Asalaam Aleiykum,
"إِنَّا خَلَقۡنَا ٱلۡإِنسَـٰنَ مِن نُّطۡفَةٍ أَمۡشَاجٍ۬ نَّبۡتَلِيهِ فَجَعَلۡنَـٰهُ سَمِيعَۢا بَصِيرًا"
"Hakika tumemuumba mwanaadamu kutokana na mbegu ya uhai iliyo changanyika, ili tumfanyie mtihani(Mtihani kwa amri zetu na makatazo yetu)tukamjaalia mwenye kusikia (na)kuona."
Sasa jitizame wewe wala usisubiri mpaka ukaletewa kitabu chako, unaweza kukiona sasa hivi, leo moja jiangalie mizigo ipi kwa siku unayopeleka ndani ya Roho yako, jiulize katika mizigo hii inangia japo aya (10)za Quraan humu ndani, jawabu laa, jee yanaingia mambo ya kheri humu ndani, laa, ukijitizama kwa uyakinifu utajikuta mpaka unakwenda kulala kilichoingia ndani ya Roho yako ni michezo ya senema au mipira, nyimbo za taraab au disco, Mambo ya watu au habari za uongo, maudhui ya siasa au mambo ya kipuuzi na kama utarejeshewa kaseti yako ya leo basi unaweza kwenda mbio, kumbe ndio hivyo ninavyoishi, haya ndio machafuzi ninayo peleka ndani ya Roho yangu, hee mbona zimejaa picha za bendera za chama basi hamna hata picha moja ya makka, ina maana humu ndani mimi sitii chochote cha kheri.
Nilikua simshukuru Mollah wangu alonikirimu huu Uhai nikaweza kuangalia yaliyo ya kheri, sikumbuki mimi kwamba wakati wowote anaweza kuchukua Uhai wake nikawa si chochote bali ni dongo linalofukiwa katika ardhi na huku mimi nalishuhudia. Ewe Ndugu yangu zinduka ujue thamani ya uhai wako, unajua kama thamani ya uhai wako ni sawa sawa na gilasi ya maji inayotolewa bure, jee unayo habari hii!! Unajua kama ukiwa jangwani umebanwa na kiu akaja mtu akakwambia baina ya Uhai wako na mali yako yote na mkeo na wanao na kila ulichonacho thamani yake ni sawa sawa na haya maji unataka niachie mimi hivyo vyote na wewe chukua hii gilasi ya maji unajua kama utatoa bila ya kujishauri.Sasa ikiwa Gilasi ya Maji ina thamani kuliko mali yako, kuliko Uraisi wako, Kuliko Ubunge wako, Kuliko Ubalozi wako, kuliko Utajiri wako kuliko Cheo chako, kuliko vyote ulivyo navyo basi kwanini humfati huyu mwenye maji, kwanini huanzi safari ya kwenda kwa mtoa maji buree bila hata ya ndururu, kwanini hufati amri zake na makatazo yake. Ikiwa maji thamani yake hii nini habari yetu sisi ya hayo mengine ya jicho halijawahi kuona na sikio halijapata kusikia.
Umepewa hayo Macho na masikio ili upate kuongoka na kushukuru basi yatumie kwa kutizama mambo ya kheri, kusikiliza mambo ya kheri, utende mambo ya kheri hilo ndio dhumuni la kuumbwa kwako, lakini wee, kilichomo ndani ya roho yako ni kero tupu, ndani umejaa matamanio, ukimtizama mtu unaanza kupanga nikimpata itakuaje, itakua jinsi kadha wa kadhaa, halafu itakua vile na hivi, na kama ghafla litaondoshwa pazia tuone una fikiri nini tutaona senema nzima ya mchezo wa maasi, haya ndio tuloyajaza ndani ya Roho zetu, kama si utajiri kiburi, kama si uongo rushwa, macho yanaonesha maradhi sisi na wagonjwa hatuna tafauti, tafauti ni ndogo sana wale wanaumwa mwili, na sisi wengine tuna maradhi ya roho, sasa Mwanaadamu ufanye nini?ENDELEA PART 4
No comments:
Post a Comment