Saturday, December 8, 2012

MAISHA YA KIDINI PART 3

Asalaam Aleiykum,

"وَفِىٓ أَنفُسِكُمۡ‌ۚ أَفَلَا تُبۡصِرُونَ"
"Na katika nafsi zenu jee hamuoni"
Mwenye-enzi-Mungu ana tutaka tujiangalie ndani ya nafsi zetu, tukisha jiangalia na kujisafisha utakutana na utajiri mkubwa usokua na mfano wake, "Ewe mwanaadamu jitizame nafsi yako utagundua utajiri mkubwa sana na kama huelewi basi haitoshi hii afya kuwa dalili kwako.
Vipi ujitizame, jitizame sababu bado unaishi nje, sasa wacha nikupe mifano ili uitizame humo ndani upate kujibadilisha, kumbuka zoezi hili la mwanzo vitu unoweza kuvitizama ni hivi, Wivu, Chuki, Hasira,Hamaki,Huruma,furaha, na Mapenzi vyote hivi vimo ndani ya nafsi yako, Basi hebu chukulia mfano huu, Mwanao kafanya kitu kimekukera, jambo la mwanzo wewe hutizami ndani ya nafsi yako ila unatizama nje kwenye hiyo kero yenyewe, na hiyo kero pengine ni maneno tu yule mtoto kakujibu au Mkeo basi kama utaachiwa unaweza kupata (Heart-Attack)kwanini kwa sababu unaishi nje, hebu rejea ndani umekerwa sasa jiulize nini kinatokea ndani ya nafsi yangu, kwanini nakereka hizi hamaki ni kitu gani, jee hichi kitu cha kunihamakisha, basi ukiweza kufanya mara mbili tatu ukawa unakumbuka kuitizama nafsi yako utaanza kuona kitu kipya kinatokea juu yako itakua hamaki zikitokea na mtazamo unatokea na ukiendelea na zoezi hili itafika wakati kabla ya hamaki kutokezea mtazamo ushafika, Na hapo tena unakua ushaanza kubadilika unakua na uwezo wa hamaki kuzigeuza huruma na ukiweza kufanya hivyo ushaanza kuishi maisha ya kidini utaanza kupata upole ambayo inafatia na Imani, hapo tena maisha yanabadilika moja kwa moja.
Na kama una wivu basi pale tendo la wivu linapotokezea wewe usitizame nje kwenye tendo jitizame mwenyewe ndani huu wivu ni kitu gani nini kinatokezea, ukiweza kufanya hivo basi kinachotokezea hapo ni mabadiliko ya wivu kugeuka mapenzi,Vipi?Utajiuliza vipi wivu ugeuke mapenzi wakati mie nampenda ndio nikaona wivu, Jawabu Naam wivu si mapenzi, wivu ni sumu ya kutaka kukikamata kitu kisikutoke mpaka kile kilokamatwa kinaanza kusikia dhiki. Basi irejee tena kuitizama hamaki, hamaki haikai nje ila inakaa ndani ya kifua chako, kama maji yalivo mtungini ukiyatia kata yanatibuka, ndio maana na wewe mtu anafanya jambo nje lakini unatibuka ndani, Bwana Mtume s.a.w kasema"Ukipandwa na hamaki basi kaa kitako", Maana yake? yatulize maji, wewe chunguza ukikaa kitako hamaki zinapungua au kutoweka kabisa, au jaribu ukishikwa na hamaki badilisha mazungumzo utaona hamaki inatulia hata hujui inakwenda wapi(Basi katika nafsi zenu hamuangalii)basi kuanzia leo ukipandishwa hamaki jitizame ndani ya nafsi yako nini kinatokea, utagundua kuna(energy)fulani inatembea na ukiendeleza zoezi hili kwa muda wa siku 90 utakuja kuona kabla ya hamaki kufika unatangulia wewe muangaliaji, na muangaliaji akiweza kumudu kuvishudia vitu viwili vitatu katika nafsi yake tayari anaishi maisha ya kidini, hapo ukitaka kujionesha huwezi tena utakua unajisuta mwenyewe ndani kwa ndani, utakua hutaki tena yale maisha ya nje niloyataja mwanzoni na hapo ndio unafunguliwa Ilham ya kuishi kama inavotaja aya hii.Endelea 4

No comments:

Post a Comment