Saturday, September 22, 2012

MADHARA YA MJA MWENYE CHUKI -PART -1

Asalaam Aleiykum.

Shukurani zisizo na upungufu anastahiki yule mwenye kutujaalia mapenzi baina yetu, Ikisha akatujulisha hili tukio la mapenzi linasababishwa na yeye na hilo ni katika Rehma zake anazo tuteremshia kila siku katika maisha yetu. Huku kuumbwa kwetu wanaadamu ni mapenzi yake Subhanna, hii afya alotupa na kuweza kuvuta pumzi, kulala kwetu na kuamka ni moja katika ishara za mapenzi yake kwetu sisi waja wake, unatakiwa Mwanaadamu kitu cha mwanzo unapoamka ushukuru kwa neema hizi.
Limezama neno hili la mapenzi kwenye nyoyo zetu mpaka imekua desturi yetu katika lugha kila kitu tunatumia hichi unakipenda au hukipendi, Na imekua bora kwetu sisi hatutumii neno(Umechukia)kwani ukitumia neno umechukia unakua umeshakwenda upande wa pili(Ambao)ni kusudio la Mada hii.
Unaposema jambo au kitu hukipendi jichunguze unabakia sehemu ya kati(Netural)unakua hukipendi lakini hukichukii, kwa hiyo inaonesha chuki ni sehemu ya pili ambayo sasa tunaingia ili tupate kuijua na kuifanyia kazi tuepuke na madhara yake.
Nini Chuki? Utashangaa nikikwambia chuki na mapenzi ni kitu kimoja lakini kinabadilika wakati inapoingia (Sumu)na hizi sumu zipo za aina nyingi ambapo leo tutachambua japo kwa uchache ili mtu apate kujijua jee yeye ana mapenzi au chuki ndani ya nafsi yake.
Mapenzi ni (Nature)yetu kama ilivyo afya, ndio maana viwili hivi huwezi kuvifafanua, unaona vipo tu na hujui kwanini. Lakini kutokana na kuandamwa kwetu na (Shetani)na vishawishi vilotangulizwa mbele ya macho yetu basi tunaikubali Sumu hii na hapo ndio tunapoanza kuibadilisha neema hii ya mapenzi na kugeuka Chuki. Hebu utizame (mfano) huu wa sumu inavoingia na kuharibu mapenzi, huenda ikawa Mke na Mume wanapendana akapita shetani ghafla akamshawishi mmoja wao kuteleza katika ile ndoa, Na akiteleza mmoja wao basi hapo sumu imeshaingia katika mapenzi na sasa utaona moja kwa moja inageuka kuwa chuki na ama iwe dhahiri au siri ya moyoni lakini chuki ni ile ile, Mapenzi hayabadiliki kuwa kitu chengine(Ukikera Chuki, Ukifurahisha mapenzi).
Tupia macho Marafiki wanavo gombana, Ndugu wanavo farakiana, yote haya yanatokana  hatutunzi Rehma hii ya Mapenzi alotushushia  Mollah wetu. Nguvu hii ya Mapenzi au (Rehma)ni chanzo kikubwa cha maradhi yetu wanaadamu, tizameni vipi watu wawili wakipendana halafu wakija kufarakiana nini kinatokea?
Endelea part 2

MADHARA YA MJA MWENYE CHUKI-PART-2

Asalaam Aleiykum,

(Wanapoachana) wawili hawa basi utaona lazima cha pili kinachofatia ni Maradhi na hili litizameni sana isiwe mimi nasema na nyinyi mnakubali na afanye mtu uchunguzi, pengine wewe yamekukuta na sasa hutaki yakukute tena, Sasa kwanini Maradhi yanafatia? Sababu kubwa ni Sumu ya chuki imeshaingia na sumu ni lazima ilete uharibifu, na sumu zenyewe zipo za aina nyingi na uingiaje wake uko wa kila aina nakupa mfano mmoja(tazama mtu akikwambia unaumwa na mguu, unacheka, akikwambia una ugonjwa wa ngozi, unafurahi, lakini nini kinatokea akikwambia wewe mwenda wazimu)? hali inayokukuta hapo ndio huo mwanzo wa hizo sumu ninazo zisema, sasa jichunguze yale ni maneno tu yamesemwa hajakugusa wala kukusukuma kakwambia tu wewe huna akili jitizame hali unayokua nayo.
Nayazungumzia mambo haya kwa kuwa jamii imezama katika janga hili na tunaendelea kuangamiza maisha yetu kwa kuharibu mapenzi baina yetu, Madhara ya sumu hizi za chuki yana tabia za kujikusanya,  na wengi wetu hatujapata taaluma ya kujisafisha, hatujui vipi kukamata jambia la mapenzi na kulichana pazia la chuki, na hakuna kiharibifu kikubwa cha mwili wa mwanaadamu kama chuki na hili sababu kubwa ni kutokana na mambo mengi ya maishani mwako, kama vile umedhulumiwa katika biashara, au umekatiliwa kupewa kitu fulani, au watu hawataki kushirikiana na wewe, hapo unaanza kujenga chuki kidogo kidogo moyoni mwako, au pengine udogoni wazee walikupuuza na wakakutekeleza, moyoni unabeba chuki, na ukibeba chuki kwa muda mrefu inaanza kutoka nje kwani maradhi mengine hayachukui kukaa muda mrefu, na kama nilivosema (Chuki)ni hayo hayo mapenzi, na mapenzi yanatabia lazima ugawe, aidha iwe kwa mkeo au wanao, iwe kwa ndugu au watu baki, basi na chuki inakuchukua katika safari hiyo hiyo inataka nayo itoke, na hakuna njia ya kupungua kwa chuki ila kwanza inahamia kwenye (Ulimi)kabla ya vitendo ni lazima ipitie kwenye ndimi.
Ndio utaona Ishara nyingi zinajitokeza mtu labda hayuko katika kundi lako, unamchukia, labda hayumo katika chama chako basi bure unamchukia na unaanza kupita kumsingizia mambo mabaya tele kwa tele, Unaanza kumtukana bila ya sababu, na ukiulizwa sababu pengine huna lakini unasumbuliwa na maradhi ya chuki. Yanapita yakikutoka maneno makubwa makubwa eti kwanini hajakusalimia,au kwanini anaringa, sasa anoringa yeye, wewe kinakusumbua nini?zinakupanda hamaki bure, lazima una matatizo jifanyie uchunguzi. Hivi karibuni Wanasayansi wametoa (Report)yao ya uchunguzi habari hizi zimetokea kwenye (Website Realbuzz.com)wanasema ukisema uongo au kuzua jambo japo dogo la masikhara tu basi linasababisha kuumwa na kichwa,unapata ugonjwa wa koo na mengi n.k sasa nini habari yako wewe unolala na kuamka na chuki.Sasa vipi chuki inakuumiza endelea part 3


