Sunday, March 2, 2014

NGAZI SABA ZA ROHO PART 1 (NGAZI 2)

Asalaam Aleiykum,

Tunaendelea na upandaji wetu wa ngazi ya Kiroho tukiwa sasa tunaikurubia ngazi ya Pili ili tujue nako kuna hazina gani, tupate kufahamu nini kipo katika ngazi hii, tumeona vipi katika ngazi ya kwanza Mja anavolimbikiza Mali, Vipi anavo jisahau katika kutafuta chumo au pato la kumstarehesha hapa Ulimwenguni, tumetambua vipi vitu hivyo vinavyoziba masikio na macho yetu tukawa hatuna habari kabisa kama ipo ngazi nyengine nayo hii ya pili ambayo Mja anatakiwa aipande.
(2)Ngazi ya Pili, Katika ngazi hii kuna jambo unajulishwa kama vile ulivyojulishwa wakati wa kuvunja ungo au kubaleghe, sasa unajulishwa hili jengine, zinakujia Fahamu katika ngazi hii kwa mara ya mwanzo kabisa unakutana uso na macho na Kifo(Death) hilo ni tukio kubwa la pili kukujia katika maisha haya unayoishi katika Ulimwengu huu. Umepewa fahamu ya kwanza, sasa unapewa fahamu ya pili, mwanzo ulioneshwa maisha na sasa unaoneshwa mauti, unakutana nayo uso kwa macho, kama mwanzo ulivogundua (Sex)na sasa unagundua (Death).
Kwa bahati mbaya ufunuo huu wengi ukiwafikia wanajaribu kuukwepa, wanajitahidi kujibabaisha, wengine wanapuuza kabisa hawataki mawazo haya, Na unakuja ufunuo au fahamu hizi katika kipindi cha miaka 40, lakini wengi unawafikia kwa ukweli wa dhati katika kipindi cha miaka 49. Hapo tena utaona Mtu kidogo anaanza kubadilika anapiga (Break) analeta (Slow down) kwa wale walo bahatika, lakini wengine waloghafilika wanaendelea kulisakata(Rumba).
Ama kama ukikujia ufunuo huu na wewe uko (Aware)Umekukuta ukiwa ni kipenzi cha Mwenye enzi Mungu, hapo katika Ngazi hii unakutana na hii aya katika sura ya Fajr. 
 يَـٰٓأَيَّتُہَا ٱلنَّفۡسُ ٱلۡمُطۡمَٮِٕنَّةُ
Ewe Nafs Ilotulia
ٱرۡجِعِىٓ إِلَىٰ رَبِّكِ رَاضِيَةً۬ مَّرۡضِيَّةً۬
Rejea kwa Mollah wako, hali yakuwa umeridhika, Na (Mollah)wako ameridhika na wewe.
Vipi kuridhika kwako?
Ukishapata Fahamu hizi za Umauti kinakujia kitu cha kukumbusha kuwa siku zote unahudhuria maziko lakini hakuna kitu kinachokugusa katika nafsi yako, unaona umekwenda tu, lakini hakuna chochote, mbona sitishiki, sasa nini hicho kinogusa nafsi yako katika ngazi hii ya pili?
endelea part 2

No comments:

Post a Comment