Sunday, March 16, 2014

NGAZI SABA ZA ROHO PART 3 (NGAZI 4

Asalaam Aleiykum,

(In loves Death does happen) Upo Ngazi ya 4 mambo yanatokezea bila ya wewe kutaka, na hali hiyo ni haki yako lazima uipate, ama ukiikataa ni shauri lako mwenyewe.Mapenzi yanatokea kwenye Moyo wako, mabadiliko kila siku yanatokea lakini kila yakitokezea wewe hupo kabisa pengine upo Dodoma, au upo kwenye Taarab, au umeketi kwenye Gumzo huna habari ya Siri hizi zinazotokea kwenye Nafsi yako.Ni kweli maneno hayo ya mwanzo Kifo kinatokezea katika hayo mapenzi ya kitu chochote, ndio maana nikasema hapo mwanzoni (Maisha, Mapenzi na Kifo)vyote ni Miujiza kwetu, bado vinatushangaza, sasa nini kinatokezea, halafu jiulize na wewe wakati mwengine hayakutokezei baadhi ya Mambo wakati pengine unasikiza dua, au umehudhuria msiba au unasikiza mawaidha nini kinatokezea?(Al-Shuara 46)"فَأُلۡقِىَ ٱلسَّحَرَةُ سَـٰجِدِينَ"
"Walipinduka Wachawi wakasujudu"
Sio wachawi hata wewe wakati mwengine inakujia uwache, inakujia upinduke lakini umezidiwa na mambo, mapenzi ya kusujudu hayajafika, hata ukisujudu bado kichwa kiko ardhini, akili ipo Disco, pengine haijarudi Dodoma, au bado hujafunga hesabu.

