Asalaam Aleiykum
"Ewe Mollah wangu" Wewe ni Mwenye kunijua udhaifu wangu, Wewe unayajua niloyafanya kwa Dhahir na Siri mengine nayakumbuka na mengine nimeyasahau, na wakati nikiyatenda Mollah wangu ulikua ukinistiri, lakini nina hakika yamehifadhiwa katika kitabu chako kisichofutika jambo lolote, Na mimi sasa nina khofu siku hiyo nitakaposomewa mambo yangu na yakaonekana hakika yalo mabaya yamezidi kiwango, na siku hiyo sina hukumu inayonikabili isipokua kuingia katika "Gereza" La Jahannam na kukabiliwa na adhabu yako ya Moto, ntakua na hali gani wakati "Joshi"la vuke la moto linaniziba pumzi.
"Ewe Mollah wangu" mimi sina subira kwenye machungu ya Jino linaponiuma seuze huo moto wako utakaponiunguza ikawa ngozi inakabili hasira za moto huo nitakua na hali gani Mollah wangu bila ya msamaha wako.
"Ewe Mollah wangu" Wewe ndie ulienionesha mimi katika kitabu chako kitukufu mfano wa kusamehe na ukawasamehe Mitume yako kwa makosa walokutendea, "Ewe Mollah wangu" Wewe ndie uliyempa Nabii Adam a.s muongozo wa maneno ya hekima ili kuweza kuomba msamaha utokao kwako alipopinga amri yako, na ukamjaalia moyo wa majuto ulojaa khofu na unyenyekevu, Basi na mimi Mollah wangu nimezipinga nyingi katika amri zako kubwa na ndogo na sasa umeniletea fahamu kuyajua makosa yangu nakuomba Yaa Raab nisamehe makosa yangu uniridhie kiumbe chako na uyakubali majuto yangu ya kweli, "Ewe Mollah wangu ikiwa Nabii Adam a.s kaamrishwa atoke peponi kwa kupinga amri zako, nini hali yangu mimi nisofikia hata chembe ya waja wema, kwa hilo Mollah wangu nahitaji msamaha wako, Nahitaji unijaalie moyo wa kukuogopa na kukupenda wewe pekee Mollah wangu, Na wala usinipe mie mbadala wa mapenzi hayo nikawa napenda kitu chengine.
"Ewe Mollah wangu" hakika wewe ndie uliyemsamehe Nabii Musa a.s pale kwa bahati mbaya alipomuua mtu na ikisha ukamsamehe, Na mimi Mollah wangu pengine nimedhulumu nafsi nikiwa labda kiongozi, au kwenye madaraka yoyote au kwenye chombo chochote nikasababisha kiumbe chako kupoteza maisha yake, Mollah wangu najua labda nimeshiriki kwa njia moja ama nyengine nikiwa kwenye kundi au chama kudhulumu viumbe vyengine kwa kupoteza maisha yao au kuwakatili furaha za Roho zao,basi nanyenyekea Mollah wangu kuomba Toba itokayo kwako, nisamehe Mollah wangu.
"Ewe Mollah wangu" Ewe Mollah wangu Nabii wako Daud a.s alifanya kosa la kumpeleka Jeneral wake vitani kwa kutaraji akifa amuoe mkewe, Mollah wangu ukampelekea Malaika wawili walopindukia ukuta na kisa cha kondoo 99, alipogundua Nabii Daud kafanya makosa alianguka na kusujudu kuomba msamaha, na Wewe Mollah wangu ukamsamehe, Mollah wangu na mimi kiumbe chako nimefanya hayo na zaidi ya hayo, na sasa Mollah wangu najitahidi na mimi kusujudu nikitaraji na Msamaha utokao kwako Weye Mlezi wangu nakuomba unisamehe.
Endelea part 3
No comments:
Post a Comment