Asalaam Aleiykum
Maskini:
Na Maskini hali kadhalika atahadhari na yeye kuwa na Alama ya Motoni kwa kupenda utajiri, kuwa na tamaa ya kudhulumu, kupita huku na huku kufanya jitihada za dhuluma ili atajirike, kupita kuomba madua ya kutaka upewe utajiri kama walivofanya maskini walopita na mpaka hii leo watu hawaridhiki, wana hamaki kwanini hakupewa utajiri, inakuaje fulani hafanyi jitihada yoyote lakini akishika biashara anapata faida yanakuaje mambo haya mbona haitendwi haki hapa, mnaambiwa nini maskini kuhusiana na kadhia hii sura ya (Tawba aya ya 75)"وَمِنۡہُم مَّنۡ عَـٰهَدَ ٱللَّهَ لَٮِٕنۡ ءَاتَٮٰنَا مِن فَضۡلِهِۦ لَنَصَّدَّقَنَّ وَلَنَكُونَنَّ مِنَ ٱلصَّـٰلِحِينَ "Na miungoni mwao wako walomuahidi Mwenye-enzi-Mungu akitupa fadhila(Utajiri)zake tutatoa sadaka na tutakuwa miongoni watendao wema"
Asipite mtu akachukua dhamana hiyo, utajiri hauna dhamana unaweza kugeuka vyovyote ukapotea kabisa, kama yule(sahaba aloombewa na Bwana Mtume s.a.w akaupata utajiri ikisha akageuka na kukataa kutoa zaka, kama aya inayofatia katika sura hiyo inavoeleza:(aya ya 76)" فَلَمَّآ ءَاتَٮٰهُم مِّن فَضۡلِهِۦ بَخِلُواْ بِهِۦ وَتَوَلَّواْ وَّهُم مُّعۡرِضُونَ"
Na alipowapa hizo fadhila zake, walifanyia ubakhili na wakageuka,(na wanaendelea)kugeuka.(kukanusha kabisa)Atahadhari mtu asije kupewa ikisha ukawa mtihani kwake ikawa Alama hili ndio kama lile nililotaja la (Mfanya Biashara) inakuaje ukisha kupewa hiyo mali "Ewe Maskini"tahadhari sana kuwa na choyo na wale walopewa utajiri, pengine Mollah kakupenda mja wake kukufanya maskini hebu ridhika usije kuwa kama walotajwa katika aya ya (77)
"فَأَعۡقَبَہُمۡ نِفَاقً۬ا فِى قُلُوبِہِمۡ إِلَىٰ يَوۡمِ يَلۡقَوۡنَهُ ۥ بِمَآ أَخۡلَفُواْ ٱللَّهَ مَا وَعَدُوهُ وَبِمَا ڪَانُواْ يَكۡذِبُو"
Akawalipa(Adhabu)ya (kuwatia) unafiki nyoyoni mwao mpaka siku ya kukutana naye(Mollah wao)sababu ya kukhalifu kwao waliomuahidi Mollah wao na kwa sababu ya kusema uongo.
Usije ukawa katika kundi hilo, jaribu kufuta alama hiyo ya kutamani utajiri mpaka ukawa tayari kufanya chochote lazima utajirike, anakwenda mtu kwa mganga kutafuta cheo au utajiri, kwa majungu yeye hasemeki, akipewa kidogo utaanza kusikia milio ya funguo na mwendo unabadilika, jitihada zote afanyazo ni kutafuta vipi atamsahau Mollah wake, vipi atamshirikisha, na subiri apewe cheo uone mambo. Basi fanya juhudi kama unalo Alama hiyo uanze kuifuta, hakuna siri kubwa kama ile ukiridhia umasikini wako basi Mollah wako anakuteremshia utajiri wa kiroho na unaishi kama mfalme kwenye ulimwengu huu, omba sana upate siri hiyo mpaka wanaadamu wenzio watakushangaa vipi huyu hana kitu lakini mbona ana furaha, mbona hana nguo lakini msafi, mbona ameridhika na kadari ya Mollah wake, ana amali gani huyu, kwako inakua ukipata sawa, ukikosa sawa huna malalamiko, basi ukiridhika kikweli kweli kuna siri Mollah wako atakupa utaijua baina ya wewe na yeye, mie nakupa kidokezo na huu ndio ukumbusho nakuletea ili upate kufanikiwa.
Abdulla Baja
No comments:
Post a Comment