Asalaam Aleiykum,
Nini Dhuluma? Dhuluma ni Dhanbi ya ziada, dhanbi lazima apatikane wapili wake ndio iwe dhanbi, lakini kama utajiua(Kutoa Roho yako) haitwi dhanbi inaitwa kajidhulumu, Kwa hiyo elewa ukidhulumu unakuwa umetenda mambo mawili yaani dhanbi na dhuluma, dhanbi ina mahusiano na (Body)mwili na dhuluma ina mahusiano na (Soul)Roho, Ama kuhusiana na dhanbi Mollah wako anasema "atasamehe yale ulomfanyia yeye lakini yale ulowafanyia watu ni lazima mpaka wakusamehe wenyewe""Atakuja mtu siku hiyo aseme Mollah wangu nihukumie huyu alinidhulumu duniani"Mollah atawaambia Malaika chukueni mema yote mumlipe alodhulumiwa ikisha mtieni peponi huyu alodhulumiwa"Ama huyu alo dhulumu makaazi yake moja kwa moja motoni.
"Enyi Madaktari(Doctor)na nyie Manesi(Nurse) nyie Makachero(Polisi)na Nyie Wake kwa Waume, wenye kuwadanganya wenzio jueni hiyo ni dhuluma kubwa, Mna wadanganya wagonjwa, na kuwatesa Raia, mna danganya mpaka nyumbani wake zenu na waume zenu zote hizo ni dhuluma na mtaulizwa siku ya (Kiyama)kwa matendo hayo.(Mfano)Daktari anakuja mwanamke kamleta mumewe mgonjwa anaumwa anataka matibabu pengine maradhi yake dawa elfu 15 unamwambia laki mbili na wao hawana uwezo huo, inabidi atoke yule mwanamke maskini aende kukopa kwa (Kibosile)huko hapewi mkopo mpaka azini, akisha kuzini anapata mimba, akipata mimba inabidi aitoe, au isiwe hivyo, mume anashindwa kupata matibabu huyo anarudi nyumbani na kukata Roho, anawacha vitoto vidogo yatima jueni (Doctor na Nurse)nyote mmo mwanzo mpaka itakapoishia, na mmedhulumu na mtaulizwa siku ya siku au mtaanza kulipwa hapa hapa duniani.
Na kama (Kachero)Polisi umetumwa kwenda kumpiga mtu ukamvunja miguu au kumuua basi mwanzo wa dhiki ya familia ile mpaka mwisho wake wewe unaendelea kuandikiwa dhanbi ya dhuluma mpaka dhiki ile iwaondoke, Na wewe Mume na mke mnopita mkadanganyana jueni pia mnadhulumiana dhuluma ilo kubwa, nyinyi mpewa amana ya maisha yenu, inakuaje leo huyo apite kule na yule apite huku eti kutafuta riziki, eti anafanya biashara hakuna chochote isipokua dhuluma na unaandikiwa dhuluma hiyo labda mpaka mtakapo achana, leo inafikia mtu anazaa vitoto, unaulizwa pesa ya kula unajibu huna ikisha huyo unatoka kwenda kutumia na kimada, atahadhari sana mtu na dhuluma hizi adhabu zake nyinyi hamziwezi, na wameumia wale wenye kuuzaa madawa ya kulevya wao pamoja na familia zao, kwani yule unayemuonjesha unga tokea siku ile alipokuwa mteja mpaka anaingia kaburini dhanbi zake zote unaandikiwa wewe umemdhulumu.
Sasa kama umezinduka kidogo rejea kwa (Boss)Mkubwa wako wa kazi kamwambie leo nimeoneshwa aya ya Quraan imeniamsha sitaki tena kudhulumu nishachoka naomba maghfira kwa Mollah wangu, mwambie nimesoma mimi sura ya Ibrahim aya ya 42-49-50 inasema:"
"وَلَا تَحۡسَبَنَّ ٱللَّهَ غَـٰفِلاً عَمَّا يَعۡمَلُ ٱلظَّـٰلِمُونَۚ إِنَّمَا يُؤَخِّرُهُمۡ لِيَوۡمٍ۬ تَشۡخَصُ فِيهِ ٱلۡأَبۡصَـٰرُ"
"Wala msidhani Mwenye enzi Mungu ameghafilika na (haya)wanayofanya Madhalimu, Hakika amewakhairishia tu mpaka siku ambayo macho yatatoka(Kwa khofu)"
" وَتَرَى ٱلۡمُجۡرِمِينَ يَوۡمَٮِٕذٍ۬ مُّقَرَّنِينَ فِى ٱلۡأَصۡفَادِ"
"Na utawaona wakosa siku hiyo wamefungwa katika minyororo"
"سَرَابِيلُهُم مِّن قَطِرَانٍ۬ وَتَغۡشَىٰ وُجُوهَهُمُ ٱلنَّارُ"
Nguo zao (siku)hiyo zitakua za lami na Moto utazijia nyuso zao(Kuziunguza).
Hayo ni baadhi ya mambo yatakayo wapata wenye kufanya dhuluma ya aina yoyote ile, siku hiyo ya kiyama, na ukitaka kujua duniani kinawafika nini-Endelea-part-5
No comments:
Post a Comment