Saturday, December 15, 2012

DIRISHA LA ROHO-PART-2

Asalaam Aleiykum,

"وَلَوۡ أَلۡقَىٰ مَعَاذِيرَهُ ۥ "
Japo anatoa udhuru(Sababu)
Wacha kujivika shungi ukawa unajificha siku zote hutaki kuyajua haya, Acha kutafuta mawaidha ya kukulaza ukawa kama mbuni unajifunika uso wako kwenye ardhi, nyanyua uso kabiliana na ukweli huu nani huyu anotembea akajiona?, nani huyu mwenye kuiona mikono na miguu na viungo vyengine?, nani huyu hata nikiwa nimelala naona ndoto zangu?, huyu mwenye kuona khassa nani? Ewe ndugu yangu jiulize maswali haya kabla ya kuulizwa, jijue kabla ya kujulishwa, ondosha sasa porojo, ondosha sasa maskhara wakati unapotea na wewe unaendelea kuleta nyudhuru unazidi kuzama katika mambo ya kujisahaulisha.
Wanataaluma ya sayansi wanatwambia kuwa Mwili wa mwanaadamu una lugha yake makhsusi(Body language)ambayo unaweza kumjua mtu kakusudia nini na ukisema uongo wanajua, basi na vile vile wanataaluma ya dini wao wamegundua mwanzo kuwa kutokana na macho yako pia wanaweza kujua nini kimekusibu. Hata wewe mtu wa kawaida unaweza kuyajua hayo hebu katizame macho ya mgonjwa na yako uijue tafauti, Ikisha ukimaliza katizame macho yako na ya mtoto mdogo au ya yule mtu alotulia kwa ghushui ya mambo ya kidini mja wa Mwenye-enzi-Mungu, Hapo utaona macho ya watoto na wacha Mungu hayana tafauti yanangara yanatoa(Sparkling)nuru yanameremeta na huku yamejawa na machozi ya unyenyekevu. Lakini maskini macho yetu kwanza makavu, ikisha yamekosa nuru ishatoweka kwa sababu ya mizigo tulobeba, macho mekundu kila unayemuona wasema ni adui yako, yeye anakuogopa na wewe unamuogopa, mkitizamana mara moja tu hamuangaliani tena kila mmoja anamtisha mwenziwe.
Kwanini inakua hivyo? Sababu kubwa Roho nayo inahitaji kula na Macho na Masikio ndio midomo (Milango)yake, Sasa mtizame Muislam anailisha nini Roho yake hata akafikia hali hiyo, Hukuti anachoingiza ndani ila kajaza majina ya (Khanga)zote anayajua yeye, Habari zote za mitaani kahifadhi yeye, mambo yote ya Ulimwengu yamejaa kifuani mwake na mbali na matatizo yake mwenyewe, ndio maana unamuona mtu kachoka ukimtizama machoni na wala hataki umtizame mara ya pili, hii ndio hali sote tulokua nayo na ni baadhi tu ya mizigo iliyomo ndani ya nafsi zetu.
Macho yanaonesha huzuni, macho yanaonesha sasa unabeba mizigo ya ziada na ukitaka kuijua ENDELEA PART 3

No comments:

Post a Comment