Asalaam Aleiykum,
Hekima ni Mtiririko wa Fahamu zinazotokea kusiko fahamika kwa (Mollah wetu)Usije kwenda kwa mganga kutaka kuitafuta hekima.
Nini Fahamu?Fahamu ni ujuzi wa ithbati wa jambo au mambo yenye kuthibitika, (Mfano)kama sasa hivi unavojijua uko macho, Na ukiwa umelala unakua hujijui huna Hekima, Na tafauti yako na mwenye Hekima kuwa wewe umelala lakini upo macho, Na yeye yupo macho ila keshaamka mwanzo, hiyo ndio tafauti yenu.
Huyo mwenye Hekima kapanda ngazi mapema, na wewe unaweza kupanda lakini inabidi tukuamshe mapema(Salaah Salaah)tukutikise mabega wewe amka kuna kitu Hekima na wewe ukipate, Upo kwenye ngazi ya tano umejaa mapenzi na hekima inaaanza kutumika, hutomkuta mwenye hekima kutumia maguvu, wakati wote anapata zawadi za hekima kutoka kwa Mollah wake na yeye anazitumia kwa ajili ya viumbe wenzie, kwa ajili ya kuwaita kwenye hekima, kuwashauri kwa mambo ya kheri, penye matatizo yeye huingia kuyatatua, penye ugonvi yeye huwa wa mwanzo kupatanisha, matendo yake yote yanashikana na dalili za kheri.
Katika Ngazi hii mwenye Hekima anajua kwa yakini kwamba matatizo, maradhi na madhara yote yanatokana na kwenda kinyume na mpangilio wa sheria za Mwenye enzi Mungu.
Sasa kwa kuwa keshajua anatumia muongozo utokao kwa Mollah wake, Na hiyo ndio maana ya sisi kuomba kwetu (Yaa Rabb)tupe Elimu na Hekima itokanayo kwako.
Kumbuka upo katika Ngazi ya 5 na matarajio yangu ushafahamu nini kusudio la darsa hii ya Ngazi saba za Roho. Na kama hujafahamu hizo (Ngazi)saba ni (Phase)ya Umri wako unopita au niseme mpito wa (Tabaka) la Maisha yako, Sasa kwa wale ambao wanapita katika mpito huu huku wamelala basi hata wakifikia Umri huu wa kupewa Hekima bado wao hawajui, hawataki, wabishi, hawawezi kuwacha. Na wakitaka yao basi utasikia wanakwenda kwa (Zee la Hekima)kuchukua ushauri, Unalijua nani zee la (Hekima)?ukisikia zee la hekima ni mganga, watu wengi siku hizi huko ndiko walikohamia hususan Waumini.
Sasa Mwenye enzi Mungu anatwambia nini kuhusu Mja Mwenye Hekima (Sura ya Luqman aya ya 12)
وَلَقَدۡ ءَاتَيۡنَا لُقۡمَـٰنَ ٱلۡحِكۡمَةَ أَنِ ٱشۡكُرۡ لِلَّهِۚ وَمَن يَشۡڪُرۡ فَإِنَّمَا يَشۡكُرُ لِنَفۡسِهِۦۖ وَمَن كَفَرَ فَإِنَّ ٱللَّهَ غَنِىٌّ حَمِيدٌ
Hakika tulimpa Luqman hikma, tukamwambia Mshukuru Mwenye Enzi Mungu, Na atakaye shukuru, kwa Yakini anashukuru kwa ajili ya nafsi yake, na atakayekufuru, Mwenye enzi Mungu ni mkwasi(Alojitosheleza)asifiwaye(hana haja ya shukurani yako).
Sasa kwanini unashukuru? unashukuru kwa sababu ya kuona wewe hustahiki kwa hicho ulichopewa, lakini kwa mapenzi ya Mollah wako kakuchagua kukupa wewe, ukiligundua hilo ndio wewe una nyenyekea kwa furaha ya mapenzi kumshukuru Mollah wako kwa kukupa Fadhila na Baraka zake zinazoendelea kukushukia mpaka mwisho wa Uhai wako.
Endelea part 3
No comments:
Post a Comment