Asalaam Aleiykum,
Tumepita kwenye maajabu na kuangaza kule na huku na kama umekwenda (Deep)itakua umegundua mambo mengi ambayo hayeshi na wala huwezi kuyagundua, hujui uwache lipi ushike lipi, dunia nzima ni maajabu matupu, Sasa unatamani upande ngazi ya Nne, shauku imekushika, ukifika hapa sasa unapewa msaada wa kuipanda ngazi hii kwa (Lift)unachukuliwa kama (Airport)na Ngazi ya Umeme, mara huyo unajikuta umewasili kwenye ghorofa ukaapo Moyo, Ghorofa yanapoishi Mapenzi.
Ufikapo kwenye Ngazi hii la mwanzo kabisa unakumbwa na (Khofu)kumbuka sio (Hofu) tafauti yake khofu ni afya, khofu ni furaha, na hofu ni maradhi, woga, shida balaa, Sasa kwenye Ngazi hii unakumbwa na khofu, ikisha unajaa unyenyekevu, katika Ngazi hii mapenzi unayokutana nayo ni ya kudumu, kila wakati hutaki ladha hii ikutoke, hapo ndio unapata siri ya kwanini kila kiumbe kimejaa mapenzi,sasa utakua unamuona Paka na vitoto vyake kwa njia nyengine, kuku na vitoto vyake kwa njia nyengine kabisa, utawatizama Ndege na vikinda vyake kwa mtazamo mwengine kabisa, ukishamaliza wanyama utagundua kumbe mpaka miti ina mapenzi, hata Miti nayo inahuzunika, mpenzi wake akifa au akikatwa kuwa mbao basi iangalie miti ilosalia inakua na hali gani?.
Mpaka Samaki nao wanapendana? nini hichi kitu kinachoitwa Mapenzi.
Nini Mapenzi? Mapenzi ni Miujiza, Nini Miujiza?
Miujiza ni kitu chenye kutokea au kubadilika bila ya matarijio, kumbuka umetoka kwenye Maajabu na sasa unaingia kwenye Miujiza, Na pia napenda uelewe vitu hivi vitatu (Maisha,Kifo,Na Mapenzi)vyote ni Miujiza(Mystirious)unaishi navyo lakini hujui siri yake, vyote vinatokea kinyume cha matarajio yako, Sasa kama ushaishi kwenye Maajabu nakuta utumbukie sasa kwenye Ulimwengu wa Miujiza ambao wewe huna Mamlaka nao.
Endelea Part 2
No comments:
Post a Comment