Saturday, December 15, 2012

DIRISHA LA ROHO- PART-1

Asalaam Aleiykum,

Imekufikia habari pale jambazi au mwizi anapo chungulia dirishani ndani ya nyumba yako? Hali gani inakutokezea, Jee unajijua unavo hangaika kuweka madirisha ya chuma na walinzi, Na usingizi sasa hupati tena. Basi elewa pia hali kama hiyo inakutokezea iwapo mtu atakutizama machoni, Hujioni wewe unavotaka kupigana, unamfata mtu na kumuuliza wewe unanitazamia nini namna hiyo, Umepata kujiuliza kwanini unakua mkali hali hiyo?.
Leo nakupeleka katika siri ilofichika ndani ya macho yako na kama ukiwa mwerevu ukaigundua siri hii basi mafanikio yako yataanzia hii leo, mada hii itakubadilisha kabisa mtazamo wako ulokua nao siku zote. Kwanini nikalizungumza hili la dirisha la Roho, sababu kubwa naona huruma nikitizama macho ya watu na kuona dalili za mateso kila mmoja wetu ana mizigo alobeba kifuani mwake na akawa hajui au hana njia ya kuitua mizigo hiyo.
Wale walosema yakua Mwili wa Mwanaadamu ni nyumba ya Roho basi pia haitokua shaka na haya Macho tulokua nayo kuwa madirisha yake. Sasa kwanini nikayaita madirisha?Nimeyaita madirisha kwa kuwa nyuma ya hayo Macho yako kuna Mtu anachungulia na uthibitisho utaupata kwenye hii sura ya Qiyama aya ya 14."بَلِ ٱلۡإِنسَـٰنُ عَلَىٰ نَفۡسِهِۦ بَصِيرَةٌ۬"
"Bali Mwanaadamu ni Shahidi wa nafsi yake"
Sasa kutaka upate yakini nenda kwenye kioo ukajitizame utaona unajiona sura yako, na hayo macho yako unayaona, sasa jiulize nani huyu mwenye kuona hivi vyote?. Katika safari hii ya kuchungulia ndani ya Madirisha hayo kusudio langu ni kukufahamisha mwenzangu vipi utaweza kusafisha macho yako na kupunguza mizigo iliyomo ndani ya kifua chako ili usije ukawa unabakisha makorokoro mengi yaso faida ndani ya hilo Jumba(Nafsi)yako.
Usije kushangaa mbona sijapata kuyasikia haya, ni vizuri hujapata kuyasikia sasa tulia upate kuzinduliwa katika somo hili la  (Tawhid)na nafsi yako ili upate kupiga mbizi ndani ya bahari hii ya (Sprituality) ENDELEA PART 2

No comments:

Post a Comment