Kwanini walipinduka, Walipinduka kutokana na (Khofu)sio Hofu, Nini tafauti yake?utaijua huko mbele, ila napenda ujue katika Mapenzi yoyote kila mpenzi ana khofu ya kumpoteza mpenzi wake, inakuaje hali hiyo, (Khofu)ni miujiza, inatokea wapi? ndio kinacho tushangaza, "katika aya za mbele Firauni" ana Nadi nitakukateni miguu na mikono ikisha nitakusulubuni" Wachawi umewafika Ukweli, Na ukweli ukikufika unakuja na mapenzi, wameshaona hakuna chengine chochote kiwezacho kuushinda ukweli huu hata kifo hakina nafasi tena hapa, Wakasema "
"قَالُواْ لَا ضَيۡرَ‌ۖ إِنَّآ إِلَىٰ رَبِّنَا مُنقَلِبُونَ "
Hakuna Dhara tena, Kwa Mollah wetu sisi tutarejea.
Hiyo ndio hali ya Mapenzi, hata kifo hujali tena, sisi tumesha (Surrender)tumetulia na tuna tamaa Mollah wetu atatusamehe Makosa yetu kwani sisi tumekua wenye kusilimu.
Na hiyo ndio Maana ya Mwingi wa Rehma Mwenye Kurehemu(Mawadat wa Rahma)Lazima viwili hivi vende pamoja, (Hapa itabidi nifafanue kidogo)kwanini hapa imewapata Khofu wakarejea kwa Mollah wao,)Tunachojua Khofu ni miujiza lakini hatujui wapi unatokea, Kitu kinafanyika Nje wewe unatetemeka ndani ya Moyo, kwanini ikawa hivyo, inabidi ufahamu msemo huu, au uwatizame baina ya shujaa na mwoga(Kwa Shujaa huenda Kilio, na Kwa Mwoga huenda kicheko)kwanini isiwe (kinyume chake)kwa sababu wawili hao wote wako sawa ila tafauti yao Shujaa ana Khofu na Mwoga ana Hofu, mambo mawili tafauti, (Khofu inatokea Moyoni) na (Hofu inatoka kwenye Akili)ndio maana mmoja yuko tayari kufa na yule wapili yupo tayari kukimbia.
Ndio maana na wewe kama unajifanya Shujaa wa hapa Duniani basi kwako kitakwenda kilio siku ya malipo, na yule alokua Mwoga hapa Ulimwenguni kwake kitakwenda kicheko. Zingatia viwili hivyo utapata faida kubwa ukifahamu. Sasa panda ngazi hii ya 4 uwapende Wazazi wako, uwapende ndugu zako, uwapende maskini na mafukara na mayatima, uwapende familia yako mke na watoto zako. Ili siku hiyo itakapo kujia siku ya habari ya Khofu usiwe katika wale wenye Sura ya Kuogopa(Sura ya Ghashiyya)ila uwe katika kundi la wale wenye sura ziloneemeka. Na hayo ndio mapenzi.
Na hakuna kitu kinacho Mtisha Kiumbe kama Moto, ndio maana mtu akiona moto hata akiwa ghorofa ya Mia, yuko radhi achupe kuliko kufa kwa Moto, watizame wanyama wanavotoka mbio kwenye misitu kuukimbia moto, Na hivi ndivo yalivyo mapenzi yetu Moto mtupu, hakuna raha magonvi yametawala, baada ya kumpenda mwenzio unapenda Mali, Unapenda Haramu, unapenda Mirungi, unapenda Pombe, unapenda Disco, kila kibaya ndicho unachopenda wewe vipi leo mapenzi matamu yatatokea kwenye Moyo wako, vipi utaipanda ngazi hii ya 4 ukiwa na mizigo hiyo yote, Miujiza hii haiwezi kutokea kwenye Moyo wako, na hata ikitokezea utaona unapenda Mpira, uko Radhi upende watu kumi na moja kuliko kumpenda mmoja alokaribu yako(Mkeo).
Tupo katika Ngazi hii ya 4 ambayo Roho pengine hivi sasa ndio inapita, sasa elewa hapa ndio kwenye kufungukiwa na Moyo wa mapenzi, hapa unagundua kumbe katika mambo mengi niyafanyao yamezungukwa na mapenzi, kumbe kama sina mapenzi nakua maradhi matupu, Bila ya Mapenzi sina afya njema, hapo tena kama una ufahamu nzuri unaomba muujiza huu wa mapenzi, na vipi muujiza huu utakufikia lazima kwanza ushushe mizigo, mapenzi yanateremka daima, lakini kwako hayafiki sababu (Vipeto)ulobeba moyoni mwako ni vingi, penzi halina sehemu ya kukaa, Matatizo sio mapenzi, matatizo ni moyo wako.
Nini Ufanye? la Mwanzo kabisa anza kusamehe kwa kila alokukosea, usibebe mizigo yao ukaweka donge moyoni, kumbuka walokosa wao kwanini unaumia wewe,Pengine katika moyo wako unatamani uwe Tajiri na hilo haliwezekani, ondosha tamaa hizo, Roho inatamani mapenzi lakini moyo hautaki.
Sasa ufanye nini katika Ngazi hii ili usikose Raha za Mapenzi, Usikose kumpenda Mollah wako, Familia yako na kila Kiumbe. Itabidi hapa tukuanzishe mazoezi, Moyo unataka mazoezi ya nje na ndani, Ama ya nje nenda (Walk)tembea tembea, moyo unakwenda mbio unapata mazoezi, Na mazoezi ya Ndani ni kushituliwa yote ni sawa, ukenda mbio unapiga kwa kasi na ukishituliwa unapiga kwa kasi, kwa hiyo (Formula)ni hiyo hiyo ya kuamsha Moyo ulo lala.
Vipi utauamsha ili ujae Mapenzi, mapenzi yaanze kuteremka, la kwanza kabisa unatakiwa ulete Maghfira angalau mara 70 kwa siku kwa muda wa miezi mitatu, Ikisha ujichunguze mambo mangapi unayapenda moyoni mwako ya hesabu(Pengine unapenda Ugali nk)ya hesabu, halafu lipitie moja baada ya jengine ujiulize kwanini, ukishajua sababu yake kazi yake imekwisha hutoganda tena kulipenda utasema (Alhamdullillah)hapo moyo wako utakua (Empty)kwa jambo hilo, sasa tena huna la kufanya subiri kidogo kidogo miujiza itaanza kushuka hapo tena Moyo utaanza kujaa mapenzi ya Mollah wako na ya kijaa tu, utaanza kupenda viumbe wenzio, sala yako itakua yakukutoa machozi, Mkeo au Mumeo umekaa naye siku zote utamuona vyengine, ukikerwa utakua unacheka, na ukifurahishwa utakua unalia kwa ajili ya mapenzi na hiyo ndio(Bliss)ipate ubadilike, Na ukibadilika kwa ajili ya mapenzi nini kinatokea?
Hayo Inshaallah tutakutana nayo kwenye ngazi ya 5.

No comments:

Post a Comment