Asalaam Aleiykum,
(Wanapoachana) wawili hawa basi utaona lazima cha pili kinachofatia ni Maradhi na hili litizameni sana isiwe mimi nasema na nyinyi mnakubali na afanye mtu uchunguzi, pengine wewe yamekukuta na sasa hutaki yakukute tena, Sasa kwanini Maradhi yanafatia? Sababu kubwa ni Sumu ya chuki imeshaingia na sumu ni lazima ilete uharibifu, na sumu zenyewe zipo za aina nyingi na uingiaje wake uko wa kila aina nakupa mfano mmoja(tazama mtu akikwambia unaumwa na mguu, unacheka, akikwambia una ugonjwa wa ngozi, unafurahi, lakini nini kinatokea akikwambia wewe mwenda wazimu)? hali inayokukuta hapo ndio huo mwanzo wa hizo sumu ninazo zisema, sasa jichunguze yale ni maneno tu yamesemwa hajakugusa wala kukusukuma kakwambia tu wewe huna akili jitizame hali unayokua nayo.
Nayazungumzia mambo haya kwa kuwa jamii imezama katika janga hili na tunaendelea kuangamiza maisha yetu kwa kuharibu mapenzi baina yetu, Madhara ya sumu hizi za chuki yana tabia za kujikusanya, na wengi wetu hatujapata taaluma ya kujisafisha, hatujui vipi kukamata jambia la mapenzi na kulichana pazia la chuki, na hakuna kiharibifu kikubwa cha mwili wa mwanaadamu kama chuki na hili sababu kubwa ni kutokana na mambo mengi ya maishani mwako, kama vile umedhulumiwa katika biashara, au umekatiliwa kupewa kitu fulani, au watu hawataki kushirikiana na wewe, hapo unaanza kujenga chuki kidogo kidogo moyoni mwako, au pengine udogoni wazee walikupuuza na wakakutekeleza, moyoni unabeba chuki, na ukibeba chuki kwa muda mrefu inaanza kutoka nje kwani maradhi mengine hayachukui kukaa muda mrefu, na kama nilivosema (Chuki)ni hayo hayo mapenzi, na mapenzi yanatabia lazima ugawe, aidha iwe kwa mkeo au wanao, iwe kwa ndugu au watu baki, basi na chuki inakuchukua katika safari hiyo hiyo inataka nayo itoke, na hakuna njia ya kupungua kwa chuki ila kwanza inahamia kwenye (Ulimi)kabla ya vitendo ni lazima ipitie kwenye ndimi.
Ndio utaona Ishara nyingi zinajitokeza mtu labda hayuko katika kundi lako, unamchukia, labda hayumo katika chama chako basi bure unamchukia na unaanza kupita kumsingizia mambo mabaya tele kwa tele, Unaanza kumtukana bila ya sababu, na ukiulizwa sababu pengine huna lakini unasumbuliwa na maradhi ya chuki. Yanapita yakikutoka maneno makubwa makubwa eti kwanini hajakusalimia,au kwanini anaringa, sasa anoringa yeye, wewe kinakusumbua nini?zinakupanda hamaki bure, lazima una matatizo jifanyie uchunguzi. Hivi karibuni Wanasayansi wametoa (Report)yao ya uchunguzi habari hizi zimetokea kwenye (Website Realbuzz.com)wanasema ukisema uongo au kuzua jambo japo dogo la masikhara tu basi linasababisha kuumwa na kichwa,unapata ugonjwa wa koo na mengi n.k sasa nini habari yako wewe unolala na kuamka na chuki.Sasa vipi chuki inakuumiza endelea part 3
No comments:
Post a Comment