MADHARA YA MJA MWENYE CHUKI-PART-3

Asalaam Aleiykum,

Chuki inakuumiza kwa (mfano)huu, Tizama akiingia mtu unayempenda inakuaje? na akiingia mtu unayemchukia inakuaje?, akiingia ambaye unayempenda (Nothing change)hakuna kinacho badilika, lakini jitizame ndani ya nafsi yako anapoingia yule unaye mchukia ghafla (inside)unabadilika, nini kinacho badilika ni (Chemical)katika mwili wako zinasumbuka, hazijui nini kimetokea, dakika iliyopita ulikua unacheka machozi yanakutoka kila kitu (Normal)mara kaingia mtu unamchukia (Brain)unaimrisha sasa peleka (Chemical)za hamaki hapo una (Confused)system yote unaanza kujiharibu mwenyewe ndani kwa ndani, maana huwezi kusema wala kupigana unabakia kujiumiza katika nafsi yako mpaka huyo uno muona adui akiondoka unakua umeshajichoma vya kutosha kwa (Chemical)mbili moja ya kucheka na nyengine ya hamaki mwilini mwako.
Na hapo ndio tena unaharibu mapafu na moyo, unaharibu tabia na hulka yako, ukitizamwa machoni kwa wenye kujua wanafahamu sasa wewe mgonjwa, chuki inakula kidogo kidogo sababu kubwa una ishi na sumu katika viungo vyako, utaanza kuchukia kila mtu mwisho mpaka wewe mwenyewe unaanza kujichukia, na maradhi yakizidi tena yanahamia kwenye viungo, mara hichi mara kile, ukifikia hali kama hiyo sasa unahamia katika darja nyengine unaanza kufitinisha watu, unaanza kuitapakaza sumu hivi na vile, unakua bingwa wa kuzulia watu uwongo, mambo yako yote yanakua ya kishetani, hapo ndipo viungo husema kuwambia (Ulimi)"Ewe ulimi, wewe ni kiongozi wetu basi tufanyie ihsani ya kutupunguzia adhabu, kwanza kwa kujichunga wewe nasie tufatie" na ishara za kuanza kwa kukusanyika kwa chuki ni kama vile "Ukiona mtu anakusalimia humjibu, basi chuki inaanza, ukimuona  mtu halafu unamgeuzia uso,chuki inaanza, unamsema mtu mambo ya uongo,chuki inaanza, unamnunia mtu bure, chuki inaanza,ukiona mafanikio ya mwenzio yanakuuzi, chuki inaanza, ukiona tabu kumsifia mwenzio japo anastahili, chuki inaanza na mengi mengine nyie mnayajua. Sasa ikiwa ishara hizi zote mtu kasha zigundua na bado hataki kujitakasa basi chuki inamchukua  na kumuweka katika kundi la (Shetani)na ukiweka katika kundi hili basi wanaadamu inabidi wapate kinga kutoka kwa Mollah wako kama inavosema sura ya(Naas)kwa sababu mambo haya yamo kwenye nafsi yako basi ni lazima ashtakiwe yule mwenye kumiliki hiyo nafsi.
"قُلۡ أَعُوذُ بِرَبِّ ٱلنَّاسِ"
Sema najikinga kwa mlezi wa wanaadamu(watu)
" مَلِكِ ٱلنَّاسِ"
Mfalme wa watu
"إِلَـٰهِ ٱلنَّاسِ"
Mwenye kuabudiwa na watu
"مِن شَرِّ ٱلۡوَسۡوَاسِ ٱلۡخَنَّاسِ"
Na shari ya mwenye kutia wasi wasi (ikisha)akarejea nyuma.
Na hivi ndivo inavokua mtu sumu ikimzidi anakwenda kuzua mambo kwa watu ikisha anakaa pembeni kuangalia mtafaruku utakao tokea, anakua anasingizia mambo au mtu jambo ambalo yule mtu hata hajasema, hivi na vile, fulani jinsi kadhaa wa kadhaa, maradhi yanakua yameshamvaa, hana muokozi.
"لَّذِى يُوَسۡوِسُ فِى صُدُورِ ٱلنَّاسِ"
Anatia wasi wasi nyoyoni mwa watu.
Na Mtu kama huyu anakuwa katawaliwa na shetani, kila kitu chake kina milikiwa na shetani, na inakua hivi kwa sumu zake anazotia watu wanakua hawajui waamini kweli au sikweli, hivo fulani ndio kweli kanisema hivi au hajanisema, mtu kama huyu anatapakaza sumu kila anapokwenda.
"مِنَ ٱلۡجِنَّةِ وَٱلنَّاسِ"
Ni miongoni mwa majini na wanaadamu(Watu)
Hapa lazima ifahamike kazi hii ya sumu inaanzwa na (Shetani)na anashirikishwa mwanaadamu mpaka na yeye anakua katika kundi la mashetani, anashiriki kutapakaza sumu mpaka shetani mwenyewe ana shangaa.
Mwisho kabisa namalizia kwa kukuombeni jaribuni kusamehe, kama jambo lipo au limepita basi kubali limetokea na haliwezi kurudi tena likajirekebisha, tuondoshe mafundo kwenye mioyo yetu,  ukifanya hivyo utaona maisha yako unaishi kwa utulivu kitu kama hukipendi unakuwa sehemu ya kati wala huendi upande wa chuki, na ukiwa (natural)ndio unaipata salama. 
Namuomba Mollah atujaalie kuwa katika kundi la waja wa kati na kati. Amin
Abdulla Baja

Saturday, September 15, 2012

HASARA YA BABA MWENYE KUTUPA KIZAZI CHAKE(PART 1)

Asalaam Aleiykum,

Ametukuka Mwenye-enzi-Mungu aliyeumba Mwanamme na Mwanamke ili wapate kupeana (ushirikiano)wa maisha ya utulivu, wapate kupeana Mapenzi, katika (taasisi)ya ndoa. Ikisha baada ya hayo akajaalia kutokea katika miili yao kupatikana kizazi ambacho ni (Zawadi)kutoka kwa Mollah wao ili wapate kuishi kwa salama na kufata maamrisho ya Mwenye-enzi-Mungu na Mtume wake ambayo ni Mwanaadamu kudumu katika Ibada.
Ikasemwa ndani ya (Quraan-sura-ya-Rum-aya-ya-21)
"وَمِنۡ ءَايَـٰتِهِۦۤ أَنۡ خَلَقَ لَكُم مِّنۡ أَنفُسِكُمۡ أَزۡوَٲجً۬ا لِّتَسۡكُنُوٓاْ إِلَيۡهَا وَجَعَلَ بَيۡنَڪُم مَّوَدَّةً۬ وَرَحۡمَةً‌ۚ إِنَّ فِى ذَٲلِكَ لَأَيَـٰتٍ۬ لِّقَوۡمٍ۬ يَتَفَكَّرُونَ"
"Na katika alama zake, amekuumbieni wake zenu(Partner)katika jinsi yenu ili mupate utulivu kwao, Akajaalia mapenzi na huruma baina yenu, hakika katika haya kuna alama kwa wenye kufikiri".
Imeanza hii aya ya Quraan kutaja Alama(Ishara)dalili zetu, ikisha mwisho wake ikamalizikia aya kwa kuwataja wenye kufikiri, hapo kuna uzinduo, lakini wapi wanaadamu tumo kwenye hasara kubwa wengi katika sisi hakuna hata mwenye kuota wacha kufikiri, sababu kufikiri unatakiwa uwe macho, na sisi sote mtu anatembea kalala, akikaa barazani kalala, mtu hata anazungumza huku kalala ndio maana utaona hata mambo yaliyomo kwenye nafsi yako yanakupita hivi hivi ukiwa umelala. Na kama hujalala jee? ushawahi hata siku moja kumtizama mkeo au mumeo japo dakika mbili machoni mkawa mnatizamana, jee ushawahi kujiuliza kwanini hususan mie nikamuoa au kuolewa na huyu?Ushawahi kujiuliza mbona tumefanana kidogo, vipi macho yake kama yangu? ilikuaje mie nikapiga goti kufunga ndoa na huyu, hivi kweli mie namjua mke au mume wangu, jee mimi naishi nae kimapenzi au tunaishi tu penzi lishakufa zamani?.Hamuwezi kutazamana unajua kwanini? kwa sababu kila mmoja ana (Masanamu-Skeleton)zake moyoni na anaogopa katika kutizamana kule yasije ya kamdondoka akaadhirika, na mwisho ushajiuliza Jee hapa Rehma zipo? Yakikujia Mawazo kama hayo basi hapo umekuwemo katika lile kundi la wenye kufikiri, na wale wenye kufikiri huchukuliwa katika safari nyengine kabisa wakafunguliwa muono mpya kabisa na wakapata kujua kwa yakini yakuwa njia hii ya mimi kufunga ndoa na fulani Imepangwa na Mollah wangu.
Na ukipata hilo hapo unakua umeamka usingizini, unakua unaridhika, unakinai, huna pupa unajua haya amenitakia yule mwenye kunipangia kudra hii na mimi sina budi ila kuikubali. Sikua mimi mwenye kupanga haya, (Wala haitokei kama accident-ajali) yeye ndie aliyenishushia mapenzi na hamu na kuniongoza mimi kuja kumposa(Kumkubali)mwenzangu huyu, na lazima katika muongozo huu kanipangia kheri na amana atakazo nipa ambazo hakuna mwengine azijuae isipokua yeye Mollah wangu."
" وَٱللَّهُ جَعَلَ لَكُم مِّنۡ أَنفُسِكُمۡ أَزۡوَٲجً۬ا وَجَعَلَ لَكُم مِّنۡ أَزۡوَٲجِڪُم بَنِينَ وَحَفَدَةً۬ وَرَزَقَكُم مِّنَ ٱلطَّيِّبَـٰتِ‌ۚ أَفَبِٱلۡبَـٰطِلِ يُؤۡمِنُونَ وَبِنِعۡمَتِ ٱللَّهِ هُمۡ يَكۡفُرُونَ"
"Mwenye-enzi-Mungu amekujaalieni (amekuumbieni)katika nafsi zenu wake, na akakujaalieni(kuumbieni)kutoka kwa wake zenu watoto na wajukuu, akakuruzukuni vitu (vilivyo)vizuri, Basi mmekua yale yaso haki mnayaamini(kuyafata)na Neema za Mwenye-enzi-Mungu(Mnazikimbia)Mnazikufuru(mnazikataa)"
"Ukiitupia macho hii aya utajua kwa uhakika kuwa huu mpango au njia kuwa mimi nimeshapangiwa(haitokei kama bahati)Nimepangiwa mimi nimuoe fulani na nikisha kumuoa atazaliwa fulani na fulani na hiyo ndio kazi alonipangia Mollah wangu, amenikabidhi amana ilotokana na damu yangu, viungo vyangu, sasa nini unafanya vitoto vikishazaliwa? vitoto pengine vitatu au vitano bado vidogo, viko katika hali ya kukuhitaji nini unafanya?-Endelea part 2

