Asalaam Aleiykum,
Mwenye Roho ilotulia hababaiki tena na Ulimwengu, hao ndio walopata ufunuo na kuweza kupanda ngazi hii ya pili bila ya matatizo, kuna wengine wao wamepuuza ufahamu huu, Umewajia lakini hawakuutaka, wanaona vifo vinatokea kwa watu wengine, kwa hiyo wacha tuendelee kuyachapa maisha, wanasahau kabisa kuipanda ngazi hii ya pili, hawakumbuki ya mwanzo sikwambii ya pili, Sasa kama ndani husikilizi Wanaadamu wanaanza kukuhimiza "wewe nenda Makaburini"kwani kifo ni mawaidha makubwa, nenda mazikoni kuna faida utaipata.
Sasa Waja wawili nyie, yule wa mwanzo na huyu wa pili wakipanda ngazi wanakutana pia na Milango miwili, mlango wa kwanza anapita huyu alosukumwa na akapanda kwa nguvu, alokua hasikilizi anayoambiwa , yeye kajaa mashaka matupu, anajiuliza hivyo "وَكَانُواْ يَقُولُونَ أَٮِٕذَا مِتۡنَا وَكُنَّا تُرَابً۬ا وَعِظَـٰمًا أَءِنَّا لَمَبۡعُوثُونَ "
"Na walikua wakisema tutakapo kufa, na tukawa udongo na mifupa ndio (Kweli)tutafufuliwa.
Hivi ndio ilivyo watu wengi wakenda mazikoni hakuna chochote kinachotokezea, hakuna ukumbusho, watu wanabadilishana namba za simu na kuzungumza habari za zamani, ndio daima unabakia sijui marungu yapo, vipi wakikujia hao viumbe wa ajabu Malaika wanakuja na (Daftari langu) kila kitu unakitilia wasi wasi, Ukijiona upo katika hali hiyo basi jua wewe katika wale ambao somo la mauti ulikua ukilipuuza, huzitaki fahamu hizo zikikujia.
Ama kwa wale walokua wakisikiliza na kulisikia somo hili, wakawa hawalipuuzi, wao wanakwenda (Deep) wao wanajua moja kwa moja mlango wao umeandikwa "لَا يَذُوقُونَ فِيهَا ٱلۡمَوۡتَ إِلَّا ٱلۡمَوۡتَةَ ٱلۡأُولَىٰۖ"(Dukhan 56 mpaka mwisho wa aya)"Hawatayaonja Mauti ila(isipokua)mauti ya kwanza".
Moja kwa moja katika Ghorofa hii wanafungua mlango na wanakutana na mambo ya Ajabu, Wanakwenda (Beyond Death)wanakikuta kitu chengine kipya ambacho tutakuja kukijua tutakapo panda ngazi ya tatu wiki ijayo kwa kadir ya uwezo wa Mollah wetu tukiwa hai, tuone vipi Mauti yanavokuonesha mambo kiajabu.
No comments:
Post a Comment