Monday, December 24, 2012

UISLAM NA MAPENZI YA MAISHA-PART-1

Asalaam Aleiykum.

Leo nataka niwaondoe wasiwasi na kuwajulisha wale wanopita kusema au kudhani kwamba Uislam unakwenda kinyume na Maisha na hutakiwi kufurahi kabisa, na huna unachokisikia ila vitisho tu, hakuna Maudhui ya upendo kabisa katika mengi ya maudhui yanayotolewa, Nadhani ukiwa na fikra hizo utakua hujapata kabisa maana ya Mawaidha au itakua usikivu wako unasikiliza maneno lakini sio mawaidha, ikiwa unasikiza maneno utakua kweli unapata vitisho kwani maneno yamjengwa kwa njia ya vitisho lakini maneno ni nyenzo inayotumika ili ukiyavuka maneno ukenda upande wa pili wa hayo maneno utakuta kusudio lenyewe nalo ndio dhumuni la kila Sheikh unayemsikiliza au Mwalim anayekusomesha anafanya kazi moja tu nayo kukurudisha katika hali ya kukumbuka "فَذَكِّرۡ إِنَّمَآ أَنتَ مُذَڪِّرٌ۬""Kumbusha hakika wewe ni mkumbushaji".
Hana haja Sheikh ya kutisha wala kukukamatia dini yako akawa anakuendesha anavo taka yeye, ukimuona Sheikh kama huyo anataka kukupangia kila jambo lako kutokana na muono wake basi mkimbie, elewa yeye mwenyewe haitambui dini yake na atakupeleka pabaya, kwani ndani ya dini hii husemwa hakuna kumlazimisha yoyote, " لَّسۡتَ عَلَيۡهِم بِمُصَيۡطِرٍ""Wewe si mwenye kuwatenza nguvu (Kuwalazimisha)".
Nimeona kuna haja la kulizungumza hili ili watu wasione Uislam unaenda kinyume na maisha haya, na Vipi Uislam utaenda kinyume na maisha, wakati ni dini ya haki na ukweli?. Kulijibu hili inabidi tujiulize tena nini dini?.
Dini ni mfumo mzima wa maisha ulojengeka kuanzia kuzaliwa kwako na kwenye afya yako pamoja na mambo yote yaliyomo kwenye Ulimwengu huu, au kwa Lugha ya ufupi(Dini ni Maisha)ya Muongozo wa kukuongoza katika furaha kwa njia ya haki na uadilifu ili yaweze kukupeleka katika hiyo hali kukumbuka(Ibadah)na kuelewa kuwa katika Ulimwengu huu yupo aloumba maisha haya na kuyapanga kama alivotaka mwenyewe na hakika yeye huyo anastahiki kushukuriwa kwa Rehma na Neema hii ya maisha alotupa waja wake, kwani mengine yote kinyume na atakavyo yeye jua yanakuongoza kwenye dhiki, mateso, na kuharibikiwa na hilo halina shaka kabisa.
Jeuri zote zinatupata pale tunapo sahau na kuwa hatujui jinsi gani bahati yako mwanaadamu baraka ilo kushukia ya wewe kuumbwa mwanaadamu, neema hii ya ufahamu hawakupewa viumbe vyengine vyote humu Ulimwenguni isipokua wewe, Wanyama hawajijui na wala hawana uwezo wa kurejea kwa Mollah, kwa matakwa yao wenyewe, lakini binaadamu kapewa uwezo akitaka anaweza kurejea kwa Mollah wake na fahamu zake bila ya kuharibika(Ndio maana wakati wa kufa unaambiwa useme-Laa-illah-illa-Allah)ufe huku unakumbuka na hiyo ndio Ibadah na huko ndiko kukumbuka, kwa hiyo kumbuka sana wakati unakata Roho uwe muangalifu wa kukumbuka (Kalimatul-Tawhid).
Sasa vipi Uislam unakubali mapenzi ya maisha, kwa mtu kustarehe katika ulimwengu huu, Endelea-PART-2

No comments:

Post a Comment