HASARA YA BABA MWENYE KUTUPA KIZAZI CHAKE-PART 2

Asalaam Aleiykum,

Jambo la kwanza (shetani) anokuonesha yakuwa mwenzako huyu uloishi naye miaka yote sasa keshakua mzee, Figure sikama ile ya zamani(Unasahau na wewe ushakua mzee)pengine sasa hapaki rangi ya kucha, Nini unafanya?.Wewe hutizami vile vitoto au mwenzio uloishi naye labda miaka mitano au kumi, wewe sasa unaanza kukimbilia nje, pengine sasa nyumbani hurejei mpaka watu wote washalala, Mkeo akiomba kutoka na wewe unamkimbia kwa kutangulia mbele, akitaka mshikane mkono ndio balaa inaanzia hapo unaweza hata kumpiga kibao, Hapo tena unaanza kutafuta kila sababu ya ugonvi ili upate kutoa talaka. Unatafuta sababu za kukimbia ulezi wa watoto wako mwenyewe, Unaanza kufikiria vipi uta-enjoy life na mwanamke mwengine, hutaki tena maisha ya ndoa, sasa dhamana zinakutia dhiki.
Mollah wako alipokataza zinaa alisema hivi:(Quraan-Isra-32)
"وَلَا تَقۡرَبُواْ ٱلزِّنَىٰٓ‌ۖ إِنَّهُ ۥ كَانَ فَـٰحِشَةً۬ وَسَآءَ سَبِيلاً۬"
"Na wala msikaribie zinaa, hakika huo ni uchafu, na njia mbaya"
kuhusu uchafu unajulikana kuanzia maradhi na mambo kadhaa mengine, Kusudio la neno njia (mbaya) ni ile ya kuzaliwa Mtoto maskini hana baba, hana malezi, mtoto yuko ovyo ovyo, hajui anakwenda au anarudi dhiki na balaa kubwa linamkuta yule kiumbe alozaliwa nje ya ndoa. Nini habari yako wewe ulozaa ndani ya ndoa ikisha ukageuka kutenda yale yale anotenda mzinifu kwa kutupa kizazi chake, wewe unafanya yale yale aloharamisha Mollah wako ndio maana ukaambiwa(katika hadith) talaka ni amri anoichukia Mollah wako(Hapa napenda kukumbusha)Mollah wako hapendi wala hachukii hiyo ni mifano mnopewa nyinyi wanaadamu kuonesha ubaya wa tendo hili la talaka.
Sasa nini unachofanya wewe Mzee unotupa kizazi chako ukakimbilia maisha mengine ya Raha na Mustarehe, Huku nyuma unaacha ile amana alokupa Mollah wako inateseka, unaipinga dini iloleta tendo hili la ndoa ili wawili nyie pamoja na familia yenu ipate utulivu, heshima na mapenzi, usalama pamoja na mahusiano ili mpate kufanya Ibada, mpate kuwa wacha Mungu. Hiyo ndio dhumuni la ndoa na uchambuzi wa neno Ibada ni mpana wenye upeo mkubwa, kama vile kila kitendo cha kheri ni Ibada, Tendo lolote la kuisaidia jamii ni Ibada, Maneno mema pia ni Ibada.
Mollah wako kakupa cheo baada ya kuoa na kuzaa vitoto sasa unaitwa (Mama au Baba)hiyo pekee inaonesha dhamana ulopewa ya kuvilea vitoto vyako mpaka viwe vikubwa, Lakini wapi umetumia maisha yako sasa unataka utumie na ya wenzako, Vijana wanashangaa mbona mzee fulani nyimbo zote anazijua, style yoyote ikitoka na yeye yumo, ndio maana utaona vizazi vyetu vingi vinaangamia, havina malezi mazuri ya msingi wa kidini, ukiuliza unaambiwa maskini baba yao kakimbia watoto wakiwa wadogo, kakimbia dhamana ya ulezi, kakimbia kuwatizama watoto wake, kakimbia kutoa hata kilo chake. Sasa anakuaje Mzee alotenda haya?enedelea part 3


HASARA YA BABA MWENYE KUTUPA KIZAZI CHAKE-PART 3

Asalaam Aleiykum,

Anakua moja kwa moja kamuasi Mollah wake, haingii huyu katika lile kundi lilotajwa katika sura ya (Muumin-aya-ya-8-)
"وَٱلَّذِينَ هُمۡ لِأَمَـٰنَـٰتِهِمۡ وَعَهۡدِهِمۡ رَٲعُونَ"
"Ambao Amana zao na (zile)Ahadi(Walochukua)wanaziangalia"
Wewe ulipo piga goti (kufunga ndoa)ukachukua ahadi ukaaminiwa na wazee pamoja na Mollah wako ikisha ukapewa dhamana ya vitoto sasa vimezaliwa wewe ndio unakimbia vipi utakua katika kundi la waliofaulu? vipi wewe utakua Muumin, ulikua Muumin pale ulipochukua ahadi ya kuzitunza amana, lakini sasa unakimbia vipi tena ubakie kuwa Muumin, wewe unakimbia tendo la Ibada, wewe una asi (Isipokua papatikane sababu za ukweli na uhakika sasa huwezi kuishi tena au huwezi kuiangalia amana hii)labda unatendewa vitimbi wazi wazi, hapo huna makosa una uhuru wa kuikimbia lakini sio kwa sababu za upuuzi na Mollah wako ni mwenye kujua japo utaficha moyoni mwako.
Vipi leo Unajiita Muumin na unasali Rakaa zisizo na idadi huku umetupa kizazi chako, unatoa sadaka huku kizazi chako kinateseka, hebu kumbuka wewe umetoa Ahadi mbele za watu na ukataka Mollah wako akushuhudie ikisha baada ya kupewa kizazi unachukua begi lako la mbao unaondoka tu bila ya fikira yoyote, ukiulizwa nini kimetokea mke kaunguza chakula, au kachelewa kurudi, au katoka bila ya ruhusa yangu, basi hee umeishi naye miaka kumi katoka siku moja ndio iwe talaka yake, ole wako wewe unayefanya kiini macho hichi cha kutupa kizazi chako kumbuka maneno ya (Luqman-aya-ya-16)"
يَـٰبُنَىَّ إِنَّہَآ إِن تَكُ مِثۡقَالَ حَبَّةٍ۬ مِّنۡ خَرۡدَلٍ۬ فَتَكُن فِى صَخۡرَةٍ أَوۡ فِى ٱلسَّمَـٰوَٲتِ أَوۡ فِى ٱلۡأَرۡضِ يَأۡتِ بِہَا ٱللَّهُ‌ۚ إِنَّ ٱللَّهَ لَطِيفٌ خَبِيرٌ۬"
"Ewe mwanangu hakika jambo lolote mfano liwe japo chembe ya Hardali;liwe ndani ya jabali au mbinguni au katika ardhi, Mwenye-enzi-Mungu atalileta(Amlipe mtu)bila shaka Mwenye-enzi-Mungu ni mjuzi wa mambo yote(Yalo dhahiri na siri)".
Napenda uelewe mwenye kukimbia kizazi chako, kama inavosema aya chochote kile kina malipo yake, basi elewa hawateseki watoto wewe ukaachiwa, wakiteseka watoto na wewe Mungu anakuondoshea unakua huna furaha kabisa ya maisha yako, hawasumbuki watoto ila na wewe unasumbuka katika akili yako, hawapati maradhi watoto ikawa hakuna wa kuwaangalia ila na wewe unapewa maradhi huko ulipo, hawakosi mapenzi watoto ila na wewe huyapati mapenzi huko uliko isipokua kudanganywa, kwani elewa ukifanya jambo la kusudi ni lazima ulipwe kutokana na kusudi yako.
Basi wajitazame wale walokimbia vizazi vyao wana maisha gani ajiulize mwenyewe jee ana furaha majibu utayajua mwenyewe katika nafsi yako, Na hivo ndivo inavokua Mtu akipinga njia ya Mwenye-enzi-Mungu na kukimbia kuziangalia Dhamana zake na amana alopewa, Ajijue Mtu anachangia kwa ukamilifu uharibifu wa mwenendo mzima wa jamii ya kiislam. Anachangia kuharibika kwa wale watoto kwa kukosa kupata malezi ya Kiislam, kwa hiyo watahadhari mababa na waangalie kwa undani pale wanapotaka kutafuta viji sababu vidogo vidogo ili wapate kuzitekeleza amana walizopewa, na wale wasojua labda ni wape uelekezi huu kwa (Mume na Mke)kuna (Time)au (Age)umri fulani hususan kuanzia (miaka 35 mpaka 40) wazungu wanaita(Middle-age-crisis)pengine Mtu umekumbwa na hali kama hiyo unatamani utoto au ujana urejee tena kwa hiyo unaweza kufanya vituko visosemeka mtu inapaswa akumbuke kuwa (Mechanism)ya Mwili wake yanabadilika na mawimbi yanatokezea lazima mtu ajifundishe vipi atapigana au kuyakwepa mawimbi hayo ili bahari ikitulia aendelee kuishi na familia yake. Watahadhari pia Masheikh na hukumu zao za Talaka bila ya kuzingatia Mustakabal wa watoto, kwani ukifanya hivyo na wewe Sheikh unashiriki kuivunja Amana ya Mollah alompa Mja wake aingalie.
Enyi Mababa inatosha kukumbuka hawa mnaowakimbia ni watoto wenu, mkija kufa wanakurithini na nyie wakifa wao mnawarithi basi inatosha hilo kukujulisha na kukufariji ili usitupe kizazi chako, Na wale watofanya kwa kusudi basi wao wanajiandalia makaazi yao huko Akhera sehemu inayoitwa(Aaraf) hapo unakua Motoni hupo na peponi huendi utakaa hapo utaabike kama walivotaabika wanao, kama ulivotesa kizazi chako. Na Muomba Mollah atunusuru na kuzurura Akhera.
Abdulla Baja

