Asalaam Aleiykum,
Umeagwa katika ngazi ilopita kwa kuambiwa maneno haya "Hakika Mwenye kupewa Hekima amepewa kheri nyingi sana" Nini Kheri? Kheri ni kinyume cha Shari, kama vile ilivyo (Shida na Raha)sote tunazijiua. Tahadhari sana wakati unaingia kwenye ngazi hii ya sita kwa sababu sakafu yake ya vioo, Na desturi ya Kioo ni lazima uone na uonekane, Unakwenda kwenye shughuli unajipamba kwa kujitizama kwenye kioo ili watu wakuone umependeza, kwa hiyo una kazi mbili ujione na uonekane.
Katika Ngazi hii ya sita katika hizo kheri nyingi unopewa moja yake ambayo kubwa ni hii ya kuona. Nikisema kuona usije kunishangaa na kusema mbona sote tunaona, hapana wewe huoni ila wewe unatizama, ndio maana unayakosa mambo mengi kuyaona. Hivi sasa umepanda kwenye Ghorofa ya Wacha Mungu, Upo katika Ghorofa ya Mawalii, katika ngazi hii kama hupo makini unaweza kuteremka kama utelezi mpaka ngazi ya mwanzo.
Hapa ndipo penye mtihani na mambo makubwa, Mja anafunguliwa kuyaona na kuyajua mambo kwa uwazi, Katika Ngazi hii ndio unapata Kuwaona Majini na Viumbe wengine katika maumbile yao halisi, Unakutana nao moyo kwa moyo, Hapa ndipo yanapopatikana Matibabu ya Maradhi takriban yote, Na kama Mja wa kheri basi wakija wenzio bila ya kuhitaji pesa unawatatulia matatizo yao, hapa wewe umeona bure kwanini unahitaji pesa kwa?
wakija wenzio unawaambia tatizo hili fanya hivi fanya vile utapona, hapa ndipo penye Muono wa mambo mepya kabisa, nikisema kuona nitafanya dhuluma kama sijafafanua kuona huku kukoje?.
endelea part 2
No comments:
Post a Comment