Asalaam Aleiykum,
"إِنَّ فِى خَلۡقِ ٱلسَّمَـٰوَٲتِ وَٱلۡأَرۡضِ وَٱخۡتِلَـٰفِ ٱلَّيۡلِ وَٱلنَّہَارِ لَأَيَـٰتٍ۬ لِّأُوْلِى ٱلۡأَلۡبَ()ٱلَّذِينَ يَذۡكُرُونَ ٱللَّهَ قِيَـٰمً۬ا وَقُعُودً۬ا وَعَلَىٰ جُنُوبِهِمۡ وَيَتَفَڪَّرُونَ فِى خَلۡقِ ٱلسَّمَـٰوَٲتِ وَٱلۡأَرۡضِ رَبَّنَا مَا خَلَقۡتَ هَـٰذَا بَـٰطِلاً۬ سُبۡحَـٰنَكَ فَقِنَا عَذَابَ ٱلنَّارِ "
"Hakika katika kuumbwa mbingu na ardhi na (katika)kutafautisha usiku na mchana, ziko alama kwa wenye Akili".Ambao humkumbuka Mollah wao wakiwa wima na wakikaa na wakilala, Hufikiri umbo la mbingu na ardhi, (husema)Mollah wetu huku viumba hivi bure, Utukufu ni wako, Basi tuepushe na adhabu ya Moto".
Hapa lazima ieleweke kukumbuka sio kule kusema Laa-Illah-Ilah-Allah kwa maneno, bali kusudio lake ni kuishi na Mollah wako nyakati zote ukiwa kazini unafanya kazi zako, Basi uwe unajua Mollah wako yupo moyoni kwako unamkumbuka kama hivi, Mollah wangu kanipa afya leo naweza kutekeleza kazi yangu, Mollah wangu kanipa ujuzi nafahamu kazi yangu, Mollah wangu kanipa maarifa naweza kufanya Biashara, Mollah wangu yu karibu na mimi ananinusuru na mambo mengi, ana ni Ruzuku fahamu hii ya kuweza kumkumbuka na kutekeleza wajibu wangu, yeye ndie alofanya nipandishwe cheo hichi, sasa ikiwa kazi ya kukaa au kusimama au umepanda farasi au gari basi mote humo unawajibika kumkumbuka Mollah wako, ikiwa umeweza kukumbuka hamaki, hasira na mengineyo huwezi kumsahau Mollah wako, na ukiipata Rehma hiyo wewe sasa unaishi Maisha ya Kidini, lakini huwezi kufikia hapo mpaka upitie kujisafisha na kujizoesha kuwa Muangaliaji wa hiyo nafsi kama nilivo taja huko nyuma. Sasa Ukishaanza kuweza kumkumbuka Mollah wako hapo tena ndio utakua na uwezo wa kuanza kufikiri kuumbwa Mbingu na Ardhi na kujua yote haya hayakuumbwa hivi hivi kuna sababu zake unaanza kugundua tena siri za Ulimwengu usije kujishughulisha sasa hivi wakati Mti ulo jirani yako huufikiri utafikiri nyota ilo Mbinguni?basi tena inakutoka ile dua ya Rabbi niepushe na adhabu ya Moto na safari hiyo ya ugunduzi inakuchukua unakua daima umo kwenye furaha, unakua ushagundua hazina iliyomo kwenye nafsi, na huo ni utajiri mkubwa ambao hausemeki na shuruti lake urejee kwenye kifua ukakutane na hiyo (Taqwa)hapo ndipo kwenye utajiri wa kuwashinda matajiri wote.
Na mwanzoni niliposema ni vilevile Rahisi kupata Maisha ya kidini nilikua nakusudia watu wa aina hii Quraan Baqarah 207.
"وَمِنَ ٱلنَّاسِ مَن يَشۡرِى نَفۡسَهُ ٱبۡتِغَآءَ مَرۡضَاتِ ٱللَّهِۗ وَٱللَّهُ رَءُوفُۢ بِٱلۡعِبَادِ"
Kuna katika watu, wauzao nafsi zao kwa kutaka radhi za Mwenye-enzi-Mungu, Na Mwenye-enzi-Mungu ni mpole kwa waja wake.
Unaweza kuyapata maisha haya ya kidini kwa urahisi ikiwa utaondosha Kiburi, Utaondosha Ubinafsi, na usidhani vitu hivyo ni rahisi kuviwacha mara moja, sababu toka utotoni vimeshaota mizizi katika nafsi yako siku zote unatizama nje mara ghafla unaambiwa utazame ndani, ndio maana nikasema vigumu kuyapata maisha ya kidini japo tunayatamani, tizama mifano Sheikh anatoa mawaidha akisha kumaliza ukimfata pembeni kumuomba pesa ya kula tu hakupi japo yeye kazungumzia kuwalisha maskini, sasa kwanini inakua hivyo, sababu yeye mwenyewe hajabadilika anazungumza maneno tu lakini ndani hajajitizama kabisa wala hajui kumekaaje, na kama unabisha mkere kidogo akimaliza kuhutubia utaona hamaki zake zinamshinda jambazi, sababu ni ile ile bado hajabadilika, ninacho sisitiza mimi kwanza jisafishe, ondoa wivu, ondoa chuki, ondoa hamaki, ondoa uadui, ondoa choyo. ondoa hasira, vikiondoka vyote hivyo kifuani kwako utajikuta ghafla umefunguliwa mlango wa hekima, mwenendo wako utabadilika, matendo yako yatabadilika, yatakua sio ya kujilazimisha bali yanatokezea yenyewe kwa desturi ya kidini, utaanza kuona dalili ndogo ndogo zinajitokeza, mtu akikuomba kitu ukimnyima basi utasikia uchungu siku ya pili hata mlevi akikuomba utampa, na huku unasema Mollah wangu umemleta huyu kuja kunijaribu mimi, sikua mimi mwenye kuweza kumnyima.
Utakua unaona ikisomwa Quraan unasikizia kifuani si masikioni tena na huku machozi yanakutoka, ukiona dalili hizo basi jijue sasa tayari ushaingia katika maisha ya kidini, hapo uanze kuwa makini usiruhusu tena mambo ya kipuuzi kuyashiriki(وَٱلَّذِينَ هُمۡ عَنِ ٱللَّغۡوِ مُعۡرِضُونَ)utaanza kuacha kutizama mambo ya kipuuzi puuzi na yasio maana, utakua husikilizi mambo ya kipumbavu pumbavu na ukiweza kuishi katika maisha ya dini basi mpaka kufa kwako mwili utazeeka lakini wewe ndani utabaki(Fresh-Inside)(إِلَّا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَعَمِلُواْ ٱلصَّـٰلِحَـٰتِ فَلَهُمۡ أَجۡرٌ غَيۡرُ مَمۡنُونٍ۬ ) na hiyo ndio njia ilonyooka Mollah wetu atujaalie kwa sote tuipate, Isiwe mawaidha kitu cha kusikiliza na kuona raha, iwe ni kitu cha kukifata ili tupate kurehemewa na huyo ndio atakua aloishi maisha ya Dini, Amin
No comments:
Post a Comment