Asalaam Aleiykum,
Umetokea kwenye Ngazi ya Mapenzi sasa nini kinatokea wakati Mapenzi yashajaa Moyoni, angalia nini kinatokea, tunajua chochote chenye kujaa lazima kitoke,(Maana ya kujaa nafasi hakuna tena)na mapenzi yakijaa lazima uyagawe au yatageuka sumu, yatageuka chuki, yatageuka wivu, ili kuipata salama ya mapenzi lazima (Share)hiyo ndiyo (Taqwa)kwanza unajipenda mwenyewe ikisha unapenda kilicho nje,(Ikiwa mwenyewe unajichukia vipi utapenda kilicho nje)ndio maana unapita kutangaza mpaka kupiga (msuwaki haramu)Naam na (Taqwa) yenyewe Uwapende Maskini na Mayatima, uwapende Mafukara na Viumbe wenzio Nk.
Ngazi ya 5. Unapanda ngazi hii lazima ufahamu kinachotokea katika (Ghorofa hii). Kinachotokea hapo ni Mgeni amewasili, na lazima utue mzigo wako, kwa sababu umebeba kitu Adhimu moyoni mwako, katika kitu hicho Mapenzi ukiyafungua zinamwagika zawadi za (Hekima). Kama yalivyo maua yanabeba vitu viwili muhimu(Uzuri na Harafu)Na Mapenzi vilevile yanabeba vitu viwili(Fadhila na Hekima)Na sasa yameshachanua , Na kama hujijui upo ngazi gani, basi wewe huna dawa tena.
Ngazi uliyopo hivi sasa kama ushajijua basi utakutana na aya ya 269 sura ya (Baqara) inayosema hivi:
"يُؤۡتِى ٱلۡحِڪۡمَةَ مَن يَشَآءُۚ وَمَن يُؤۡتَ ٱلۡحِڪۡمَةَ فَقَدۡ أُوتِىَ خَيۡرً۬ا ڪَثِيرً۬اۗ وَمَا يَذَّڪَّرُ إِلَّآ أُوْلُواْ ٱلۡأَلۡبَـٰبِ"
(Mwenye enzi Mungu)Humpa Hekima amtakaye, Na aliyepewa Hekima bila shaka amepewa Kheri nyingi, Na hawakumbuki ila wenye Akili.
Ndio Maana anopenda haogopi kutoa, kheri alizopewa nyingi, Zawadi imetokea Kwa Mollah wake, kajaa mapenzi mwenye hekima humkuti kucheza (Karate au Judo)kwa sababu kajaa kitu chengine kabisa(Blissful)ukenda na Magonvi anapatanisha, Na wala hachonganishi, yupo kwenye Raha ndio maana husema hata usingizi sipati, hataki kuikosa raha ya Ku (Enjoy).
Nini Hekima?
Endelea Part 2
No comments:
Post a Comment