Sunday, March 16, 2014

NGAZI SABA ZA ROHO PART 2 (NGAZI 4)

Asalaam Aleiykum,

(4)Ngazi ya Nne, Ngazi hii ya Nne watu wakishafika Mtu anasahau kwanini yupo kwenye ngazi hii, Na katika usahaulivu huo unatukuta Muujiza huu katika tamaa zetu za Maisha ndio unajikuta Mtu unasutwa na Quraan sura ya Fajir aya ya 20.وَتُحِبُّونَ ٱلۡمَالَ حُبًّ۬ا جَمًّ۬ا
Na Mnapenda Mali pendo la kupita kiasi"
Unayageuza hayo mapenzi kwenye kitu kisichosema, kisicho hisi,unakua ugonjwa  wako mapenzi ya pesa, unapenda Mali mpaka unafikia kusahau kuwa wewe umezungukwa na watu, Mali inakucheka Maskini mtizameni huyu mgonjwa, ananipenda mimi nisokua na fahamu, badala ya kumpenda mwenye fahamu anashughulika na mimi.
Nini Mapenzi? Hakuna awezaye kujibu swali hili, nani anoweza kuueleza muujizi ni nini? tunachoweza kufanya ni kuishi kwenye muujiza, kwenda karibu yake na kujiunga na huo muujiza, kupata hisia zake, hilo tu ndilo tunaweza kulitenda na ukitoka katika huo muujiza ndio unahadithia  wenzio tafsiri chungu nzima, Unaanza kwa kusema Mapenzi ni Ukarimu, Ukarimu ni Uhuru, sasa wanokusikiliza wanachanganyikiwa na maneno haya, Na kama mtu ataleta ufanisi wa lugha maana yote itampita ya kufahamu Mapenzi.
Sasa yasome nini Mapenzi ujue kwa uzuri, Mapenzi ni Uhuru na hapa Wazungu wanamsemo mzuri ikiwa utazingatia, wanasema hivi (Ukimpenda Mtu Mwache aende akirudi mwenyewe kwa hiyari yake basi jua huyo ni Kipenzi chako).
Upo katika Ngazi ya 4, Soma kwa Makini ili uishi ndani ya Muujiza huu wa Mapenzi upate kujua yanakuaje, ili yatakapo kujia au kukuta ujue unayakabili vipi, Kumbuka Miujiza ipo mingi lakini muujiza wa Mapenzi lazima Roho ipite Ngazi ya 4 ili kukutana nayo, sasa yatupie macho mapenzi. uyaone yanaanza vipi?.
Kwanza kabisa Mollah wako kwa hayo Mapenzi ya Kiumbe wake kakuumba ikisha akakufanyia Ukarimu wa Uhai na kukufanya Khalifa, Halafu tena akakupa Uhuru kukuwaachia utende unavyopenda, Halafu tena akakupa ukumbusho  Ewe Kiumbe changu Ukirudi kwa hiyari yako hayo ndio Mapenzi juu yangu, Ndio akasema Mollah wetu katika Quraan mimi (Nawapenda) (Surat Buruj 13-14)إِنَّهُ ۥ هُوَ يُبۡدِئُ وَيُعِيدُ 
"Yeye ndiye aliyeanzisha(aliyeumba)Na ndiye atakayewarejesha(tena)وَهُوَ ٱلۡغَفُورُ ٱلۡوَدُودُ
"Naye ni Mwingi wa Msamaha (Na)Mpenda(Viumbe vyake).
Na hiyo ndio maana ya Ibadah,kurejea kwa Mollah wako kwa Mapenzi, Na hiyo ndio Miujiza pekee (Something inside)Ndani ya Moyo wako inakutuma umtafute na kumjua Mollah wako kipenzi kwa hiyari yako, sio kwa kuogopa Moto au kuitaka Pepo.
Kuumbwa kwako Binaadamu ni Miujiza na kurejea kwako vilevile ni Kimiujiza. Unataka kujua vipi unarejea kimiujiza hudhuria kisa hichi katika Quraan ili ujue unarejea vipi?
Endelea part 3

No comments:

Post a Comment