Asalaam Aleiykum
Hakuna kitu ambacho Mwanaadamu anakua karibu na Mollah wake kama wakati wa kuomba Dua, Maisha yako yote yamezungukwa na Dua Tupu, na hata hiyo Sala yenyewe ni Dua. Na Jambo la Dua lina seheme mbili, Ya kwanza ni ile ulopangiwa kutoka kwenye Quraan na tulofundishwa na Bwana Mtume s.a.w, Na aina ya Pili ya Dua ni ile yako mwenyewe(Binafsi) Lazima Mja ufanye jitihada ili upate ukuruba wa kuwasiliana na Mollah wako, ufanye Ikhlas na ukweli mtupu katika maombi yako, ukileta (Carbon copy) ya Dua unakua hupati faida yoyote, unachoambulia Aamin tupu, faida anapata Sheikh na makanzu yake, sababu yeye ndio anotoa moyoni, zengine anajiombea yeye wewe unaitikia Amin sababu hujui kiarabu, na hata ukijua kiarabu unakijua kukisoma lakini hujui maana, kwenye kuomba pesa unaomba upewe elimu, kwenye kuomba pepo wewe unajiombea Moto hivi ndivo inavokua, unachukua dua za zamani kujiombea mambo mepya, unasahau kuwa Mollah wako ndio aloumba hiyo Lugha unayoongea, kwa Lugha yoyote utakayoomba yeye anakusikia na atakujibu maombi yako, huna haja tena kuomba pesa ukasoma sura ya Zil zal. Dua ni wewe na Mollah wako basi chagua kwa uzuri maneno ya kwenda kuzungumza na Mollah wako ili akuridhie ili na wewe upate kusamehewa, isipokua ile Dua ya pamoja hiyo huna haja ya kupeleka maneno yako acha msomaji akupelekee na wewe itikia Amin.
Kwa hiyo hapa nakupa mfano wa vipi utajitupa kwa Mollah yako na maneno ya unyenyekevu mpaka Malaika wajiunge na wewe kuitikia Amin.
"Ewe Mollah wangu natanguliza kwa shukurani za kuweza kunijaalia mimi mpaka leo niko Hai nikaweza kupata Muongozo huu wa kusogea kwako nikiwa na matumaini ya kupata Radhi zako ili unisamehe makosa yangu makubwa na madogo, Nilokutendea wewe Mollah wangu pamoja na viumbe wenzangu".
"Ewe Mollah Wangu hakika Wewe ni Shahid wa yote niloyatenda kwenye Umri wangu, Na mimi sasa nimefika mahali sina mategemeo yoyote ya kupata Shufaai isipokua itokayo kwenye Dhati ya Uwezo wako, Na kama ukiniacha katika hali hii nilo nayo, basi Mollah wangu mimi sina matumaini ya kuweza kuepuka Adhabu zako, Na mimi Mollah wangu sina kifua cha kuchukua adhabu zako zenye mchungu yasioelezeka, kutokana na khofu nilokua nayo, Na ukomo nilofikia kuwa siwezi kuyatengeneza yale niloyaharibu,basi sina la kufanya ila kukuomba Rehma yako ya kusamehewa inishukie Mja wako mimi kabla ya kukabiliwa na Mauti yangu".
"Ewe Mollah wangu ulonijaalia Kuwa, ikisha Nikawa, Nakushukuru kwa Rehma hii ya Uhai, Ila nina huzuni kwenye moyo wangu ya kujua sijawa kama ulivoniamrisha niwe, Na sasa naona kila siku zikizidi Mitihani inaongezeka, Na wasi wasi wangu mimi majawabu yalo mazuri yanazidi kupungua, Basi Ewe Mollah wangu Mie Kiumbe chako Nimetenda mengi ya kukukera Wewe Mollah wangu pamoja na Viumbe Wenzangu, na kwa hilo mimi sina shaka nalo, pia mimi nimedhulumu nafsi yangu pamoja na za Wanaadamu wenzangu basi nakuomba Mollah wangu Nipe mimi zawadi ya kunisamehe kama vile ulivonipa zawadi ya Uhai".
Endelea part 2
No comments:
Post a Comment