Asalaam Aleiykum,
Unakwenda mazikoni unaona ni kumfukia mwenzio, ndio maana unafanya maskhara makaburini, sababu huna hisia, maziko hayakukumbushi chochote , lakini ukipata fahamu za mauti, sasa kifo kinakua kweli juu yako, Unakutana na kile kitu kinacho chukua kila kitu ulokua nacho, Mali, Mke,Mume,watoto,marafiki, kila kitu ulichoita chako kwenye Ulimwengu huu kinatoweka, Na kuchukuliwa na kifo.
Unapata kufahamu katika ngazi hii kuwa wakati wowote zamu yangu itafika, wako wapi wazee wangu, wako wapi marafiki zangu,wangapi wameshatangulia, wengi nilokua nao washatangulia chini ya Ardhi, kifo kinamchukua kila mtu, hapo tena kama Mja Mwema ulojifunga na Mollah wako unashukuru Mungu kwa yote ulofanya katika Ulimwengu huu yaliyo mema, Na yale Mabaya unajifunga kuanza kuomba msamaha(Toba).
Hapo zinakujia fikira kuwa Mollah wako kakupa nafasi na kukumbusha kadhia hii ya Mauti, unaanza kuona kadhia yote ya Vyeo, kutafuta mali, kushiriki anasa yashapitwa na wakati, linakujia wazo kuwa huna haja tena ya kutafuta (Viagra) na hivi na vile, unakumbuka kuwa Mollah wako mwanzo ndio alokupa nguvu hizo na sasa amezichukua lazima kuna mpango wake alonipangia nguvu hizo sasa zitumike vipi, Na mimi nimeridhika nafata amri zake, Nakubali wakati wowote namie Mauti yatanihudhuria, Na kwa jambo hilo mimi sina mamlaka nalo.
Kwa hiyo kuanzia hivi sasa nimeridhika na Namuachia Mollah ndio awe Muamuzi wa mambo yangu yote, kama kikija cheo au ukubwa fulani sawa, Nikipata mali sawa, nikikosa sawa, sasa nimeshagundua Mauti na kazi yake na hakuna kinacho ni shughulisha isipokua Mollah wangu. Na mimi kwa hilo nimeridhika sasa najiunga na watu wema kusubiri fadhila za Mollah wangu.
Endelea part 3
No comments:
Post a Comment