Asalaam Aleiykum,
Unakaribia wakati kwa baadhi yetu kupewa vidonge vya kulala na Muangalizi wetu wa malazi Shetani(Ibilis). Jee unawajua wale wanolala mwaka mpaka mwaka, Jee umejitizama kama na wewe umo katika hao walalao, Hao ni wale ambao wanaanda na kusheherekea mwaka mpya, wanajifunga kwa kuandaa makuku ya kuchoma, makatlesi ya samaki, chupa za whisky nk, na pia wale wanokwenda kununua vinywaji baridi kama juice na soda wote wanashiriki katika kuandaa malazi ya mwaka mzima ili wapate kumsahau Mollah wao kama anavo himiza (Ibilis)ili wapate kuamka (December 31)mwakani. Hawa wote wanatumia miezi yote 12 kutenda maovu na machafu kwa ajili ya kuhudhuria siku hii moja na kunywa hichi kidonge cha mwaka mpya.
Na cha kusikitisha zaidi wengi wetu katika Imani ndio tunashiriki sherehe hizi nini anatwambia Mollah wetu alipotutumia ujumbe kupitia kwa kipenzi chetu Bwana Mtume s.a.w. sura ya kahf aya ya 1-3,"ٱلۡحَمۡدُ لِلَّهِ ٱلَّذِىٓ أَنزَلَ عَلَىٰ عَبۡدِهِ ٱلۡكِتَـٰبَ وَلَمۡ يَجۡعَل لَّهُ ۥ عِوَجَاۜ "
"Sifa zote anastahiki Mwenye-enzi-mungu ambaye amemteremshia Mja wake kitabu,(Ambacho)hakukifanya kuwa na kwenda upande (upungufu).
" قَيِّمً۬ا لِّيُنذِرَ بَأۡسً۬ا شَدِيدً۬ا مِّن لَّدُنۡهُ وَيُبَشِّرَ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ ٱلَّذِينَ يَعۡمَلُونَ ٱلصَّـٰلِحَـٰتِ أَنَّ لَهُمۡ أَجۡرًا حَسَنً۬ا "
"Kimetengenea vizuri(Kwa ukamilifu)ili kiwaonye watu adhabu kali itokayo kwake(Mollah wako)na kiwape habari njema wale wanoamini ambao wanafanya matendo mema, yakwamba watapata malipo mema"."مَّـٰكِثِينَ فِيهِ أَبَدً۬ا""wakae humo(katika hayo malipo)daima.
Wametajwa makundi mawili kwanza wale wanokwenda kujilaza wameambiwa nyie nendeni lakini kumbukeni kuna adhabu kali itokayo kwake ikiwa mtajilaza na kutenda maovu, na lile kundi la pili litakalo jizuia na kukaa macho likaelekeza imani zao kwa Mwenye-enzi-Mungu basi juu yao kuna malipo yasokatika yatadumu milele.
Haya mambo ya kuitikadi mwaka mpya ni wito wa Shetani(Ibilis)kama vile mnavoitwa kufunga Ramadhani na shetani ana siku yake nayo ni hii mwaka mpya, Na huizungusha shetani siku hii kwa sumu ya vivutio mbali mbali ili upate kwenda ukameze kidonge chake cha kulala mwaka mzima na kidonge chaweza kupenyezwa kokote ndani ya pombe au juice au kwenye chakula chochote, alaa usikatae mbona anakushawishi wala humuoni atashindwa kukutilia kidonge kwenye sambusa, sina haja ya kukutisha kasheherekee mwaka mpya halafu kama utaweza kuamka jitizame mwaka mzima matendo yako umekula kidonge au hujala.
Sasa nataka nifahamu vipi nalala mwaka mzima?
Inakuaje mwenyewe nakua sijui kama nimelala,
Kulala kuna tabaka(Level)3, Tabaka ya kwanza ni ile Unalala(Fofoo)umepotea kabisa hujui chochote umerejea kwa Mollah wako kwa ukamilifu, ndio maana ukiamka unajisikia fresh, umelala vizuri sana hujaota wala kusikia chochote, kulala huku tunaita kurejea kwa Mollah wako(1).Ama kulala kwa aina ya pili huendi kokote unabakia kwenye (Body)yako na hapo ndio tena unapata ndoto hizi na zile, huku ndiko kulala kwa aina ya pili(2). Ama kulala kwa aina ya tatu huku ni kulala ukiwa macho, na mifano ya kulala ukiwa macho ni kama vile maji yametoka(Kupwa) baharini akaja mtu kukuuzia kiwanja kwenye kando ya bahari maji yakirudi huna kiwanja, Au sasa hivi unasoma mawaidha haya lakini unakumbuka hadith fulani kwenye ile hadith ndio unakua umeamka na kwenye haya mawaidha utakua umelala, au mfano wengine ukenda kusali, kwenye ile sala unakua umelala na unaamka kwenye biashara jitizame wewe fikira zako zinakua wapi wakati unasali, na huku ndio kulala aina ya (3).
Na zaidi ya kulala huku kama vile unavo jilazimisha kwa unywaji wa pombe, usikilizaji wa Taarab ili upate kusahau kumbuka husahau tafrani zako tu bali unamsahau na Mollah wako, hizo ndio juhudi zako zote unazofanya ili upate kulala kwa mwaka mzima huku unakumbuka maasi na hicho ndio kidonge cha shetani na
madawa ya kulevya yapo ya aina nyingi tizama ishara halafu utajijua umelala kwa kula kidonge cha mwaka mpya au uko macho, tizama wewe ukimkuta mkubwa wako anachukua rushwa jee wewe utaacha au utazidisha kuchukua, angalia ukimkuta Sheikh anatizama TV na huku kakwambia haramu wewe ukirudi nyumbani unaweza kuweka senema nzima,Shetani siku zote ana kuamsha kwenye maasi ndio maana na kutahadharisha kwenda kwenye sherehe hizo, Jitizame unavo kuwa mvivu kwenye mambo ya kheri sababu umelala, Angalia Ramadhani ikimalizika unavokua, unajua kwanini, sababu Ramadhan inakuamsha na mwanaadamu jambo la kuamshwa halipendi kabisa, ndio maana ikifika Ramadhani ya 29 wengine washalala kwa pombe na maasi mengine, sasa anokua macho anakua na hali gani, na Muumin anatakiwa asherehekee nini? kutaka kupata taaluma ya SHEREHE ZA SIKU MPYA, ENDELEA-PART-2
No comments:
Post a Comment