Asalaam Aleiykum:
Inaendelea:
Mambo yenyewe mwanaadamu huna hata uwezo nayo ni haya, la kwanza linatokea hulioni, lakini la pili linatokea unakua mwenye kuliona lakini yote hayo yanatokea wewe ukiwa si mshiriki wake, kwanza kuzaliwa huna maombi katika swala hili huwezi kuchagua baba yangu au mama yangu awe fulani, Na la pili siku ya kufa kwako, huna dua au chengine chochote cha kuweza kuzuia jambo hili, zawadi hizi mbili anakupangia Mwenye-enzi-Mungu, ndio maana ukaambiwa unapofika umri wa miaka (40)(katika Qura'an) nishukuru mimi na wazee wako wawili, Sasa ikiwa wako hai unaambiwa uwashukuru vipi leo wanaondoka katika ulimwengu huu wewe unakatazwa usiwashukuru,usiwaombee,usiwasalie na kuwatakia rehma na wewe unakubali kirahisi hebu amka usikubali mtu akukamatie dini yako, dini unayo mwenyewe huyo anokwambia na wewe hamna tafauti, asizuke mtu akakwambia haifai na wewe ukakubali hakuna jambo la kheri lenye makosa kwa Mollah wako, hakuna Dua itakayokuadhibu hebu amka usingizini na muanze kuwaombea Maiti zenu, elewa kufa hakutokei siku zote ni nadra sana ingekua inatokea siku zote si mngekua mshakwisha, wazee wenyewe wawili, watoto wenyewe wawili basi hata hao unaondoshewa hii fadhila ya kuwasalia na kuwatakia maghfirah na wewe unakubali, siku hii ya leo wanakuhitaji sana, siku hii ya leo ndio siku yako ya kufanya (Communion)na alo wako siku zote ulikua unadharau yupo ntazungumza nae, yupo hana neno tukipata nafasi tutazungumza sasa leo ndio kaondoka milele na wewe mgonjwa wa kusahau hivyo utamkumbuka tena baada ya leo usijidanganye muombee maiti yako leo kabla ya kesho wala asikwambie mtu haifiki dua yako ndio inafika hassa kwani ukiomba wewe ndio unaomba kwa hiyo(Communion-heart to heart)kwanini unamwachia mtu mwengine amuombee maiti yako.
Soma maudhui ilo pita(Umuhimu wa dua)utajua katika makutano ya (Roho)hakuna umbali wowote baina ya muombaji(Talib wa Mattlub)anaeomba, tena tahadhari sana na watu hawa hawakutakii mema au wao wenyewe hawana ujuzi wa elimu ya (Tawhid)wakapata kujua nini kina tokea wakati mwanaadamu anakata (Roho)au masaa kadhaa baada ya mtu kufariki kwake, sasa ni kinatokea?anahadithia Umm Salamah r.anha"Alikuja Bwana Mtume s.a.w wakati Abu Salamah anakata roho, akamfunika macho yake, ikisha akasema roho inapochukuliwa na macho yanaifata, walozunguka pale wakaanza kulia kwa mayoe machozi yana watoka wakaanza kusema maneno, akasema Bwana Mtume .s.a.w " msiseme chochote isipokua kitu kizuri, kwani Malaika ni wenye kuitikia Amin kwa kila mnachosema, ikisha akaanza kuomba dua""akasema Ewe Mollah wangu msamehe Abu Salamah, mnyanyue darja yake, muweke katika kundi la waja wema, mjaalie mrithi mwema alobakia, mpe msamaha yeye na sisi tulobakia".
Sasa ikiwa Bwana Mtume s.a.w kenda kwenye nyumba akaanza kuomba dua vipi leo sisi tunakwenda nyumba za misiba mpaka tunaondoka hata dua hatuombi wapi tumeyapata mafunzo haya hili nakuachia mwenyewe, Enyi ndugu zangu tukifikwa na misiba tusijizuie kulia au kuhuzunika Mtume s.a.w kafanya hivyo kafanya mbele ya masahaba zake, jueni kulia ni hiyo(communion)kulia ni Imani kulia ni hisia ndani ya kilio ndipo hapo zinapotokea dua, kulia ni huruma na ukilia basi jihesabu wewe hasa ndio mtu wa Mollah, Ahadithia Anas r.a alikuja Bwana Mtume s.a.w wakati mwanae Ibrahim anakata roho macho ya Mtume s.a.w yakajaa machozi Abrahman bin Auf r.a akasema hata wewe Bwana Mtume s.a.w unalia, akajibu Mtume s.a.w "Ewe Ibn Auf"ni kutokana na mapenzi na huruma nafanya hivi, ikisha akalia kwa nguvu "akasema"Macho yetu yanatoka machozi hatutosema isipokua kinacho kuridhisha weye Mollah wetu, huyo ndio Bwana Mtume s.a.w. Sasa jichunguzeni nyinyi nini mnafanya nyumba za misiba? mtapata majibu yenu.
