Asalaam Aleiykum
Unaijua tafauti ya watu wa Ulaya na Africa katika kupanda Mti? Ni ile ya Watu wa Ulaya kuupanda Mti kwa kutumia Ngazi na kuvaa makofia ya kuwakinga na Ajali, Lakini Africa wao wanaupanda bila ya kutumia chochote, hawaogopi hata Ajali, wakivunjika mguu kwao sawa, hata wakifa pia kwao sawa, sasa kwanini ikawa hivyo kwa sababu bado wanaishi kwa Imani iwe yoyote ile lakini (Still) wana Imani fulani inayowafanya hawataki (Gurantee) hawataki(Insurance) na kwa Imani yangu mie nahisi hivyo ndivyo unavotakiwa kupandwa mti, lazima uhisi umekuchuna mapaja, umekukwaruza kwaruza damu zinakutoka, halafu ukisha uzoea mti unakua rafiki yako, hata Tawi likitaka kukatika linakupa taaria mapema, na hivyo ndio ulivo Mti wa Ibada lazima upate tabu, lazima uhangaike, uamke Alfajiri, ufunge Ramadhan ukumbatie mayatima, utumie kilicho chako kwa kukitoa buree umemkuta mtu kakaa unampa, na huku huna (Gurantee)kama ukifika kileleni utachuma matunda au itatokea nini? lakini ukianza kuvaa makofia na ukaweka ngazi ina maana unataka uhakika usianguke na hivi na vile.
Elewa Ulimwengu huu umeumbwa na Athari za Ajali, wewe mwenyewe huna (Gurantee) unaweza kuwa umeficha maradhi, unaweza kufa wakati wowote, Ndio maana unatakiwa ufanye juhudi ya kuupanda Mti huu wa Ibada, Na huu ndio wakati mzuri wakuuzungumza Mti huu wakati umo katika tawi moja wapo la kufunga mwezi wa Ramadhan.
Mti wa Ibada Ukoje?
Mti wa Ibada ni mkubwa sana na hauna kikomo kwa urefu wala mapana, Sababu Mti huu una matawi mengi na matunda mengi, Na hapo ndio unatizamwa mpandaji unataka kupanda kufikia Tawi gani, jee una (Stamina) ya kuupanda Mti huu. (Stamina) utaipata wapi wakati unaogopa kupanda Mti huu wa Ibada, unataka uwekewe ngazi iwe ushafika Juu bila ya tabu yoyote, na huku unauliza mti wenyewe unaitwaje, na sisi kila ukituuliza tunakwambia Mti wenyewe ni unaitwa (Mdini) Dini, usije ukadhani nimesema (Mdimu).
Na cha kusikitisha zaidi wengine wanaukimbia Mti huu hata kwenye mwezi wa Ramadhan, tumo ndani ya Uislam na kanzu zetu nyeupe, na saum zetu tunajidai zinapanda, vipi saum hizo zitapanda wakati tunasutwa, tunaambiwa kwenye sura ya (Maun)
أَرَءَيۡتَ ٱلَّذِى يُكَذِّبُ بِٱلدِّينِ
Je Umemuona yule anayekadhibisha Dini.
Aya imesema vizuri sana, kwani ingesema unamjua ungekua ubishi mkubwa, utajuaje kama mtu anatoa au hatoi, ana amini au haamini kama akhera ipo? ndio ikasemwa umemuona, kwa sababu unasali nae, pengine jirani yako, mnakwenda darsa pamoja, kila siku mnaona, wewe unamuangalia na yeye anakuangalia, nini kinatokea katika hicho unacho kiona.
فَذَٲلِكَ ٱلَّذِى يَدُعُّ ٱلۡيَتِيمَ
Huyo ni yule anomsukuma yatima.
Vipi anamsukuma yatima? kukisukuma kitu lazima uwe karibu nacho, mayatima wapo mitaani tunaishi nao, maana yakua yatima wako chini ya uwezo hawana wazazi, zaidi ya hilo wewe mwenye uwezo unawasukuma kwa kuwaacha usiwasaidie, wanakukera kwa hiyo unaamua kuwasukuma shimoni wazidi kuteseka kwa dhiki na madhila ya Roho, kwa sababu wanawaona watoto wako mara wana baskeli, mara wana gari, mara wana suruali mpya mara wanakula (Ice Cream)huko ndiko kuisukuma Roho ya Yatima
Endelea part 2
No comments:
Post a Comment