Sunday, September 9, 2012

HAKI YA KUMSALIA MAITI UKIWA MBALI (PART 1)

Asalaam-Aleiykum:
Mwanaadamu kapewa cheo mara mbili na Mollah wake, kwanza pale alipoumbwa mara ya mwanzo Nabii Adam a.s  wakaambiwa Malaika wamsujudie,  Sote tunakifahamu kisa hiki hakuna haja ya kukirejea, Ikisha akapewa darja yengine anapofariki(kufa)basi atapewa heshima ya kusaliwa au kuombewa(utakavo penda kuita).
Bwana Mtume s.a.w akatufanyia hisani ya kutufundisha vipi njia ya kufanya na taratibu zake na mipango yake na dalili zake zote wala hakuweka kizuizi katika hilo.Vipi? Mbali na zile sala za kuwasalia maiti waliokuwepo machoni mwake pia aliwasalia walokuwa mbali na hata walokwisha kuzikwa ili atufahamishe sisi kuwa yote ni sahihi na ndio mafundisho yake, na wala hakuna pahala aliposema hivi msifanye nafanya mimi tu, kwa kuwa hili wamepangiwa ni Sala ya (Mitume)hakuna jambo hilo, nini alifanya Bwana Mtume s.a.w "Anahadithia Sayyid Abbi Hurairah r.a "Alipata habari siku alokufa Najash,(King-Negus-wa-Ethopia)Akatoka na masahaba kwenye(kiwanja)akawapanga safu,ikisha akatoa Takbira na (Kumsalia)fundisho la kwanza,(Bukhari-na-Muslim-kitab-janaiz)halafu kisa chengine yule Bibi wa kimaskini alokua akifanya kazi za kufagia msikiti, Alipewa habari Bwana Mtume s.a.w kuhusiana na maradhi yake akaagiza ikiwa atakufa basi nambieni, Alipofariki ilivokua usiku Mtume s.a.w kashalala Masahaba zake wakaamua kumzika bila ya kumuarifu Bwana Mtume s.a.w, ilipofika asubuhi wakampa taarifa akawaambia sikukuamrisheni mnipe habari atakapokufa?wakasema tulikhofu tusije kukuangaisha usiku "Ewe mjumbe wa Mwenye-enzi-Mungu"Akatoka Mtume s.a.w na Masahaba mpaka kwenye lile kaburi akawapanga safu masahaba zake ikisha akatoa takbira (4)yaani kumsalia:Imetajwa pia na (bukhari na Muslim katika kitab cha salah ya kwenye kaburi).Naam hiyo ndio habari, hayo ndio mafundisho hayana pingamizi ila uwe unampinga Mtume s.a.w, hapa sisi waislamu tumepata mafundisho hata ukiwa mbali unaweza kumsalia na kumuombea maiti yako, na hata kama kazikwa unaweza kumsalia kama vitendo vya hadith vinavoelezea na hii ni faraja kwa wale pengine kwa sababu zisizoweza kuzuilika hawatoweza kuhudhuria hiyo (Fardh-kifaya)basi wanaweza kusali na inajuzu kumsalia Maiti wako au muislam mwenzio yoyote yule.
Sasa na tuingie kwa undani tutazame kwanini tunasali hii Sala ya Maiti? Napenda uelewe sala hii ina sehemu mbili, ama sehemu ya kwanza ni ile kuupa heshima ule mwili wa marehemu kwa wale walokaribu wanapata nafasi hii ya kusimama mbele ya maiti na kumsalia(Sio kutoa heshima za mwisho)unafanya hivo pengine alokufa Mkeo, au Baba yako au Mama yako au Mwanao, nimewataja hawa wa karibu kuonesha umuhimu wa jamaa kwa yule alotangulia mbele ya haki, yule wewe umeishi naye, umekua naye, kipenzi chako umesimama mbele yake unapata nafasi ya kumuaga kwa kumsalia na kumuombea kwa njia za Mwenye-enzi-Mungu yule kiumbe mlokua pamoja katika ulimwengu huu(Nasisitiza wale walokaribu wasikae nje ya misikiti na kuacha kusalia Maiti zao)isiwe basi ndio kafunikwa vitambaa ndio yale mahusiano yenu yote yamekwisha anakuhitaji hususan siku hii ya leo, nitaita sehemu hii ya mwanzo ni (Physical).
Na hii sehemu ya pili ambayo nitaiita (Sipiritual-cum-Mental)hii ni ile ya kiroho au (Communion) napenda nifafanue (communion)ni tendo la moyo kwa moyo au roho kwa roho au (Roho)na (Mollah)wake, usije ukababaishwa na (Communication)ni (head to head)maombi hayo hayafiki kokote,  sasa nini mfano wa hiyo (Communion)ni kitendo cha hisia(Mfano)kama vile kaja mtu mbele yako hajakwambia chochote kasimama mbele yako machozi yanamtoka pengine na wewe yatakutoka machozi au bila ya kujitambua, kilochotokea hapo ndio hiyo (communion)ni mawasiliano ya kiroho au kimoyo ita utakavyo na mifano iko mingi wewe ishakutokea, kama vile umeona (Accident)umekwenda kutizama mgonjwa kuna kitu kinatokezea ndani ya (Ufahamu)wako na hiyo ndio adhma yangu ya kuizungumzia hii (Sipiritual communion)ambayo haikatiki, ianayokatika ni communication. Na  sio sisi  Binaadamu peke yetu wenye hii (communion)hata wanyama wanayo, Wanasayansi walifanya uchunguzi wakachukua wale wanyama wanozaa, wakawapeleka mji mwengine kabisa, Halafu wakachukua vitoto vya wale wanyama vikachinjwa, Wanasema wachunguzi hao tuliona mfadhaiko na huzuni kwa Mama za wanyama hawa, sasa ikiwa vinyama hali hiyo nini hali yetu sisi Binaadamu unapofiwa na alio wako?
Kutokana na hii (communion)ndio Bwana Mtume s.a.w akasema "Wakipatikana watu mia wasomshirikisha Mollah wao na chochote ikisha wakamuombea maiti anakua Mollah ni mwenye kuipokea dua yao na hadith ziko nyingi na zengine zimetaja watu (40)nk.
Kwanini sasa nikasisitiza watu wa karibu ni uzuri kumuombea (Maiti)? sababu zinazopelekea hapa ni ile (Communion)niloitaja, Nimehudhuria misiba kadhaa nimekuta watu wa marehemu labda kwa kutokujua au kufahamiswa vyengine wanakua hawasali sala hii, wengine wananifahamisha jambo hili halifai, au watamsalia walio karibu naye huko nyumbani, walomwambia hivo wao wenyewe hawana ushaihidi wa jambo hili, au pengine ndani ya mioyo yao hakuna (Communion)hisia zimeondoka na jambo hili ni hatari kubwa, Watu wanakuwa hawasalii watoto zao au watoto hawasalii wazee wao na hii ina kunyima siku hii adhimu ya kumuombea mzee wako,  ana hali gani yule mzee au mtoto atakapo tizama nyuma na kuoneshwa hata alo wako leo hataki kukuombea au kukusalia anapiga (story)za mambo ya kipuuzi na wenzie, basi jikumbushe mwanaadamu una mambo mawili ambayo huna uwezo nayo,Mambo yepi hayo? Endelea sehemu ya pili.

HAKI YA KUMSALIA MAITI UKIWA MBALI (PART 2)

Asalaam Aleiykum:

