Monday, December 24, 2012

UISLAM NA MAPENZI YA MAISHA-PART-2

Asalaam Aleiykum,

Uislam ni dini yenye kukubali maisha ambapo anatakiwa Mtu aishi kwa ukamilifu, ndio maana utaona hukuti hata (utawa) katika dini hii unataka mapenzi ya Mungu fanya huku umeoa, una familia kila jambo limepangwa kwa kiasi na watu wameruhusiwa kufurahi, kuwa na mapenzi na ushirikiano ila yamewekwa masharti ukifurahi wewe uwe na uhakika walo wako,maskini,mafukara, wageni, wapita njia walopotelewa nao wanafurahi pia, pia unatakiwa katika hayo mapenzi yako ya maisha katika dunia hii ukumbuke pia kuna Upande wa pili ulio bora zaidi wa huu unaoitwa Akhera, anokumbusha ni yule yule alokupa maisha haya ya mwanzo na pia anachukua ahadi ya kukupa mara ya pili tena mazuri kupita haya.
Sasa wapi yametajwa haya Al-Imran aya ya 14.
"
زُيِّنَ لِلنَّاسِ حُبُّ ٱلشَّهَوَٲتِ مِنَ ٱلنِّسَآءِ وَٱلۡبَنِينَ وَٱلۡقَنَـٰطِيرِ ٱلۡمُقَنطَرَةِ مِنَ ٱلذَّهَبِ وَٱلۡفِضَّةِ وَٱلۡخَيۡلِ ٱلۡمُسَوَّمَةِ وَٱلۡأَنۡعَـٰمِ وَٱلۡحَرۡثِ‌ۗ ذَٲلِكَ مَتَـٰعُ ٱلۡحَيَوٰةِ ٱلدُّنۡيَا‌ۖ وَٱللَّهُ عِندَهُ ۥ حُسۡنُ ٱلۡمَـَٔابِ "
"Wanaadamu wamepewa huba ya kupenda wanawake na watoto na  (Wingi)wa Dhahabu na Fedha, na Farasi wanotunzwa vizuri, na wanyama na mashamba, na hayo ni matumizi ya maisha ya Duniani, na kwa Mwenye-enzi-Mungu ni kwenye marejeo mazuri"
Nafsi ya Mwanaadamu (Nature)yake imeumbiwa mapenzi, nikisema  neno mapenzi nina maana ya kupenda na kupenda ipo tafauti baina yake na mapenzi (Like na Love).
Nini kupenda?, Kupenda ni mkusanyiko wote wa  Raha na Furaha zote za ulimwengu huu, kupenda ni kama vile Afya tunajua ipo lakini hatujui kitu gani hiyo afya, na kupenda hali kadhalika tunajua tunapenda mambo mengi lakini hatujui kwanini tunapenda, na hayo yalotajwa katika hiyo aya ni machache ili kukupa yakini wewe Muislam kuwa una ruhusiwa kuwa na Mali, majumba, mashamba, nk, na hilo ndio umbile letu sisi wanaadamu imelazimishwa nafsi kuwa katika hali hiyo, ila unachotakiwa hapo usije kusahau ukawa mapenzi yako umekamatana na mali na majumba na madhahabu hata ukafikia kumsahau huyo alokupa haya maisha na hayo uloyapata.
Nini Mapenzi? Tafauti ya mapenzi na kupenda ni hii, kupenda umezaliwa nako(Nature)yako, lakini mapenzi ni kitu kinacholetwa baadae, ni zawadi ikiwa unastahiki kutoka kwa Mollah wako anakushushia(Kama ile aya ya Ndoa)inavosema ikisha tunajaalia Mapenzi na Rehma, na kwa njia ya rahisi ili upate kufahamu na kunielewa vizuri ni kama hivi, Kupenda ni kama Waridi, na mapenzi ni ile harufu yake, (Sasa fanya uchunguzi)mwenyewe ujue lipi linokuja mwanzo Waridi au harufu yake, pia napenda uelewe unaweza kulikamata waridi lakini huwezi kukamata harufu, harufu ndio kama mapenzi huna amri nayo inakuja yenyewe na inaondoka yenyewe, Unaweza kupenda kitu lakini usikipate, na unaweza kumpenda mtu lakini ukawa huna mapenzi naye, hiyo ndio maana yake.
Sasa tunarudi katika ile aya iliposema tumewafanya watu kuwa na huba ya kuwapenda wanawake, kusudio sio upande moja tu, ni pande zote mbili yaani kwa wanaume na wanawake ndio maana mwanzo ikatajwa watu, ilipowekwa khususia kwa kutaja wanawake ni kutokana na umbo la wanawake kuwa maridhiwa(Receptive)lakini katika jinsia wanawake wanawapenda wanaume na wanaume wanawapenda wanawake hakuna tafauti. Huo ndio mfumo wa Maisha ikisha ikaendelea aya na kupenda watoto, ili mfumo huu uwe wa mwenendo wa haki na maridhiano ndio ikawekwa mkisha kupendana mfunge ndoa, na mkifunga ndoa mtapewa zaidi ya hiyo kupendana, na hiyo zaidi ni hayo mapenzi na hizo Rehma ni hao watoto, na huo ndio mfumo wa haki na uadilifu unaotakiwa wa kuwapenda wanawake na watoto, na hizo Rehma zitaendelea kwa kupewa zaidi na zaidi hayo marundo ya dhahabu na fedha, na mafarasi, si lazima upewe mafarasi usije kusema mbona siyaoni hayo mafarasi, pengine wewe umepangiwa umiliki kuku, na hiyo ndio kadara uliyokusudiwa, sasa ukianza kushindana kuyatafuta mafarasi matatizo ya maisha yanaanzia hapo unakua huna furaha hupendi kitu, kila wakati umekunja uso, sababu unashindana na yule alokupangia, ukiwa na kidani kimoja shukuru usishindane ukataka upate bangili ishirini, na ukishukuru utaona huna habari kabisa na hayo madhahabu mengi, na pia msishangae na wale wanopenda wanyama, ikawa unamcheka anompenda paka, au mbwa, kuanzia leo jua yule ndio maumbile yake na wewe pia unavyo unavo vipenda unavijua mwenyewe, mwengine anapenda shamba lake anaona raha kulima na kupanda mazao yake, mwengine anapenda gari yake, mwengine anapenda nyumba yake na mapambo yake hakuna kosa katika hilo, ila msisitizo usije kusahau alo kupa uwezo wa maisha hayo, na haikatazwi kwako kuomba mazuri uyapendayo kutoka kwa Mollah wako, lakini utakua na Imani kubwa na unyenyekevu iwapo utaridhia na kusema "Ewe Mollah wangu weye ndie Uloniumba na wewe ni mwenye kujua mahitajio yangu, basi naomba nipe kama ulivo nipangia wewe  katika hizo raha na mapenzi ya maisha haya, nifanye mimi kuwa maridhawa kwa chochote kile kijacho katika maisha yangu, ukinipa raha na starehe nipe na afya nipate kufurahi na huku nakukumbuka weye, na utakaponipa shida na matatizo, basi nipe na ustahamilivu na shukurani huku nikikukumbuka weye Mollah wangu. Amin.

No comments:

Post a Comment