MSAMAHA NA UJIRA MKUBWA
Ametoa Ahadi Mwenye Enzi Mungu ya Kwanza kusamehe wale wote wenye kuzifata hizo njia 10, Japo moja ukiishika basi haikupotezi, isipokua ikiwa hutaki mwenyewe huo msamaha, Na hizo njia kumi nilizozitaja ni kama mtego ukiikamata yoyote inakuongoza kwenye haki, inakupeleka kwenye Ahadi ya Pili nayo ni ya kulipwa Ujira, Na hakuna ujira anostahiki Mja isipokua hiyo Pepo, amabayo imeandaliwa na Mwenye Enzi Mungu kwa ajili yetu, ikiwa Raha na Furaha za Uhai hali hii, Ina hali gani hiyo Pepo kwa Viumbe sisi wenye tamaa ya kuipata hiyo pepo.
Basi hakuna cha kufanya isipokua Fata njia hizo kumi ambazo zina kuhakikishia kupata huo msamaha na hiyo Pepo. Mollah wetu tujaalie tuwe Miongoni wa wenye kupata Msamaha wako na ujira ulo tuwekea kutupa.Amin
No comments:
Post a Comment