Inaendelea:
Mambo yenyewe mwanaadamu huna hata uwezo nayo ni haya, la kwanza linatokea hulioni,  lakini la pili linatokea unakua mwenye kuliona lakini yote hayo yanatokea wewe ukiwa si mshiriki wake, kwanza kuzaliwa huna maombi katika swala hili huwezi kuchagua baba yangu au mama yangu awe fulani,  Na la pili siku ya kufa kwako,  huna dua au chengine chochote cha kuweza kuzuia jambo hili, zawadi hizi mbili anakupangia Mwenye-enzi-Mungu,  ndio maana ukaambiwa  unapofika umri wa miaka (40)(katika Qura'an) nishukuru mimi na wazee wako wawili, Sasa ikiwa wako hai unaambiwa uwashukuru vipi leo wanaondoka katika ulimwengu huu wewe unakatazwa usiwashukuru,usiwaombee,usiwasalie na kuwatakia rehma na wewe unakubali kirahisi hebu amka usikubali mtu akukamatie dini yako, dini unayo mwenyewe huyo anokwambia na wewe hamna tafauti,  asizuke mtu akakwambia haifai na wewe ukakubali hakuna jambo la kheri lenye makosa kwa Mollah wako, hakuna Dua itakayokuadhibu hebu amka usingizini na muanze kuwaombea Maiti zenu, elewa kufa hakutokei siku zote ni nadra sana ingekua inatokea siku zote si mngekua mshakwisha, wazee wenyewe wawili, watoto wenyewe wawili basi hata hao unaondoshewa hii fadhila ya kuwasalia na kuwatakia maghfirah na wewe unakubali, siku hii ya leo wanakuhitaji sana, siku hii ya leo ndio siku yako ya kufanya (Communion)na alo wako siku zote ulikua unadharau yupo ntazungumza nae, yupo hana neno tukipata nafasi tutazungumza sasa leo ndio kaondoka milele na wewe mgonjwa wa kusahau hivyo utamkumbuka tena baada ya leo usijidanganye muombee maiti yako leo kabla ya kesho wala asikwambie mtu  haifiki dua yako ndio inafika hassa kwani ukiomba wewe ndio unaomba kwa hiyo(Communion-heart to heart)kwanini unamwachia mtu mwengine amuombee maiti yako.
Soma maudhui ilo pita(Umuhimu wa dua)utajua katika makutano ya (Roho)hakuna umbali wowote baina ya muombaji(Talib wa Mattlub)anaeomba, tena tahadhari sana na watu hawa hawakutakii mema au wao wenyewe hawana ujuzi wa elimu ya (Tawhid)wakapata kujua nini kina tokea wakati mwanaadamu anakata (Roho)au masaa kadhaa baada ya mtu kufariki kwake, sasa ni kinatokea?anahadithia Umm Salamah r.anha"Alikuja Bwana Mtume s.a.w  wakati Abu Salamah anakata roho, akamfunika macho yake, ikisha akasema roho inapochukuliwa na macho yanaifata, walozunguka pale wakaanza kulia kwa mayoe machozi yana watoka wakaanza kusema maneno, akasema Bwana Mtume .s.a.w " msiseme chochote isipokua kitu kizuri, kwani Malaika ni wenye kuitikia Amin kwa kila mnachosema, ikisha akaanza kuomba dua""akasema Ewe Mollah wangu msamehe Abu Salamah, mnyanyue darja yake, muweke katika kundi la waja wema, mjaalie mrithi mwema alobakia, mpe msamaha yeye na sisi tulobakia".
Sasa ikiwa Bwana Mtume s.a.w kenda kwenye nyumba akaanza kuomba dua vipi leo sisi tunakwenda nyumba za misiba mpaka tunaondoka hata dua hatuombi wapi tumeyapata mafunzo haya hili nakuachia mwenyewe, Enyi ndugu zangu tukifikwa na misiba tusijizuie kulia au kuhuzunika Mtume s.a.w kafanya hivyo kafanya mbele ya masahaba zake, jueni kulia ni hiyo(communion)kulia ni Imani kulia ni hisia ndani ya kilio ndipo hapo zinapotokea dua, kulia ni huruma na ukilia basi jihesabu wewe hasa ndio mtu wa Mollah, Ahadithia Anas r.a alikuja Bwana Mtume s.a.w wakati mwanae Ibrahim anakata roho macho ya Mtume s.a.w  yakajaa machozi Abrahman bin Auf  r.a akasema hata wewe Bwana Mtume s.a.w  unalia, akajibu Mtume s.a.w "Ewe Ibn Auf"ni kutokana na mapenzi na huruma nafanya hivi, ikisha akalia kwa nguvu "akasema"Macho yetu yanatoka machozi hatutosema isipokua kinacho kuridhisha weye Mollah wetu, huyo ndio Bwana Mtume s.a.w. Sasa jichunguzeni nyinyi nini mnafanya nyumba za misiba? mtapata majibu yenu.
Enyi ndugu zangu tukifikwa na misiba msiache nyinyi kuwaombea maiti zenu na kuwasalia kumbukeni nyinyi ni wakaribu zaidi na huyo marehemu, na dua zenu ni kama sadaka kwa vipenzi vyenu vilotangulia, dua zenu ni rehma kwao kwa yule anopokea maombi yenu, Maombi haya pia ni heshima kwa ule mwili ulokuzaa wewe, na huko kuomba kwako dua ni rehma kwa (Roho)ya marehemu awe mtoto au mzee, kumbuka mapenzi alokupa alipokua hai, kumbuka huruma na msaada alokufanyia japo kidogo wakati mnaishi pamoja, kumbuka mema alokufanyia kukuhudumia akisimama na wewe kwa afya na maradhi basi leo astahiki kupata sala yako na maombi yako, jikumbushe mlipokaa pamoja mkala pamoja mkacheka pamoja leo ndio unamtupa kama gunia, hebu jifundishe japo kidogo upate kuufungua  moyo wa mapenzi, ujaze huruma msalie hata alokua mgonvi wako apate kurehemewa na wewe upate rehma zitokazo kwa Mollah wako.
Kwanini dua zako zisifike kwani Mollah wako si ndie alio kuumbieni hizo (Redio-Wave)mtu akawepo umbali wa masafa elfu nne ukawa unamsikia,  vipi leo uwe na mashaka dua yako haifiki au haifai, Napenda kukufahamisha kuwa dua ndio njia maalumu alokufanyia Mollah wako ili upate kuwasiliana naye, asije akakuwekea mtu yoyote masharti katika jambo hili, Haiwi makosa kumsalia Maiti yako na kumtakia Rehma na maghfirah, Na nyinyi (Mama)zangu mlioko majumbani salieni maiti zenu msikae mkawa mnapitwa na fadhila hizi za kuwaombea maiti zenu.
Sasa napenda nikukumbusheni jambo moja linatokea mbele yenu  lakini limefunikwa pazia hivo wewe huoni,  akija mtu akakwambia kusalia maiti haifai humuulizi kitu lakini akija mtu akakwambia inafaa unamwambia lete ushahidi!! unajua kwanini? nitakupeni kisa cha Abdi(Jahil)kimetokea katia mji(kumbuka uko katika mambo ya kufahamu basi pata fahamu nzuri ili usije kuhadaika)ilikuaje, alimfata Abdi Jahil ulaamaa mkubwa mwenye kusifika katika ule mji, akamwambia mimi ni taabani kwa aibu, watu wote wanajua sina elimu, wanafahamu mimi mtupu sasa nataka nipate heshima katika hii jamii nimechoka, yule Ulamaa akamwabia unataka elimu au unata ujulikane una elimu(Umesoma)? akasema nataka nijulikane nina elimu, basi akamnongoneza sikioni baada ya miezi kadhaa mji mzima ukawa unauliza hee imekuaje Abdi Jahil kawa hivi siku hizi,  watu wote wanamuheshimu haingiliki kwa Ilmu ana siri gani?, anatesa watu namna hivi ,walipomuendea yule ulamaa akamwita Abdi Jahil akmwambia waambie mwenyewe au nitawaambia mimi siri yako, akasema Abdi Jahil nitawaambia mimi mwenyewe,nilivokuja kwa Mualim huyu alinifundisha kitu akanambia (Trick)hii nenda kinyume cha kila kitu utapata umaarufu hakuna njia nyengine, wakikwambia sala ya maiti halali waambie haramu, sio wewe ulo sema haramu wao wanosema halali ndio watotakiwa kuleta ushahidi na wakileta ushahidi na wewe hapo unasoma, akasema ndio imekua kazi yangu kila ninaloambiwa mie nabisha na kwa sababu nabisha nyote mnaniona mie msomi ki ukweli nyinyi nyote mnayeniogopa ndio walimu wangu.Na hivi ndivo tulipofikia kitu chochote unaambiwa lete ushahidi sahihi, na hii ndio hasara kubwa tunasomesha watu bila ya kujijua. Mwisho nakuusieni enyi ndugu zangu tunapofikwa  na misiba tuwasalieni na kuwombea mati zetu,  fungueni mioyo yenu muungane na yule wenu alotangulia. Na Inshaallah Mollah wetu atapokea sala zetu na dua zetu. 
Amin.
Abdulla Baja

Saturday, September 1, 2012

ALAMA ZA WATU WA MOTONI(PART 1)

Asalaam Aleiykum.

