Asalaam Aleiykum,
Quraan Noor aya ya 30
"قُل لِّلۡمُؤۡمِنِينَ يَغُضُّواْ مِنۡ أَبۡصَـٰرِهِمۡ وَيَحۡفَظُواْ فُرُوجَهُمۡۚ ذَٲلِكَ أَزۡكَىٰ لَهُمۡۗ إِنَّ ٱللَّهَ خَبِيرُۢ بِمَا يَصۡنَعُونَ "
"Waambie waislam wanaume wainamishe macho yao, na wazilinde tupu zao, hili ni takaso kwao, Mwenye-enzi-Mungu anazo habari(zote)za wanayoyafanya".Na pia aya inayofatia ya 31 wanatajwa wanawake kwa maelezo hayo hayo ya hapo juu isipokua yameongezeka ya ziada kwa ajili ya ruhusa za wanawake:
Yalo katazwa yapo mengi sina haja ya kuyataja yote kwa kuwa mimi niko katika maudhui ya kukumbusha nipe nafasi niendelee japo kidogo nikupe hii maana ya kuangusha macho ili ujue kuna kuwaje huko kutakaswa(Kusafishwa, kushushwa hiyo mizigo)unayojitwisha Rohoni mwako.
Katika kutizama kuna mambo mawili yanafanyika la kwanza(1)Unatoa ita upendavyo(Energy au Light)kwenda nje, nadhani utakua ushapata ujuzi wa hiyo (Light)kwani ukifikicha macho si unaona nyota nyota zinaelea kwenye macho yako. Na la pili(2)ni (Reverse process)unarudisha(Information)ndani kile unacho angalia kinatoa (Energy-Light) yake kuja kwako, sasa kama ikiwa hicho unacho angalia ni mambo ya matamanio basi zinatumika nguvu zaidi za kutizama(Kupeleka kwa kuona)na kwa (Kurudisha)ndani ndio maana ukaambiwa angusha macho, jihifadhi na hifadhi tupu yako kwani hicho ndio kina kumaliza kabisa, huo ni mfano mmoja tu nilo utaja kwa ufupi na mifano ipo mingi tu.
Hiyo mizigo ya nguvu nilizo zitaja ndio inokwenda kujaa humo ndani ya kifua chako, na zikishamiri sana hazina pahala pa kukaa inabidi sasa nguvu hizi zitoke nje, na zikitoka nje ndipo hutoa ishara zake, na ishara zake ni hizi.
Jitizame wewe kama unapenda mali hali yako inakuaje ukiona mali za watu, kama unapenda pesa vipi unakua ukitajiwa mambo ya pesa, kama una mahamaki vipi unakua ikiwa utachokozwa kidogo, kama unapenda wanawake au wanaume jitizame vipi unavo hangaika ukiona watu wamechonga nyusi na kope zao, kama unapenda habari za watu jiangalie unavozitafuta habari hizo, ikiwa mpenzi wa uongo jitizame ustaadi wako wa kupanga na kugeuza mambo, kila kilojaa katika Roho yako basi na jinsia yako inageuka kuwa mjumbe wa hilo tendo, na hali hiyo inaendelea kujaza daftari lako la Akhera.
Sasa ufanye nini? Umepewa (Simple technic)mbinu au nyenzo ya kuyaepuka mizigo hiyo, umeambiwa angusha macho yako, ukiona mambo yasofaa(Simple)geuza uso kama huwezi kuangusha macho, ikiwa umepandwa na hamaki jitizame ndani kwanini nimehamaki, wewe una uwezo wa kuona nje kwanini usiwe na uwezo kuona ndani, Ukiona mali sema moyoni kwanini unaipenda mali isokua yangu,ukiona matamanio jisemeze kwanini natizama, ukiweza kufanya hivyo ukajigundua tabia yako isofaa kwa muda wa mwezi mmoja utakua unaanza kushusha hiyo mizigo taratibu tena yote hata ulobeba zamani, na utaanza kusikia raha ya maisha inakuteremkia na utaona wepesi mkubwa katika Roho yako na hapo ndio zinaanza hizo ishara za Utakaso ulotajwa, mapenzi yataanza kukushukia ndani ya Roho kwa njia ya ajabu.
Ewe Ndugu Muislam punguza mizigo uishi maisha ya raha,huna haja ya kuteseka kama unavoteseka hivi sasa, yakiondoka madhila hayo Mwenye-enzi-Mungu anakujaza Rehma zake inakua kama ulopewa ile gilasi ya maji jangwani tena yalo bariidi. Namuomba Mollah Karima atujaalie kuweza kushusha mizigo yetu bila ya kuchelewa, Namuomba Mollah atufungulie fahamu ili tupate kuyafahamu haya tunayo fahamishwa.Amin.
No comments:
Post a Comment