Asalaam Aleiykum,
Leo tunaingia katika Maudhui hii ya Maisha ya kidini tukiwa na tamaa kila mmoja wetu kupata angalau japo kwa uchache kuishi kama maamrisho ya kidini yanavo himiza, Kwanini tunatamani?.
Tunatamani kwa sababu (Nature)yetu ina tutaka tuishi hivyo, Dhumuni la kuumbwa kwetu linasisitiza tuishi kwa mwenendo huo, lakini imekua hasara kubwa, imefikia hasara yenyewe katika kila watu mia (100)basi unapata watu wawili tu ndio wenye kuishi maisha ya kidini, na sababu kubwa yule mwenye kuishi maisha ya kidini hawezi kuhadithia kwani akihadithia hakuna ato muamini na wengine wanaweza kusema sasa mambo tayari, apelekwe mirembe au kidongo chekundu huyu kesha, akili zisha haribika, ndio maana wenye kuishi maisha haya wamenyamaza kimya wanaendelea kutumia utajiri wao waloupata na ufalme wao uso kuwa na kikomo.
Hawa wanoishi maisha haya kwao hakuna kuteseka, hamna machungu, hamna kujuta kila siku wanapoamka ni furaha tupu, kwa ajili ya Neema itokayo kwa Mollah wao, hawana kero za Akili wala lawama za wanaadamu.
Sasa inakuaje wachache sana kuyapata maisha haya? na kama raha hizo zote na furaha zinapatikana kwanini wengine hatuwezi kuyapata maisha haya?. Naam Maisha haya ni magumu sana kupatikana na pia rahisi mno iwapo utaamua kuyataka. Nini tafauti yake?
Tafauti yake ni ndogo tu, kwamba bado hujaingia dini Kikamilifu, usije ukajisumbua na kusema mbona nasikiliza mawaidha sana, mbona nasoma Quraan vizuri, usije ukasema navaa hijab siku zote na hayo yakakufanya uamini sasa unaishi maisha ya kidini, lisije likakusumbua sijida kuubwa ukaona sasa nimeshazama kwenye maisha ya kidini, bado kabisa, ndivo vizuri unajitahidi lakini bado unatakiwa uzidishe juhudi na ubadilishe mwenendo wako na hii ndio madhumuni ya mada yetu ya leo, ili kukupa mawili matatu yapate kukuchukua kukupeleka kwenye hayo maisha ya kidini.
Sasa ufanye nini?kuyapata maisha hayo msikilize Bwana Mtume s.a.w kasema nini kuhusiana na kuishi kidini,"Alionesha kifuani mara tatu na kusema Ucha Mungu(Taqwa)uko humu ndani"Alikua na maana gani? Maana ilokusudiwa hapo hakuna nyengine ila kutakiwa Mja urejee ndani, unatakiwa uingie katika nafsi yako(peke yako)ujiulize jee naishi maisha ya Kidini?. Jee nimeingia dini yangu kikamilifu? .Sura ya Baqarah aya ya 208,
"يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ ٱدۡخُلُواْ فِى ٱلسِّلۡمِ ڪَآفَّةً۬ وَلَا تَتَّبِعُواْ خُطُوَٲتِ ٱلشَّيۡطَـٰنِۚ إِنَّهُ ۥ لَڪُمۡ عَدُوٌّ۬ مُّبِينٌ۬
"Enyi Mloamini ingieni katika hukumu za Kiislam zote,(Kwa ukamilifu)Na wala msifate nyayo za Shetani, Hakika yeye kwenu ni adui alo dhahiri".
Vipi utajijua umeingia kwenye hizo hukumu, hapo ndipo pagumu kwanza lazima uondoshe nyayo za Shetani kwani japo una sali na kuomba dua lakini baada ya kwenda kulia wewe unafata nyayo za shetani kuelekea kushoto, Sasa vipi utazikimbia nyayo za Shetani.
Endelea part 2
No comments:
Post a Comment