Siku moja yalikuja maswali katika ukumbi wa Zanzinet, maswali haya yalitupwa ukumbini kwa anaetaka ajibu, kwa kuwa mie sina dasturi ya kujibu swali nisiloulizwa kwa hiyo nikawa naangalia majibu ya watu yanavotiririka, lakini kuna swali moja kati ya hayo yaloulizwa sikuliona jawabu lake ndio nimeamua kwa faida ya wasomaji wangu nilijibu ili msipate kuyumbishwa katika msimamo wa dini yenu, na hususan wakati naandika mada hii kuhusu (Motoni).
Swali lenyewe lilikuwa namba 3 na liliulizwa hivi:"Kwanini mtu amefanya dhanbi kwa muda wa miaka yake (70)hapa duniani akatiwe motoni milele(Daima)Muulizaji anasisitiza kusema kuwa hapa Allah atakua sio muadilifu, kwa sababu mtu amefanya madhanbi miaka (70)na kutiwa motoni milele,haiendani kihukumu?".
Jawabu:Naam sijui Muulizaji alikua Mwanasheria, au Mtu wa dini gani, au alikua Mtu asoamini Dini ningepata kujua Mtu wa aina gani ningemjibu kutokana na Imani alokua nayo, ningemtosheleza kwa kadiri ya ujuzi wake ili apate kuridhika, kwa kuwa katika hilo swali katajwa Allah basi nachukulia labda muulizaji Muislam lakini ana shaka tu na Imani yake, na hivi ndivo wengi tulivo, hatuna tafauti na wale wasoamini, utaona mmoja anasema hakuna Mungu hana ushaidi wa kuthibitisha hayo, na wewe unosema yupo una shaka kwa kuwa huna ushaidi na huwezi kutoa ushaidi, hutaki kutafuta ushaidi ndio maana na wewe japo umekubali lakini kuna shaka katika nafsi yako.
Swali limeanza kwa lugha ya kwanini? ndani ya mwanzo huu kuna(Challenge)ya kubeza(au muulizaji ana kiburi)pengine cha elimu nk, Anasema Mtu amefanya Dhanmbi miaka yake (70)Napenda Muulizaji aelewe hiyo miaka (70)sio yako ni ya Mwenye-enzi-Mungu, Alokupa zawadi ya kukuleta hapa Ulimwenguni, Akakupa Afya na kukutengenezea kila kilo chema katika dunia hii, Ikisha akakupa fadhila kubwa za kukufanya wewe kuwa mwanaadamu na kukupa fahamu," فَأَلۡهَمَهَا فُجُورَهَا وَتَقۡوَٮٰهَا "(Shams aya ya 8)"Ikisha akaifahamisha uovu wake na wema wake",
Wewe sio tembo, au Punda milia, wewe sio Kima mtini wewe mwanaadamu Mollah wako amekukirimu kitu adhimu, kakukabidhi fahamu unajua hili baya na hili jema.
Sasa inakuaje atiwe Motoni milele, Hapa Mwenye-enzi-Mungu atakua sio muadilifu? Mie simlaumu Muulizaji akili za kibinaadamu zimejaa(Bussiness)au hajazama deep kwenye fahamu zake akajua kutafautisha mambo. Imempeleka shauku yake ya kupanga kuwa hapa Duniani si nina fanya miaka 70 na huko basi angalau nilipwe nikakae humo motoni miaka 70, hiyo ndio itakua haki vyengine vyovyote itakua sio Uadilifu, naonewa na huyo Hakimu hatendi haki kabisa.
Jee wewe unajiamini kukaa Motoni japo kwa siku moja, kwani hutizami nafsi yako pale unapolala, Au kakae pangoni bila ya saa au kuona jua, jee hukusoma Sura ya(Kahfi-aya-ya-11-17-18-19)basi kama hujafanya hivo kimbilia upesi ukajue hiyo miaka 70 itakuaje na milele itakua vipi wakati au saa(Time)ikipotea. 
Nini (Time)muda, ni kitu kilichopangiwa hapa ulimwenguni lakini katika ufalme wa Mollah wako hakuna wakati, (Time na Space)ni kitu kimoja ndio maana utaona wanasayansi wana hesabu dunia imeumbwa miaka (Billioni)kadhaa halafu hawawezi kuendelea kwa sababu (Time na Space)zimeshakomea hapo, vimepotea kabisa vimekua (Single unity)na ndio wewe ukifariki (time)inapotea kama vile ukiwa umelala unajua sasa hivi saa ngapi?,ndio maana ukaambiwa kiama kitakuwepo, wewe una shaka nacho unaona hee watu wote walokufa miaka yote lini watafufuliwa kwa sababu wewe unahesabu muda(Time)lakini kwa Mollah hakuna (Time).
Sasa ikiwa hakuna muda(Time)sasa jee utiwe Motoni mwaka mmoja tu una ghali gani, fanya iwe masiku  jee unaweza kustahamili Joshi la Moto wa Mwenye-enzi-Mungu, na kama unajiamini basi wacha nikujulishe kwanini ikawa milele, vipi utaona kwako wewe daima, pengine unalipwa hiyo hiyo miaka yako sabini lakini unaweza kuchukua kishindo chake. 
Pata mfano hapa ulimwenguni, Polisi wanakutafuta unasubiri gari ije kukuchukua, umejiona unavokua tafrani, sasa karibu ndio utakamatwa na hivi na vile kutwa unatizama saa lakini gari ikitokea unasahau kila kitu, na ikiondoka ndio unacheka na hivo ndio itavokua kwenye huo (Moto)basi tahadhari sana na hiyo miaka yako 70, ogopa sana hukumu ishatolewa na wewe unatakiwa ukakae hiyo miaka 70 na wakati huo (Time) au muda ushapotea ndani ya dhiki ya huko motoni ndugu yangu kwako inakua ni kama milele katika tanuri la Motoni, Namalizia kwa kusema Haikmu ni Mwadilifu, lakini adhabu iumizayo ndio utaona umekaa milele, kwani nafsi ya mwanaadamu haistahamili dhiki, na mfano unaona hapa duniani unaona vipi ukiwa na dhiki unavokua na ukiwa na furaha unavokua, tizama katika kimoja hicho (Time)inapotea nakuachia ukichunguze mwenyewe ni kipi hicho, Na ukisha kukijua basi nakushauri kikumbatie usikiwache abadan fanya jitihada mpaka unatoka roho yako uwe umekidhibiti kaa ukijua kina faida kubwa ya milele na mfano wake hausemeki. Sasa tunaingia katika Mada yetu tulokusudia (Alama za watu wa Motoni)endelea sehemu ya Pili-Part 2

ALAMA ZA WATU WA MOTONI(PART 2)

Asalaam Aleiykum.

Tunaingia katika maudhui ya watu wa Motoni kila Mmoja ana kovu(Alama)zinatafautina katika ufafanuzi hapa leo nazizungumzia za watu wa Motoni kama ilivotajwa katika sura ya(yunus aya ya 27)وَٱلَّذِينَ كَسَبُواْ ٱلسَّيِّـَٔاتِ جَزَآءُ سَيِّئَةِۭ بِمِثۡلِهَا وَتَرۡهَقُهُمۡ ذِلَّةٌ۬‌ۖ مَّا لَهُم مِّنَ ٱللَّهِ مِنۡ عَاصِمٍ۬‌ۖ كَأَنَّمَآ أُغۡشِيَتۡ وُجُوهُهُمۡ قِطَعً۬ا مِّنَ ٱلَّيۡلِ مُظۡلِمًا‌ۚ أُوْلَـٰٓٮِٕكَ أَصۡحَـٰبُ ٱلنَّارِ‌ۖ هُمۡ فِيہَا خَـٰلِدُونَ
"Wale waliochuma maovu, Malipo ya uovu wao ni mfano ule ule(kama walivo tenda)na watakua na udhalili(utawafika).Hawatakua na awezaye kuwalinda(zidi)ya Mwenye-enzi-Mungu,Zitakua Nyuso zao kama(Alama)zimefunikwa(zimezungukwa)na vipande vya usiku wenye kiza kikubwa, Hao ndio watu wa Motoni, na humo watakaa daima."
Inakuaje alama hizi, vipi unaweza kuitambua Alama hii na vipi wengine wanaijua alama yako jee tayari kipande cha giza kimekufunika?maswali hayo utajijibu mwenyewe ukiendelea kusoma na kupata kujua una Alama gani na kama huna basi wewe nenda kasome (Dalili za Mcha Mungu). Usishangae kuwa una Alama hata Mti (Tree)wanasayansi wanatwambia ukiupasua kati unakwambia tarehe fulani, mwaka fulani, saa fulani ilinyesha Mvua kikafatia na kimbunga, na vile vile mwaka huo huo kulikuwa na joto kali huo ni mti unatoa habari hizo waulize wanataaluma wa kilimo watakufahamisha.Sasa nini habari yako wewe kuhusiana na Alama yako.?Kazi yangu hapa kukujulisha hizo Alama za Motoni kwa ithbati kamili unajua wewe mwenyewe na Mollah wako kama unazo au huna Alama hizi, Anasema Mollah katika    Sura ya (Al-Qalam aya ya 7)"إِنَّ رَبَّكَ هُوَ أَعۡلَمُ بِمَن ضَلَّ عَن سَبِيلِهِۦ وَهُوَ أَعۡلَمُ بِٱلۡمُهۡتَدِينَ "
"Hakika Mollah wako  anamjua aliyepotea katika njia yake, Na anawajua waloongoka". Yeye pekee ndie mwenye hakika fulani ni mtu mwema, na fulani ana ufisadi ndani ya nafsi yake, hakuna mwengine mwenye kujua siri hiyo, lakini visa vikizidi, vituko vikiongezeka, kusudi ikizidi na ikawa ndio dasturi yako hapo tena inabidi utiwe Alama na Binaadamu wapate kukujua usipite ukawa unazidi kuwafanyia hadaa, Mollah anawaonea huruma viumbe wake, ndio kama hadithi ya yule kijana alokua anamkera sana Bwana Mtume s.a.w na Waumini wengine ikabidi iteremshwe aya na kuambiwa(Al-Qalam aya ya 12)"مَّنَّاعٍ۬ لِّلۡخَيۡرِ مُعۡتَدٍ أَثِيمٍ"
"Azuiaye kheri, anayedhulumu viumbe wenzie, na ana Muasi Mwenye-enzi-Mungu". Huyu Bwana kero zake zilivozidi Waislam wakawa hawamfahamu basi sasa wakaambiwa katika aya ya (16)
"سَنَسِمُهُ ۥ عَلَى ٱلۡخُرۡطُومِ " Tutamtia kovu juu ya pua yake" ili mpate kumjua, na hivi ndio mpaka leo watu wanaendelea kutiwa Alama makovu kila mtu anayo sijui lako wewe limejificha wapi, ndio maana utaona ukipenda pesa watu watakujua, ukiwa baghili watu watakujua, ukiwa mzinifu watu watakujua. ukiwa fisadi watu watakujua muradi kila mmoja ana Alama yake inajulikana na mwenyewe anaijua ilikojificha japo ataleta dharura, ikisha Mollah wako akakupa nafasi midamu Uhai upo, bado unavuta pumzi basi unayo nafasi ya kuifuta Alama hiyo lakini ukitaka. sasa wacha tuzitaje hizo Alama mimi nitazitaja(4)lakini zitakusanya(Majority)na nyengine zitajieleza zenyewe, Alama ya Mwanzo-Endelea part 3

