Sunday, March 9, 2014

NGAZI SABA ZA ROHO PART 2 (NGAZI 3)

Asalaam Aleiykum,

Kama ulivopita kwenye (Baleghe)na kwenye Mauti unapita hivyo hivyo ukiwa (Live), Ndio maana unaambiwa kumbuka Mauti, hili tukio lipo, pia litatokea, kwa hiyo wakati una Akili yako timamu kabla hujawa mgonjwa hudhuria kadhia hii, nini kinatokezea ukihudhuria unafahamu zako kikamilifu.
(3)Ngazi ya Tatu: Inatokezea (Transformation)mabadiliko makubwa, yakiambatana na maajabu makubwa, unakua (New Man) kama kweli utaipanda Ngazi hii kwa fahamu zako ukadhihiri ukweli wa (Mauti)inakujia Fahamu, kumbuka Fahamu inatokea ndani sio kwa yule (maiti)unayemuona ila (Understanding) ya kujua kumbe kinachokufa ni kiwiliwili changu, Kinachopita katika haya Mauti ni kitu chengine kabisa ambacho hakiguswi na haya Mauti, Nini hichi ambacho baada ya Mauti yangu kinabakia?.
Jee Naweza kukijua nikiwa Hai, sio mpaka nisubiri mpaka siku yangu ya kufa, Jawabu ndio,بَلِ ٱلۡإِنسَـٰنُ عَلَىٰ نَفۡسِهِۦ بَصِيرَة.
Anza safari ya kukutana na Nafsi na ukikutana nayo inakupeleka katika safari ya maajabu, inakutoa katika dhiki ya Dunia na kukupeleka kwenye Raha na maajabu ya Ulimwengu huu ambayo ulikua huyajui, Na ukiingia katika Ulimwengu wa Fahamu hii ya kuijua Nafsi yako unabadilika na kuwa Mtu mwengine kabisa, unatoweka katika maisha ya kawaida na hapo tena unaanza safari ya Ulimwengu wa kushangaza nini unakutana nacho katika maajabu hayo, katika ngazi hii kila kitu unakiona kwa njia nyengine kabisa, kila jambo linajifungua tafsiri yake na kuweka wazi siri zake.
Unapokutana na Nafsi yako kitu cha mwanzo unacho gundua ni kuona kumbe huu Mwili wangu (Body) ni (Inteligence)tupu inafanya kazi bila ya mimi kuingilia, ni miujiza baada ya miujiza inatumika, una elewa kumbe mimi nimeubeba tu mwili huu, lakini unafanya kazi zake bila ya kunihitaji mimi, unasaga chakula, unasafisha damu, unajiponesha wenyewe, na unafanya kazi zake nyingi pasi mimi kuingilia, kuanzia kidole gumba mpaka utosini muujiza huu unajitosheleza wenyewe.
Hapo tena unagundua kumbe mimi nimebeba kiwanda kizima natembea nacho, Nani huyu Mwenye kujua, nani huyu mwenye kusikia,Nani huyu Mwenye kuhisi, Nani huyu anoshuhudia haya yote, Na baada ya kushuhudia mwisho anakwenda wapi huyu Shahidi?, hapo sasa ukimaliza utaanza kuangaza Nje uone nako kuna nini?,(Hakika Nafsi ni Yenye kuona) Ukiweza kuona basi na kutizama inakua Rahisi, kumbuka kuona ni (Within)Ndani, Na kutizama ni (Outer)Nje hapo utaanza kuona mengine ya mfano kama wako na mengine zaidi, Nini hayo?
Endelea Part 3

No comments:

Post a Comment