Asalaam Aleiykum,
Ipo njia nyengine lakini wewe upo tayari kuamka kwa njia nyengine, basi kama uko tayari kisome kisa cha Mcha Mungu Bolkiyah aliyemuachisha mwizi kuiba, ilikuaje?. Siku moja katika mji wa Asia mtoto wa Mtawala alikua anaumwa, alimaliza dawa zote Mfalme yule lakini hakupata matibabu ya mwanawe, Mmoja katika washauri wake akashauri wamfate Mcha Mungu Bolkiyah aliyekua anaishi kwenye pango msituni, wakatumwa watu wende kumleta bwana huyo, alipofika Mtawala akamwambia nimepewa habari ya kuwa wewe uko karibu na Mungu, naomba uniombee ili mwanangu apate kupoa, Bolkiyah akasema nitakuombea kwa Mungu lakini shuruti langu ni moja tu sitaki kushukuriwa, Mtawala akasema kwa hilo umepata, Bolkiyah akamuombea yule mtoto kabla hata hajaondoka kitoto kikaanza kurukaruka, alipotaka kuondoka Mfalme akamwambia umesema hutaki kushukuriwa na pia najua hutaki chochote katika mali wala chenye thamani , basi naomba mimi uniridhie nikupe bakuli la kuombea chakula. Bolkiyah akakubali akafungiwa lile bakuli alipotoka nje kulifungua akakuta bakuli la dhahabu na nje wezi wakamuona Bolkiyah ana bakuli la dhahabu mwizi mmoja akawa anamfata nyuma ili apate kuliiba, Bolkiyah alipofika msituni akaingia pangoni mwake ikisha akalirusha lile bakuli nje, mwizi akashangaa sana akaokota lile bakuli na kuingia pangoni akamwambia "Ewe"Bolkiyah mbona leo umenishangaza mie nilikua nasubiri upitiwe na usingizi ndio niingie niibe lakini leo umeniistaajabisha umenirushia nje ili nisipate hata shida ya kukusubiri, inaonesha umekinai huna haja na chochote cha Ulimwengu huu, basi nakuomba nifundishe na mimi niondoke katika hali hii ya kudhulumu mali za watu, niwache mimi hii tabia ya wizi, Bolkiyah akamwambia nitakufundisha lakini itabidi uendelee kushangaa , nitazidi kukushangaza akamwambia nifundishe sasa sishangai tena.
Bolkiyah akamwambia kuanzia leo nenda kaendelee kuiba kwa muda wa mwezi mmoja, lakini kila ukitaka kuiba fanya jambo moja, kumbuka sasa naiba, Yule mwizi akaondoka baada ya siku kumi karudi kwa Bolkiyah machozi yanamtoka anamwambia umenifanyia (Trick)gani sasa siwezi kuiba tena(Nishaamka)kila nikitaka kuiba nakumbuka, na kila nikikumbuka ina nijia fikira yakua nadhulumu, na ikija fikira hiyo nakua siwezi tena dhuluma ya wizi, basi kuanzia hapo yule mwizi akawa mwanafunzi wa Bolkiyah na akawa Mcha Mungu na mji mzima ukapata habari na kushangaa kwa ghafla jambazi lile kubadilika, hiyo ndio njia alotumia Bolkiyah kumuamsha huyo mwizi, sasa kama na wewe itakufaa itumie kabla hujadhulumu au kwenda (Jela kwa sheria za siku hizi).
Na huo uzinifu vilevile unaweza kuamka, kwa kuwa sasa hivi umelala na umebadilisha mwenendo mwanzo matamanio yalikua (Nature)lakini umeyabadilisha kuyapeleka Akilini sio (nature) yamezama kwenye (Mind)unafikiri wakati wote ukipewa salamu aleiykum unatafsiri anataka, ukikosa mwanaadamu unakimbilia magazetini, ukikosa kwenye magazeti mbio kwenye video, sasa nini ufanye amka na wacha (Nature)ifanye kazi tena, utaona umerejea kuwa binaadamu mwenye akili timamu na afya iliyo nzuri, kila yakikujia mawazo machafu kuwa (Alert)matamanio hayo, ukiwa unayagundua pale yanapokuja au ukazuia pumzi ghafla utaona yanapotea, au pitia maudhui zilizopita ili upate dawa ya kadhia hii.
Nini Dhuluma?Endelea-part-4
No comments:
Post a Comment