Siku moja yalikuja maswali katika ukumbi wa Zanzinet, maswali haya yalitupwa ukumbini kwa anaetaka ajibu, kwa kuwa mie sina dasturi ya kujibu swali nisiloulizwa kwa hiyo nikawa naangalia majibu ya watu yanavotiririka, lakini kuna swali moja kati ya hayo yaloulizwa sikuliona jawabu lake ndio nimeamua kwa faida ya wasomaji wangu nilijibu ili msipate kuyumbishwa katika msimamo wa dini yenu, na hususan wakati naandika mada hii kuhusu (Motoni).
Swali lenyewe lilikuwa namba 3 na liliulizwa hivi:"Kwanini mtu amefanya dhanbi kwa muda wa miaka yake (70)hapa duniani akatiwe motoni milele(Daima)Muulizaji anasisitiza kusema kuwa hapa Allah atakua sio muadilifu, kwa sababu mtu amefanya madhanbi miaka (70)na kutiwa motoni milele,haiendani kihukumu?".
Jawabu:Naam sijui Muulizaji alikua Mwanasheria, au Mtu wa dini gani, au alikua Mtu asoamini Dini ningepata kujua Mtu wa aina gani ningemjibu kutokana na Imani alokua nayo, ningemtosheleza kwa kadiri ya ujuzi wake ili apate kuridhika, kwa kuwa katika hilo swali katajwa Allah basi nachukulia labda muulizaji Muislam lakini ana shaka tu na Imani yake, na hivi ndivo wengi tulivo, hatuna tafauti na wale wasoamini, utaona mmoja anasema hakuna Mungu hana ushaidi wa kuthibitisha hayo, na wewe unosema yupo una shaka kwa kuwa huna ushaidi na huwezi kutoa ushaidi, hutaki kutafuta ushaidi ndio maana na wewe japo umekubali lakini kuna shaka katika nafsi yako.
Swali limeanza kwa lugha ya kwanini? ndani ya mwanzo huu kuna(Challenge)ya kubeza(au muulizaji ana kiburi)pengine cha elimu nk, Anasema Mtu amefanya Dhanmbi miaka yake (70)Napenda Muulizaji aelewe hiyo miaka (70)sio yako ni ya Mwenye-enzi-Mungu, Alokupa zawadi ya kukuleta hapa Ulimwenguni, Akakupa Afya na kukutengenezea kila kilo chema katika dunia hii, Ikisha akakupa fadhila kubwa za kukufanya wewe kuwa mwanaadamu na kukupa fahamu," فَأَلۡهَمَهَا فُجُورَهَا وَتَقۡوَٮٰهَا "(Shams aya ya 8)"Ikisha akaifahamisha uovu wake na wema wake",
Wewe sio tembo, au Punda milia, wewe sio Kima mtini wewe mwanaadamu Mollah wako amekukirimu kitu adhimu, kakukabidhi fahamu unajua hili baya na hili jema.
Sasa inakuaje atiwe Motoni milele, Hapa Mwenye-enzi-Mungu atakua sio muadilifu? Mie simlaumu Muulizaji akili za kibinaadamu zimejaa(Bussiness)au hajazama deep kwenye fahamu zake akajua kutafautisha mambo. Imempeleka shauku yake ya kupanga kuwa hapa Duniani si nina fanya miaka 70 na huko basi angalau nilipwe nikakae humo motoni miaka 70, hiyo ndio itakua haki vyengine vyovyote itakua sio Uadilifu, naonewa na huyo Hakimu hatendi haki kabisa.
Jee wewe unajiamini kukaa Motoni japo kwa siku moja, kwani hutizami nafsi yako pale unapolala, Au kakae pangoni bila ya saa au kuona jua, jee hukusoma Sura ya(Kahfi-aya-ya-11-17-18-19)basi kama hujafanya hivo kimbilia upesi ukajue hiyo miaka 70 itakuaje na milele itakua vipi wakati au saa(Time)ikipotea.
Nini (Time)muda, ni kitu kilichopangiwa hapa ulimwenguni lakini katika ufalme wa Mollah wako hakuna wakati, (Time na Space)ni kitu kimoja ndio maana utaona wanasayansi wana hesabu dunia imeumbwa miaka (Billioni)kadhaa halafu hawawezi kuendelea kwa sababu (Time na Space)zimeshakomea hapo, vimepotea kabisa vimekua (Single unity)na ndio wewe ukifariki (time)inapotea kama vile ukiwa umelala unajua sasa hivi saa ngapi?,ndio maana ukaambiwa kiama kitakuwepo, wewe una shaka nacho unaona hee watu wote walokufa miaka yote lini watafufuliwa kwa sababu wewe unahesabu muda(Time)lakini kwa Mollah hakuna (Time).
Sasa ikiwa hakuna muda(Time)sasa jee utiwe Motoni mwaka mmoja tu una ghali gani, fanya iwe masiku jee unaweza kustahamili Joshi la Moto wa Mwenye-enzi-Mungu, na kama unajiamini basi wacha nikujulishe kwanini ikawa milele, vipi utaona kwako wewe daima, pengine unalipwa hiyo hiyo miaka yako sabini lakini unaweza kuchukua kishindo chake.
Pata mfano hapa ulimwenguni, Polisi wanakutafuta unasubiri gari ije kukuchukua, umejiona unavokua tafrani, sasa karibu ndio utakamatwa na hivi na vile kutwa unatizama saa lakini gari ikitokea unasahau kila kitu, na ikiondoka ndio unacheka na hivo ndio itavokua kwenye huo (Moto)basi tahadhari sana na hiyo miaka yako 70, ogopa sana hukumu ishatolewa na wewe unatakiwa ukakae hiyo miaka 70 na wakati huo (Time) au muda ushapotea ndani ya dhiki ya huko motoni ndugu yangu kwako inakua ni kama milele katika tanuri la Motoni, Namalizia kwa kusema Haikmu ni Mwadilifu, lakini adhabu iumizayo ndio utaona umekaa milele, kwani nafsi ya mwanaadamu haistahamili dhiki, na mfano unaona hapa duniani unaona vipi ukiwa na dhiki unavokua na ukiwa na furaha unavokua, tizama katika kimoja hicho (Time)inapotea nakuachia ukichunguze mwenyewe ni kipi hicho, Na ukisha kukijua basi nakushauri kikumbatie usikiwache abadan fanya jitihada mpaka unatoka roho yako uwe umekidhibiti kaa ukijua kina faida kubwa ya milele na mfano wake hausemeki. Sasa tunaingia katika Mada yetu tulokusudia (Alama za watu wa Motoni)endelea sehemu ya Pili-Part 2
No comments:
Post a Comment