ALAMA ZA WATU WA MOTONI(PART 3)

Asalaam Aleiykum.
Mashekhe: Wakianza khutba Mashekhe husema Nausia nafsi yangu pamoja na kuhusia nafsi zenu, basi leo hapa naanza na Mashekhe au wale wanoingia katika taasisi za kidini, au kuvamia miskiti kwa ajili ya kula mali za yatima, au kuleta visingizio vyovyote katika jambo la kidini ili upate kudhulumu Waumini, basi Alama zenu mnazijua na sisi tunazijua na kama aya inavosema ambayo nyinyi mnakwenda kinyume chake mechoka kumkera Mollah wenu mitaani sasa mnamfata katika nyumba zake za Ibada aya inahimiza vipi (Sura ya Saff aya ya 10-11)"يَـٰٓأَيُّہَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ هَلۡ أَدُلُّكُمۡ عَلَىٰ تِجَـٰرَةٍ۬ تُنجِيكُم مِّنۡ عَذَابٍ أَلِيمٍ۬ "
"Enyi Mloamini jee nikujulisheni biashara itakayo kuepusheni na adhabu iumizayo".
Nyinyi mnataka kufahamishwa biashara ya kufanya ili muepushwe na adhabu, lakini mmeamua kufanya kinyume chake mnakwenda kuiba huko huko kwenye kutoka hiyo adhabu, hasara ilioje juu yenu kwenda kufanya ufisadi kwa Waumini wa Mwenye-enzi-Mungu, mateso gani yatakukabili huko mbeleni Mollah ndio mwenye kuyajua, nyinyi mnazigeuza taasisi za Kidini ndio sehemu za kazi zenu za kuchota Sadaka za Jamii, watahadhari sana hata wale wanosaidia kufanyika ufisadi huu, ikiwa kina mama majumbani au mkubwa kazini, atahadhari mtu kuyanyamazia mambo haya kwani kunyamaza ni nusu ya kushiriki na wewe utapata fungu la malipo ya kunyamaza kwa hilo halina shaka.
Na kwanini unafanya hivo zitupie macho sababu katika aya inayaofatia utajua kwanini unatenda ufisadi kama huo.
"تُؤۡمِنُونَ بِٱللَّهِ وَرَسُولِهِۦ وَتُجَـٰهِدُونَ فِى سَبِيلِ ٱللَّهِ بِأَمۡوَٲلِكُمۡ وَأَنفُسِكُمۡ‌ۚ ذَٲلِكُمۡ خَيۡرٌ۬ لَّكُمۡ إِن كُنتُمۡ تَعۡلَمُونَ "
"Mumuamini Mwenye-enzi-Mungu na Mtume wake, Na mpigane (kwa ajili)ya Dini ya Mwenye-enzi-Mungu kwa mali zenu na nafsi zenu, hayo ni bora kwenu, Ikiwa mnajua."
Hiyo ndio Biashara yenyewe Mwenye-enzi-Mungu kashafanya yake, kakupa uhai, kakufanyia kheri zote,kakuruzuku afya, wewe una nguvu za kufanya kazi, katimiza upande wake wa biashara, sasa nini upande wako jee umekamilisha, na wala hakuhitaji mengi kutoka kwako kataka ufanye mema na ibada vitu viwili tu ili akupe faida nyingi zisizo malizika.lakini wapi Wewe ndio unamwendea huko huko kwa waumini wake kuanza kudhulumu, na ndio maana aya ikaanza kwa(nikujulisheni)sababu kitu hicho kipo na kigumu sana juu yenu wanaadamu(Adhabu iumizayo) basi mfanye nini jambo la kwanza(Iman)ukiona unakula mali za waumini,maskini,mayatima au hata wananchi basi jijue wewe huna iman ogopa sana kama Mollah wako atakuchukua uko katika hali hiyo,ukiweza kufanya hayo unayoyafanya basi humuamini Mwenye-enzi-Mungu wala Mtume wake, sasa vipi utaweza kupigana hiyo (Jihad)ya nafsi na Mali.Wewe unaambiwa uchume Mali ukatoe, leo wewe wale wale walokwambia ndio unakwenda kuwaibia, kuwadhulumu hivi na vile unakula haram, umejitia katika dini ya Mwenye-enzi-Mungu ndio unaifanya kitega uchumi, (Nimepokea habari wengine wanakwenda kwa waganga kulinda cheo au Uimam msikitini), Atahadhari sana mtu akiwa na Alama hii haifutiki abadan, na dhanmbi zake hazisemeki, asije akajidanganya mtu eti uwadhulumu watu ikisha umeumwa au umekua mzee tena hapo unaanza na (Istighfara)za Mdomo hukubaliwi abadan, wewe uchukue Mali au Pesa zinufaishe watoto wako, ikisha huku upeleke maneno,  hakuna toba hiyo, Kama ulivokopa ndivo utakavolipa.
Endelea part 4 

ALAMA ZA WATU WA MOTONI(PART 4)

Asalaam Aleiykum
Wanasiasa:  Alama ya pili wanasiasa, hakuna ulevi mtu anodumu nao mpaka uzeeni kama siasa, tabu sana kuachia utamu huu wa vyeo na madaraka na utawala, Uteja huu unakupa uwezo fulani dhidi ya wenzio, unajenga joho la kiburi, mwanasiasa hawezi kuchanganya dini na siasa lazima azidi kumoja na wapi kazidi anajua mwenyewe, wachache sana wanakua wanasiasa na huku wanatenda mambo ya kheri, anajijua yeye mwenyewe vipi anawafanyia uadilifu Raia zake, tabu sana kumpata mwanasiasa kama huyu na akipatikana basi Dini inaamrisha alazimishwe kubakia kuendelea kuongoza, sasa inakuwaje mwanasiasa akawa hivyo, kwa sababu (system)yenyewe yote imeoza, imejengeka kwa dhuluma, uonevu,fitina na udhalilishaji kwa hiyo ufanyavo vyovyote Alama unayo, na mwenyewe ndio una hakika nayo hiyo Alama itakupeleka Peponi au Motoni.Bwana Mtume s.a.w aliwanasihi sana wanasiasa wa Kikureshi lakini kwa ajili ya kulinda maslahi yao walikataa kubadili mwenendo wao wakateremshiwa aya ambayo mpaka leo unaona inaendelea na (mfano)ni ule ule na pengine wewe mwanasiasa inakugusa ndio maana unakua mbishi na jeuri aya inasemaje:(Yaasin-aya-ya-10)"سَوَآءٌ عَلَيۡہِمۡ ءَأَنذَرۡتَهُمۡ أَمۡ لَمۡ تُنذِرۡهُمۡ لَا يُؤۡمِنُونَ" "Na ni sawa kwao ukiwaonya au usiwaonye, hawataamini"
Utakavo mwambia mwanasiasa amesahaulishwa kabisa mambo ya Mollah wake, dini anayoifata ni itikadi ya chama chake, hana habari kama anaangamiza nchi yake au dini yake, anapoteza kizazi chake, analeta uharibifu katika jamii yake na hata ukimfahamisha hataki kuamini chochote, kwa hiyo ukimuonya au usimuonye yeye alama yake ndio hiyo, keshaamua kwenda kukaa motoni milele na huwezi kumbadilisha ila atake mwenyewe.
"نَّمَا تُنذِرُ مَنِ ٱتَّبَعَ ٱلذِّڪۡرَ وَخَشِىَ ٱلرَّحۡمَـٰنَ بِٱلۡغَيۡبِۖ فَبَشِّرۡهُ بِمَغۡفِرَةٍ۬ وَأَجۡرٍ۬ ڪَرِيمٍ "
Unaweza kumuonya yule anaefata(kuyasikia)mawaidha na kumuogopa mwingi wa Rehma japo kuwa hamuoni, Basi mbashirie huyo(kuyapata)msamaha na ujira wenye heshima,
Basi mpe habari akigeuza Alama yake huyo mwanasiasa atakua sio tena mtu wa motoni na atapata kuridhiwa na Mollah wake, lakini tabu sana kwa mwanasiasa kubadilika na kuwa na iman hiyo, na wala usishtuke mbona anasali sana, mbona sijda kubwa, msikitini hatoki visikushughulishe vitendo hivyo wewe tazama  alama zake utajua mtu wa aina gani ni lazima alama itajitokeza tu haijifichi.
"إِنَّا نَحۡنُ نُحۡىِ ٱلۡمَوۡتَىٰ وَنَڪۡتُبُ مَا قَدَّمُواْ وَءَاثَـٰرَهُمۡۚ وَكُلَّ شَىۡءٍ
 أَحۡصَيۡنَـٰهُ فِىٓ إِمَامٍ۬ مُّبِينٍ۬"
"Hakika sisi tutawauhisha(Kuwafufua)wafu(watu)na tunaziandika (Amali zote wanazozifanya zisoacha athari) (nyuma yake) na (zile wanazozifanya zikaacha) taathira (nyuma yake)na kila kitu tumekihifadhi katika daftari,(Linalohifadhi kila kitu)linalobainisha kila jambo".
Atahadhari sana mtu kuingia katika Medani ya siasa na dhamira ya ufisadi, akawacha Alama yake hapa duniani, ikiwa ya kheri atapata faida yake hapa duniani na huko Akhera, lakini ikiwa Alama ya shari basi ole wake ajionee huruma yeye mwenyewe yatakayo mkuta kesho motoni, ambako hakuna muombezi, ni mfano kama vile usivoweza kumuomba Allah akuepushe na Mauti na huko motoni kwenye joshi kubwa itakua hivo hivo huwezi kuomba Mollah niepushe na Moto.