Enyi ndugu zangu tukifikwa na misiba msiache nyinyi kuwaombea maiti zenu na kuwasalia kumbukeni nyinyi ni wakaribu zaidi na huyo marehemu, na dua zenu ni kama sadaka kwa vipenzi vyenu vilotangulia, dua zenu ni rehma kwao kwa yule anopokea maombi yenu, Maombi haya pia ni heshima kwa ule mwili ulokuzaa wewe, na huko kuomba kwako dua ni rehma kwa (Roho)ya marehemu awe mtoto au mzee, kumbuka mapenzi alokupa alipokua hai, kumbuka huruma na msaada alokufanyia japo kidogo wakati mnaishi pamoja, kumbuka mema alokufanyia kukuhudumia akisimama na wewe kwa afya na maradhi basi leo astahiki kupata sala yako na maombi yako, jikumbushe mlipokaa pamoja mkala pamoja mkacheka pamoja leo ndio unamtupa kama gunia, hebu jifundishe japo kidogo upate kuufungua moyo wa mapenzi, ujaze huruma msalie hata alokua mgonvi wako apate kurehemewa na wewe upate rehma zitokazo kwa Mollah wako.
Kwanini dua zako zisifike kwani Mollah wako si ndie alio kuumbieni hizo (Redio-Wave)mtu akawepo umbali wa masafa elfu nne ukawa unamsikia, vipi leo uwe na mashaka dua yako haifiki au haifai, Napenda kukufahamisha kuwa dua ndio njia maalumu alokufanyia Mollah wako ili upate kuwasiliana naye, asije akakuwekea mtu yoyote masharti katika jambo hili, Haiwi makosa kumsalia Maiti yako na kumtakia Rehma na maghfirah, Na nyinyi (Mama)zangu mlioko majumbani salieni maiti zenu msikae mkawa mnapitwa na fadhila hizi za kuwaombea maiti zenu.
Sasa napenda nikukumbusheni jambo moja linatokea mbele yenu lakini limefunikwa pazia hivo wewe huoni, akija mtu akakwambia kusalia maiti haifai humuulizi kitu lakini akija mtu akakwambia inafaa unamwambia lete ushahidi!! unajua kwanini? nitakupeni kisa cha Abdi(Jahil)kimetokea katia mji(kumbuka uko katika mambo ya kufahamu basi pata fahamu nzuri ili usije kuhadaika)ilikuaje, alimfata Abdi Jahil ulaamaa mkubwa mwenye kusifika katika ule mji, akamwambia mimi ni taabani kwa aibu, watu wote wanajua sina elimu, wanafahamu mimi mtupu sasa nataka nipate heshima katika hii jamii nimechoka, yule Ulamaa akamwabia unataka elimu au unata ujulikane una elimu(Umesoma)? akasema nataka nijulikane nina elimu, basi akamnongoneza sikioni baada ya miezi kadhaa mji mzima ukawa unauliza hee imekuaje Abdi Jahil kawa hivi siku hizi, watu wote wanamuheshimu haingiliki kwa Ilmu ana siri gani?, anatesa watu namna hivi ,walipomuendea yule ulamaa akamwita Abdi Jahil akmwambia waambie mwenyewe au nitawaambia mimi siri yako, akasema Abdi Jahil nitawaambia mimi mwenyewe,nilivokuja kwa Mualim huyu alinifundisha kitu akanambia (Trick)hii nenda kinyume cha kila kitu utapata umaarufu hakuna njia nyengine, wakikwambia sala ya maiti halali waambie haramu, sio wewe ulo sema haramu wao wanosema halali ndio watotakiwa kuleta ushahidi na wakileta ushahidi na wewe hapo unasoma, akasema ndio imekua kazi yangu kila ninaloambiwa mie nabisha na kwa sababu nabisha nyote mnaniona mie msomi ki ukweli nyinyi nyote mnayeniogopa ndio walimu wangu.Na hivi ndivo tulipofikia kitu chochote unaambiwa lete ushahidi sahihi, na hii ndio hasara kubwa tunasomesha watu bila ya kujijua. Mwisho nakuusieni enyi ndugu zangu tunapofikwa na misiba tuwasalieni na kuwombea mati zetu, fungueni mioyo yenu muungane na yule wenu alotangulia. Na Inshaallah Mollah wetu atapokea sala zetu na dua zetu.
Amin.
Abdulla Baja
No comments:
Post a Comment