Sunday, March 30, 2014

NGAZI SABA ZA ROHO PART 3(NGAZI 6)

Asalaam Aleiykum,

Hakika kwa Mja yoyote alopewa kuona huku basi unakua kwake ni mtihani, ambayo naogopa hata kuitaja asije Mja akadhurika au kuwadhuru viumbe wenzie, ila nakupa mfano mmoja tu halafu siendelei , katika kuona huko unaweza kupewa ukaona kiumbe mwenzio yuko katika hali ya matamanio, Na kama utafanya kitu fulani hawezi kukukatalia amri yako ya kufanya chochote, hilo ndio tatizo lenyewe, huo ndio mtihani uliyopo na mambo mengi katika ngazi hii, ndio maana hawapewi kuona huku watu wengi, ingekua balaa.
Na pazia hili pia anopewa anapewa kwa mujibu wa ukuruba wake na Mollah wake, na wako wanopewa kwa bahati itokayo kwa Mollah pia, ila hao ni wachache sana, Na wengine hupata kuchungulia tu kidogo wakajua baadhi ya mambo na wakaanza kuyatumia vibaya. Ndio utaona kupewa huku kuona mambo ya siri wengine wanageuka na kua watabiri, wanageuka kutenda makosa makubwa makubwa, na wakizuiliwa kuona huku hapo tena wanaanza kutumia viumbe wengine kama majini kuwaletea habari, na Mwenye enzi Mungu anasema katika sura ya (Mulk aya ya 5)
"وَلَقَدۡ زَيَّنَّا ٱلسَّمَآءَ ٱلدُّنۡيَا بِمَصَـٰبِيحَ وَجَعَلۡنَـٰهَا رُجُومً۬ا لِّلشَّيَـٰطِينِ‌ۖ وَأَعۡتَدۡنَا لَهُمۡ عَذَابَ ٱلسَّعِيرِ "
Kwa hakika tumeipamba mbingu (Hii ya dunia)ya karibu kwa mataa, Na tumeyafanya ili kuwapiga mashetani, Na tumewaekea tayari adhabu ya moto uwakao kwa nguvu.
Hao wanoanza kuwatuma kufanya urafiki na majini na kuanza kuwatuma ili wapate habari ndio wanaambiwa wakipanda kutaka kusikiliza wanapigwa kwa vijinga vya moto, (Hapandi mtu ngazi ya sita kwa hiyari yake mwenyewe).
Na ukiwa Mja mwema kwenye ngazi hii unapewa zaidi kuona huku mambo ya siri, Roho inafunguliwa kuona kwa upeo wa juu  katika ngazi hii, na huyo muonaji unamshukia upole na ukimya katika nafsi yake, na hawi tena mwenye kuonja dhiki wala mateso, na hapo anasubiri kuipanda ngazi ya saba ambayo tutaimalizia wiki ijayo.

No comments:

Post a Comment