ALAMA ZA WATU WA MOTONI(PART 5)

Asalaam Aleiykum
Matajiri:
Naam kila mtu yumo, atahadhari sana mwenye uwezo, ajilinde sana awe anajuta na kutoka machozi, kwani ajue amepewa mtihani sawa na mwanasiasa au kumpita, yeye Alama yake kubwa huonesha waziwazi hajifichi, basi aogope sana mwenye mali asije akaitumia Alama hii kwa njia ya kumpeleka motoni, Isije ikawa anapata usingizi na huku jirani yake hajatia riziki kinywani na yeye anajua.
Asije akawa Alama yake inawaka moto hapa hapa duniani kama inavosema aya:"أَلۡهَٮٰكُمُ ٱلتَّكَاثُرُ""Meghafilika katika kuchuma kwa wingi wa (Mali na kujisifu)"
Hii ndio kawaida ya tajiri yoyote hatosheki lazima apate sifa, lazima watu wamjue, anasikia fakhari watu wakenda kumuomba, kiburi ndio uteja wake, ndio maana ukaambiwa tajiri tabu sana kuingia peponi isipokua wachache Mollah wao alowapa utajiri ikisha akawaruzuku siri ya kuishi kama maskini katika roho zao,(hao wamefaulu)wamepewa fadhila kubwa kabisa na Mollah wao kuliko huo utajiri  mnaouona nyinyi machoni mwenu.
"حَتَّىٰ زُرۡتُمُ ٱلۡمَقَابِرَ""Mpaka mmehudhuria makaburini",
Tajiri Amekufa ghafla,amevamiwa na kutolewa Roho kwa kishindo pengine(heart attack)ulikua umekaa kwenye kiti unatizama(Bank statement)ilivojaa, unacheka na mauti yanakuhudhuria, na watu wanavotaka kukurithi haraka haraka mara wamekuchukua wanakufukia kwenye shimo la futi(6 feet)makaburini, basi tahadhari sana pale umeshaingia kaburini mara jitu la ajabu linakufungu sanda ikisha mnatizamana, na aogope sana mwanaadamu kumkuta hali kama hiyo na yeye ana Alama ya Motoni."  لَتَرَوُنَّ ٱلۡجَحِيمَ ""Hakika mtauona moto".
Jambo la kwanza lepe lepe la mauti linakutoka unauona moto, ukijifanya huoni uzuri, hujui imekuaje mbona uko hapa,kwanini mie."ثُمَّ لَتَرَوُنَّہَا عَيۡنَ ٱلۡيَقِينِ""Ikisha Mtauona kwa yakini Moto".
Ukijifanya hamnazo hufahamu kitu, unasogezwa karibu ili upate yakini yakua humu ndio itakua makaazi yako, na yakini maana yake kuthibitishiwa haya ndio yatakua maskani yako ya kudumu, ukiuliza kwanini, nimefanya nini." ثُمَّ لَتُسۡـَٔلُنَّ يَوۡمَٮِٕذٍ عَنِ ٱلنَّعِيمِ""Ikisha mtaulizwa siku hiyo juu ya neema".
Vipi ulitazamaje mayatima, ulitoa kuwapa maskini,wasojiweza walifaidika na misaada yako, jee ulifanya kheri yoyote,ulisaidia wagonjwa, uliwastiri vizee wasojiweza, ikiwa huna jawabu ya maswali haya na mengine basi matokeo utayajua mwenyewe, labda ikiwa kabla umri haujakatika ulipata nafasi kuibadilisha Alama yako ikawa sio ya motoni tena, lakini mpaka sasa hivi alama ipo vile vile na kivumbi cha mateso kipo pale pale, fanya haraka ubadilishe mwendo wako asaa utafutiwa Alama ya motoni na kupewa alama ya peponi na hiyo ndio yenye kheri kubwa.
Endelea part 6

ALAMA ZA WATU WA MOTONI(PART 6)

Asalaam Aleiykum
Maskini:
Na Maskini hali kadhalika atahadhari na yeye kuwa na Alama ya Motoni kwa kupenda utajiri, kuwa na tamaa ya kudhulumu, kupita huku na huku kufanya jitihada za dhuluma ili atajirike, kupita kuomba madua ya kutaka upewe utajiri kama walivofanya maskini walopita na mpaka hii leo watu hawaridhiki, wana hamaki kwanini hakupewa utajiri, inakuaje fulani hafanyi jitihada yoyote lakini akishika biashara anapata faida yanakuaje mambo haya mbona haitendwi haki hapa, mnaambiwa nini maskini kuhusiana na kadhia hii sura ya (Tawba aya ya 75)"وَمِنۡہُم مَّنۡ عَـٰهَدَ ٱللَّهَ لَٮِٕنۡ ءَاتَٮٰنَا مِن فَضۡلِهِۦ لَنَصَّدَّقَنَّ وَلَنَكُونَنَّ مِنَ ٱلصَّـٰلِحِينَ  "Na miungoni mwao wako walomuahidi Mwenye-enzi-Mungu akitupa fadhila(Utajiri)zake tutatoa sadaka na tutakuwa miongoni  watendao wema"
Asipite mtu akachukua dhamana hiyo, utajiri hauna dhamana unaweza kugeuka vyovyote ukapotea kabisa, kama yule(sahaba aloombewa na Bwana Mtume s.a.w akaupata utajiri ikisha  akageuka na kukataa kutoa zaka, kama aya inayofatia katika sura hiyo inavoeleza:(aya ya 76)" فَلَمَّآ ءَاتَٮٰهُم مِّن فَضۡلِهِۦ بَخِلُواْ بِهِۦ وَتَوَلَّواْ وَّهُم مُّعۡرِضُونَ"
Na alipowapa hizo fadhila zake, walifanyia ubakhili na wakageuka,(na wanaendelea)kugeuka.(kukanusha kabisa)Atahadhari mtu asije kupewa ikisha ukawa mtihani kwake ikawa Alama hili ndio kama lile nililotaja la (Mfanya Biashara) inakuaje ukisha kupewa hiyo mali "Ewe Maskini"tahadhari sana kuwa na choyo na wale walopewa utajiri,  pengine Mollah kakupenda mja wake kukufanya maskini hebu ridhika usije kuwa kama walotajwa katika aya ya (77)
"فَأَعۡقَبَہُمۡ نِفَاقً۬ا فِى قُلُوبِہِمۡ إِلَىٰ يَوۡمِ يَلۡقَوۡنَهُ ۥ بِمَآ أَخۡلَفُواْ ٱللَّهَ مَا وَعَدُوهُ وَبِمَا ڪَانُواْ يَكۡذِبُو"
Akawalipa(Adhabu)ya (kuwatia) unafiki nyoyoni mwao mpaka siku ya kukutana naye(Mollah wao)sababu ya kukhalifu kwao waliomuahidi Mollah wao na kwa sababu ya kusema uongo.
Usije ukawa katika kundi hilo, jaribu kufuta alama hiyo ya kutamani utajiri mpaka ukawa tayari kufanya chochote lazima utajirike, anakwenda mtu kwa mganga kutafuta cheo au utajiri, kwa majungu yeye hasemeki, akipewa kidogo utaanza kusikia milio ya funguo na mwendo unabadilika, jitihada zote afanyazo ni kutafuta vipi atamsahau Mollah wake, vipi atamshirikisha, na subiri apewe cheo uone mambo. Basi  fanya juhudi kama unalo Alama hiyo uanze kuifuta, hakuna siri kubwa kama ile ukiridhia umasikini wako basi Mollah wako anakuteremshia utajiri wa kiroho na unaishi kama mfalme kwenye ulimwengu huu, omba sana upate siri hiyo mpaka wanaadamu wenzio watakushangaa vipi huyu hana kitu lakini mbona ana furaha, mbona hana nguo lakini msafi, mbona ameridhika na kadari ya Mollah wake, ana amali gani huyu, kwako inakua ukipata sawa, ukikosa sawa huna malalamiko, basi ukiridhika kikweli kweli kuna siri Mollah wako atakupa utaijua baina ya wewe na yeye, mie nakupa kidokezo na huu ndio ukumbusho nakuletea ili upate kufanikiwa.

Abdulla Baja