Sunday, March 9, 2014

NGAZI SABA ZA ROHO PART 1 (NGAZI 3)

Asalaam Aleiykum,


Tumepita kwenye ngazi mbili za mwanzo huku tukitupiwa maua ya Fahamu, Na kama hujapanda vizuri au ulikua unapepesuka au niseme hujafahamu, basi wacha kidogo nifafanue kabla hatujapanda ngazi hii ya Tatu. Mwanzo kabisa tumeanza na maji ya Uzazi au (Baleghe)wakati ule ulipopewa Fahamu, Ikisha tukapanda ngazi ya Pili tukakutana na (Kifo)au(Mauti), Na watu wengi wanadhani huo ndio Mwisho wetu.
Kweli inaweza kuwa mwisho wako ikiwa umekwama kwenye ngazi ya kwanza(Lift)halifanyi kazi, lakini kama umepanda ngazi ya pili ikisha ukamudu kuja katika ngazi hii ya tatu, Utafahamu nini maana ya Mauti, kwanini ukawa unasisitizwa uyakumbuke mara kwa mara, nini kinatokezea yanapokukuta Mauti, hapa napenda nifahamishe yapo mauti ya aina ngapi?
Mauti yapo ya aina mbili, unategemea vipi yatakukuta, au utayafata, kukukuta yanakuja, kuyafata ni kuyakuta na kwenda (Beyond).
Yakikukuta inakua ghafla, unakua hujajitaarisha, unahisi umeonewa, kuna mambo hujamaliza, pengine hujaandika Urithi, hapo kwa ukaidi wako unakwenda lakini kwa vishindo, Machungu, Woga mkubwa wakati wa tukio hili la kutolewa (Roho).
Ukiyafata ukayajua unakwenda (Beyond)Unakua wewe Nafsi ilotulia, unapita katika Mauti kama ulivopita kwenye kufungukiwa na (Sex)au Baleghe.
Inakuaje hali hiyo Endelea part 2

No comments:

Post a Comment