Saturday, December 1, 2012

MAHUJAJI WA DUNIANI PART-2

Asalaam Aleiykum,

(2)Kwanini niko hapa Ulimwenguni?
"مِنۡہَا خَلَقۡنَـٰكُمۡ وَفِيہَا نُعِيدُكُمۡ وَمِنۡہَا نُخۡرِجُكُمۡ تَارَةً أُخۡرَىٰ"
"Kutokana na hii (Ardhi) tumekuumbeni, na humo tutakurudisheni, na kutoka humo tutakutoeni mara nyengine tena,(Ili mupate kuishi tena)."
Uko hapa Ulimwenguni sababu kila kilichomo katika Ardhi hii pia na katika umbile lako kimo, Na baada ya mauti yako mwili wako unarejea tena kuwa Ardhi kwa mara nyengine tena, hiyo Ardhi unayo ikanyaga sasa hivi ukaifanyia ufisadi baadae na wewe watu wengine watakuja kukukanyaga mwili wako kama unavo kanyaga wewe sasa hivi."Ewe Mwanaadamu wewe na Mti hamna tafauti, jitizame wewe ni mbegu umetokea kuwa mwanaadamu na mti ni mbegu umetokezea kuwa mti, Ila tafauti yenu ipo katika hiyo zawadi Adhiim alo kukirim Mollah wako, akakutafautisha wewe na viumbe wengine akakupa kitu kitokacho kwake mwenyewe nayo ni hii Roho, Ngombe, paka na wengineo wanazo roho lakini si kama yako yako imepewa hadhi ya juu zaidi imetunukiwa fahamu mpaka ikatambua kama kuna kifo na mengineyo.
Amekuagiza Mollah wako yakua anakuleta hapa Ulimwenguni katika safari hii ya Hijja ya Uhai wako na ukishamaliza hakika utarejea kwake, Na hataki chochote kutoka kwako Mwanaadamu isipokua kumuabudu.
"وَمَا خَلَقۡتُ ٱلۡجِنَّ وَٱلۡإِنسَ إِلَّا لِيَعۡبُدُونِ"
"Sikuwaumba Majini na Binaadamu ila wapate kuniabudu"
Nipe Ahsante, Nishukuru na uridhike kwa hilo na yafate maamrisho yangu, zitizame alama za kuwepo kwangu, furahi kwa kujua hili jua, ule mwezi, zile nyota, hawa ndege,haya maua,  zitizame neema zangu hapa Ulimwenguni ili nipate kukuonesha zaidi utakaporejea kwangu.
(3)Lini Nitaondoka?
"وَمَن نُّعَمِّرۡهُ نُنَڪِّسۡهُ فِى ٱلۡخَلۡقِ‌ۖ أَفَلَا يَعۡقِلُونَ"
"Na tunayempa umri (mrefu), tunamrejesha nyuma katika umbo, basi hawayazingatii(haya)"
Tunakupa ishara za kuondoka kwako katika umbile lako, Unaanza baadhi ya mambo kukushinda, Tunakuondoshea uwezo wa kulala sana, Mapigo ya moyo yanapungua kasi yake, kiwango cha meno kinapungua mdomoni mwako, nguvu za macho zinapotea, mwendo wako unakua wa taratibu, Tunazibadilisha nywele zako na kuzifanya nyeupe, Tunakupunguzia marafiki unakua nao wachache, kasi yako ya kula inapungua unakua huwezi kula sana, Halafu mwisho tena mwili ulochoka unashukiwa na maradhi hapo tena unakua tayari kwa safari yako ya kurejea kwetu ulipotokea.
Wapi ninakwenda?Endelea part-3

No comments:

Post a Comment