Saturday, December 1, 2012

MAHUJAJI WA DUNIANI PART-1

Asalaam Aleiykum,

Nini Hajj? Hajj ni Ibada maalum ilopangwa ili mtu afanye safari ya Kiroho(Sipiritual-Journey)kuhudhuria nyumba Takatifu(mji)uloridhiwa na kuchaguliwa na Mwenye-enzi-Mungu ili kukamilisha nguzo hii ya (Ibada).Likaregezwa shuruti la Ibada hii na kusemwa kwa Mwenye uwezo basi na akatende Ibada hii, Mletaji wa agizo hili anajua kuwa kuna wengine watakua hawana uwezo maskini, wengine wagonjwa nk.
Hiyo ni Hijja ya kwanza ambayo wengi tunaifahamu, Lakini kuna Hijja nyengine ambayo haina wepesi, ambayo haijaregezwa masharti, Hijja hiyo imelazimishwa kwa kila mmoja wetu na ndio imekua sababu yetu yakuja katika Ulimwengu huu ndani ya hijja hii nataka ujiulize maswali haya matano?
Mimi Nani?(1)Kwanini niko hapa Ulimwenguni?(2)Lini nitaondoka?(3)Wapi ninapokwenda?(4)Na Vipi yatakua mapokezi yangu huko niendako?(5).
Sote tumekuja katika Ardhi hii ya Mwenye-enzi-Mungu kama mahujaji ili tupate kutizamwa yupi katika sisi atotimiza Hijja yake hii ya Uhai na kurejea huko alikotoka akiwa safi. Ndio Maana swali la Mimi nani? linakuwa gumu, Mwanaadamu analiogopa kwani akijiuliza huwenda akakutana na ukweli, na ukweli siku zote unauma, ukweli unatisha, ukweli mzito na ndani ya ukweli  ni lazima utakua Muislam kamili, na ukiwa Muislam kamili ina maana lazima uitekeleze hiyo Hijja ya Uhai kama ilivokusudiwa na hijja yenyewe ni Ibada.
(1)Mimi Nani?
Mwanaadamu una vitu viwili ambavyo vinakufanya uwe Binaadamu, La kwanza ni Umbo lako ambalo linatokana na hii Ardhi, Umeumbwa kwa vizuri na Mollah wako baada ya kukamilika umbo hili hapo tena ukapewa kitu chengine kabisa nayo ni hiyo Roho. Kwa hiyo hapa tunaweza kusema wewe Mwanaadamu nusu nii hii Ardhi na nusu Nyengine ni hiyo Roho,(Lakini kumbuka huo ni mfano)Umbile la Binaadamu tunalifahamu lakini umbile la Roho hatulifahamu, Na hiyo Roho ni kitu chengine ambacho kinatoka kwa Mwenyewe Mwenye-enzi-Mungu na sisi hatuna elimu nayo, hiyo Roho ndio ilokuja kuhijji hapa ulimwenguni, kama anavosema Mwenye-enzi-Mungu katika Quraan Sura ya Sad aya ya 72.
"فَإِذَا سَوَّيۡتُهُ ۥ وَنَفَخۡتُ فِيهِ مِن رُّوحِى فَقَعُواْ لَهُ ۥ سَـٰجِدِينَ "
"Nitakapo mkamilisha na Kumpulizia Roho itokanayo na mimi, basi mwangukieni kwa kumsujudia."
Hiyo ndio Roho isiyokufa milele, wakati wa kufa kwako, kinachokufa ni kiwiliwili tu, Roho inashuhudia kifo chake na ukikamilika uchungu wa kutoka hiyo Roho, ikishakutoka inachukuliwa na kupelekwa katika makazi ya Barzak ambapo masafa yake ni makisio yenu maili 50,000.
"تَعۡرُجُ ٱلۡمَلَـٰٓٮِٕڪَةُ وَٱلرُّوحُ إِلَيۡهِ فِى يَوۡمٍ۬ كَانَ مِقۡدَارُهُ ۥ خَمۡسِينَ أَلۡفَ سَنَةٍ۬ "
Malaika na Roho hupanda kwake katika siku ambayo muda wake (Kwa makadirio yenu)ni Miaka hamsini elfu.
Hivyo ndivo ulivo mwanaadamu, hilo ndio jibu la mimi ni nani?
Kwanini niko hapa Ulimwenguni?Endelea part-2

No comments:

Post a Comment