Asalaam Aleiykum,
Desturi ya kuona unayoifahamu wewe ni kuchukua (Information)Nje na kuzipeleka ndani, hata hivyo mamia ya (Information)unayasahau kabla hayajafika ndani kuchambuliwa, mfano wa (Cinema)unaona Nyumba, unaona (Furniture)na kila kitu, lakini unasahau yote ila unakumbuka jambo moja nalo ni (Story)kwa hiyo utakua umeiona (Story) na yule alo (Act) kwa kufanya hivyo kuona kwako umetumia (Akili) ndio maana kila unachoona hivi sasa ni vilevile viliyopo kwenye (Memory)yako.
Na kuona kwa aina nyengine ni huku kutumia Roho(Direct communion)kuona huku kumetajwa ndani ya Quraan sura ya (Najm)aya ya 10"مَا كَذَبَ ٱلۡفُؤَادُ مَا رَأَىٰٓ ""Moyo haukusema Uongo uliyoyaona".
Huko ndio kuona kwa (Clear)huwezi kukadhibisha, hakuna uongo katika kuona huko, ila kuna mshangao, na kwanini ikawa kwenye Moyo? hayo tutayazungumza siku za mbele kukujulisha chini ya Moyo kuna kaa nini? Ila nitakupa kitu ukitizame(Ukicheka kama unaweza kukumbuka jitizame)kila kitu kina (Dis-appear)litizame hilo neno vizuri halafu litie maana utagundua kitu fulani, Ukicheka (Time) inapotea kwa sekunde unabakia wewe na huoni chochote, ukimaliza kucheka jiulize nani yule alocheka, hapo utagundua kumbe hata kicheko kinatokea Moyoni, na hapo hapo ndio unapo patikana huo Muono.
Kwa mara ya mwanzo unapoondolewa pazia hili au kufikia ngazi hii ya sita, utajua kumbe hapa ndio ngazi ya wale matabibu wote wa ukweli, kumbuka sio (Uchawi) sababu uchawi ni tendo linalopatikana kwenye (Akili), Lakini Utibabu unatokea kwenye Roho, Na kitokeacho kwenye Roho kimetoka kwa Mwenyewe Mollah Mkarim, (Tukawajaalia kusikia na kuona). Kuona huku anako funguliwa Mja ni hisani ya Mollah wako kukuonesha mambo yalofichikana, Ili kumkaribisha kiumbe katika ufalme wa mambo ya siri ndio pazia linaondoshwa kidogo kidogo kwa daraja yako ya Ucha Mungu, na zaidi sana hupewa wale walokwisha kuihama dunia hii wakawa hawana haja nayo japokua wako hai.
endelea part 3
No comments:
Post a Comment