Asalaam Aleiykum,
(4)Wapi ninakwenda?
" إِنَّا نَحۡنُ نَرِثُ ٱلۡأَرۡضَ وَمَنۡ عَلَيۡہَا وَإِلَيۡنَا يُرۡجَعُونَ"
"Bila ya shaka sisi tutairithi ardhi na walio juu yake, Na kwetu watarejeshwa"
Unakwenda sehemu zinapokaa Roho, huko kuna walinzi wasomuasi
Mollah wao, Ni sehemu ya upweke ni ngeni katika fahamu yako, jicho halijapata kuona, pahala ambapo hapana mfano wake na zaidi yategemea mizigo ulobeba na vipi hijja yako ya uhai uliitumia vipi, uliishi vipi na wenzio, ulikua ukisamehe, pahala unapokwenda inategemea na ulipotokea jee ulikua umeridhika? ulikua hutaki zaidi, ulikua hutumii nguvu kuchukua vitu vya watu, huko unapokwenda kuna daraja kwa hiyo mwenyewe ndio utajua unakwenda kukaa wapi magorofani au kwenye vibanda tena hayo utayajibu mwenyewe kutokana na vitendo vyako.
(5)Vipi yatakua mapokezi yangu?
Unataka kujua vipi yatakua mapokezi yako basi kwanza tazama nini matendo yako hapa kwenye Ulimwengu huu, Maneno ya Bwana Mtume s.a.w "anasema"Fanya wepesi mizigo yako unayochukua"kwa sababu safari unayokwenda ni refu, usije ukachukua magunia ya dhanbi ukaja kuteseka milele, jionee huruma kwani wewe huwezi hapa duniani kubeba gunia moja vipi utaweza kubeba huko magunia japo mawili ya dhanbi.
Elewa hizi dhanbi unazotenda ni kitu kizito sana ndio maana utaona ili ipatikane mizani ifanane ukaambiwa ukija na jema moja tutakulipa mara kumi yake, kwanini? hebu sasa fanya hesabu zako utizame wewe mwenyewe inakuaje pale ukifanya dhanbi moja lina uzito wa kima gani(Mfano)tizama mfano huu wa kosa hili dogo, Umesema uongo kuwa mwenzio kaiba ukamfukuzisha kazi, yatizame madhara yake.(1)Nyumbani familia yake hawana chakula(2)Mtoto wake kaumwa hana pesa za kumtibia mpaka kafa(3)Na yeye anampenda mwanae kalia mpaka kaumwa(4)sasa hawezi hata kutafuta kazi(5)anagombana na mkewe sababu haleti chakula(6)anakua omba omba huku na kule anaadhirika(7)watoto wake hawawezi kusoma tena(8)Ibadah hawezi kufanya tena hana utulivu wa ki akili(9)watu katika familia yake wanaanza kutafuta riziki kwa njia ya haramu(10)Magonvi yamezidi anaachana na mkewe. Hiyo ni dhanbi moja ndogo inazaa mlolongo wa mambo hayo yote, hii ndio dhanbi ndogo wewe uliyo isahau, hiyo ndio mizigo unayo ambiwa uifanye mepesi usije ukenda na magunia mazito mazito, Sasa kumbuka katika Hijja hii ya maisha ushafanya dhanbi ngapi zenye mlolongo kama huo.?Nini habari yako wewe usotaka kumuabudu Mollah wako.
Anaendelea Kusema Bwana Mtume s.a.w "Fanya (ukithirishe)uzidishe zawadi unazochukua huko"Unarejea nyumbani fanya hima sana mizigo yako ya (thawabu)zawadi hizo ziwe nyingi mno, punguza mizigo ya maasi ili upate kuzidisha magunia ya wema, Pia napenda uelewe wema haununuliwi dukani, thawabu ni kitu cha bure cha kuchuma na miti yake ni mingi na kila moja malipo yake ni mara kumi, kusaidia mayatima si kwa kuwapa chakula tu bali kuwachukua na kuwalea, kusaidia watu wasojiweza, kuwalisha maskini, kuwonea huruma walofikwa na matatizo ukawasaidia kuyatatua, kusomesha watu, kuwahudumia wagonjwa, kuwaenzi na kutunza familia yako, kufanya Ibadah kwa wingi vyote hivyo ni zawadi katika hijja hii ya Uhai, hata kukisadia kinyama pia katika zawadi, kumsaidia mtoto kuvuka barabara pia katika thawabu, ukimkamata mkono mtu mzima ukamsaidia pia moja katika zawadi Mwenye-enzi-Mungu atujaalie tuwe wenye kutekeleza sio wenye kusoma tukayaacha hapa hapa, Mollah tupe Imani na nguvu ili mazoezi yetu yawe katika kufata amri zako, tumiminie mapenzi yako na Rehma zako tuishi katka hali ya kukumbuka wewe Daima.Amin
No comments:
Post a Comment