Asalaam Aleiykum,
Hapo tena utaanza kumuona Ndege kwa njia Nyengine, utajiuliza vipi anabeba Mwili wake na kupaa angani, kitu gani kinacho mfanya apae na kubakia Angani, Nini kile kilichobeba Mwili ule hapo tena ukizidi kuchambua na kutaka kuyajua, unakutana na maajabu juu ya maajabu na nitayataja machache sura ya Hajj aya ya 18."أَلَمۡ تَرَ أَنَّ ٱللَّهَ يَسۡجُدُ لَهُ ۥ مَن فِى ٱلسَّمَـٰوَٲتِ وَمَن فِى ٱلۡأَرۡضِ وَٱلشَّمۡسُ وَٱلۡقَمَرُ وَٱلنُّجُومُ وَٱلۡجِبَالُ وَٱلشَّجَرُ وَٱلدَّوَآبُّ وَڪَثِيرٌ۬ مِّنَ ٱلنَّاسِۖ
(Mpaka mwisho wa aya)
(Uko katika kuona)"Jee Huoni kwamba Mwenye Enzi Mungu kinamsujudia kila kilichomo Mbinguni na kilichomo Ardhini, Na Jua na Mwezi na Nyota na Milima na Miti na Wanyama na Wengi Miongoni mwa Watu".
Hapo yamesemwa maneno makubwa yanatakiwa kuzingatiwa ili yakubadilishe muono wako, ikiwa vyote vilotajwa hapo vina Sujjudu ina maana lazima katika vitu hivyo ipo (Consciousness) (Awareness)ya kumjua Mollah wake, vyote vinafanya kitendo cha (Surrender)kwa Mollah wao, vyote vimeumbwa na vinaleta heshima kwa kumjua Mollah wao, kwa ajili hiyo basi lazima vitu hivi vitakua na (Sense) ya kuhisi kama ulivo mfano wa Mti wenye kufata maji chini kwa chini hata mita mia mbili, Na milima na sauti zake za mzungumzo ya kimya kimya, na Wanyama na tabia zao zilopangika za kupumzika wanapokwisha kula, vipi wanasujjudu? lazima kwanza tujiulize nini Sujjudu(Sijda) Ni (Surrender)kujisalimisha kikamilifu, kwa heshima na kuridhia na kufahamu kuwa kila kiumbe kimeumbwa na katika kuifanya hiyo (Sijda)ni kutekeleza Utiifu wako kwa Muumba, unakwenda kwa heshima zote kuwa umefata Amri za Mollah wako, umeacha kila kitu, unakwenda ukiwa msafi na sasa unaanguka kurudi kwa Mollah wako kwa Unyenyekevu ukiwa umekubali huna tena pengine pakwenda isipokua kurejea kwa Muumba wako ukiridhi apitishe hukumu yake, (Complete)huna cha kutenda zaidi ya kushukuru kwa hisani ya kuumbwa.
Sio hizi Sijda unakwenda ushadhulumu, umekwiba, umezini umepinga amri zote za Mollah halafu unakwenda kusujjudu? hizo hazifai kabisa, kwanza acha ulonayo halafu tena ndio nenda ukaipate sijida, utaikuta sijida yako tafauti, utajikuta machozi yanakumiminika bure ndani ya sijjida, na hiyo ndio maana ya vyote vinamsujudia, vyote vimekiri, vyote havendi kinyume na Mollah wao, hulikuti Jua kuutangulia mwezi wala mwezi kutangulia Jua, vyote vina tii, Na ndio ukichunguza sana utaona Milima, Nyota , wanyama Binaadamu vyote tushajua vinakufa vilobaki viwili ambavyo pia vinatarajiwa kufa navyo ni Jua na Mwezi sasa ikiwa umepata habari hii chache ya ngazi ya Maajabu endelea kutafuta mwenyewe mengine yalosalia ambayo hayeshi katika Ulimwengu huu. Inshaallah tumepita katika ngazi hii ya maajabu, Wiki ijayo tutaingia ngazi ya Nne yenye Miujiza.
No comments:
Post a Comment