Asalaam Aleiykum
Uislam ni Dini ya haki na Mollah Muumbaji ni Mwenye kuhakikisha haki inatendeka na hayo ndio maamrisho ya kisheria katika Ulimwengu huu, hakuna yoyote Mwenye kulazimishwa jambo kinyume na matakwa yake, Sasa kuna haki moja ambayo mwanamke anateseka sana ambapo ikiwa ataamua kuidai kutoka kwa Mumewe au katika mamlaka ya Dini yake ya Kiislam, katika kadhia hii ya Talaka Mwanamme katawala mpaka kudhani ana Mmiliki mwanamke katika nyanja zote za maisha ya Kidini na kidunia hassa ukizingatia Mamlaka haya ya Talaka katajiwa Mwanamme ndie awezaye kuitoa, basi swali la kujiuliza jee haki hii kapewa mwanamme peke yake, katika maudhui hii tutalitizama hilo ili tupate kujua jee Mwanamke na yeye anayo haki hiyo.
Kwa kuwa Wanaume wamepewa haki ya kuwaongoza Wanawake basi imekua desturi hata mwanamme akiwa mkosa basi kesi nzima inatizamwa na kufanywa mwanammke ndio (Guilty Part)hata kama ana sababu za kimsingi za kumaliza mahusiano na mwanamme husika ambaye itakua kachoka kustahamili au mapenzi yameondoka kutokana na sababu anazo zifahamu Mwenyewe.
Basi atakapoamua sasa anahitaji Talaka au anataka kumaliza mahusiano hayo kwa njia ya salama kabisa ndio huwa sababu ya magonvi na kuteseka kuipata haki yake hiyo ya kimsingi, Pengine itambidi aangukie masheikh labda wamsaidie kuipata haki yake hiyo, mpaka wamwambie sasa uko huru umeeachika, sio (Guilty)tena tumekubali unaweza kuolewa, basi inapaswa Wanawake wajiulize jee kuna haja ya Mateso haya?.
Kabla ya kujiuliza huko wacha kwanza tuguse hiyo ndoa yenyewe ikoje mpaka ikaitwa ndoa, Ndoa ni maridhiano ya nyoyo ya kukubali kwa ridhaa ilo Barikiwa na Mwenye enzi Mungu wako, Kuwa wewe na fulani Muanze mahusiano ambayo yataleta Mapenzi na Rehma ya kizazi na Riziki njema katika maisha yenu ya kidini na dunia baina ya wawili nyinyi, katika mahusiano haya napenda uelewe mnokutana ni wawili nyinyi wenye tabia tafauti ambazo mnatakiwa kuziunganisha ziwe kitu kimoja, ziwe zilofungana nyoyoni ikawa akipigwa (Amin anaumia Amina).
Endelea part 2..
No comments:
Post a Comment