Asalaam Aleiykum,
Mambo yenyewe la kwanza ni ile (Tohara)inayopatikana kutokana na usafi wa viungo kama ilivo taja aya ya sita ya surat Maidah halafu kuna la pili lake karibu na mwisho wa hiyo aya ambalo ulikua hulijui limo katika (Udhu)" مَا يُرِيدُ ٱللَّهُ لِيَجۡعَلَ عَلَيۡڪُم مِّنۡ حَرَجٍ۬ وَلَـٰكِن يُرِيدُ لِيُطَهِّرَكُمۡ وَلِيُتِمَّ نِعۡمَتَهُ ۥ عَلَيۡكُمۡ لَعَلَّڪُمۡ تَشۡكُرُونَ
"Mollah wenu hataki kukutieni kwenye taabu, bali anataka kukutakaseni na kutimiza neema yake juu yenu,ili mpate kushukuru"
Ipi neema hiyo, ni ile neema ya kusamehewa kila ukitia udhu wakati unaenda kusali kabla hata ya kuanza huko kusali basi Mollah wako kwa Rehma zake anakufutia madhanbi kwa udhu huo, lakini Udhu wenyewe lazima utimie wende kwa adabu na unyenyekevu, ukikosha viganja vyako na mikono(labda)kuna vijidhanbi vya mkono umevifanya katika wakati ule tambua unavifuta, Ukikosha uso labda kuna dhanbi za macho unafutiwa, ukitia maji mdomoni kusukutuwa labda kuna uongo au jambo umesema la dhanbi unafutiwa,ukitia maji masikioni pengine umesikiliza mambo maovu unafutiwa dhanbi zake, ukitia maji kichwani labda ulikua na mawazo mabaya unafutiwa dhanbi zake, ukitia maji miguuni pengine ulikwenda pahala penye maovu kwa hiyo unafutiwa hiyo dhanbi, hii ndio Neema ya Mollah juu yako.Usije ukashtuka hee mbona huyu anasema hivi(Kwanza katafute asili ya neno Tawba)toba utalikuta maana ya asili yake kurejea na wewe unarejea kwa siku mara tano huo ndio Udhu nje Tohara ndani maghfira)na aya inamalizikia ili mpate kushukuru ndipo unaingia katika Sala mwanzo unaanza," ٱلۡحَمۡدُ لِلَّهِ رَبِّ ٱلۡعَـٰلَمِينَ".
Hapo ndipo Bwana Mtume s.a.w alipomuuliza Bilal "Ewe Bilal r.a mimi nasikia nyayo zako peponi una matendo gani unafanya hata ukapata hayo" akajibu Sayyidna Bilal r.a haunitoki Udhu sala mpaka sala.
Sasa ikiwa Udhu unatia kila mara iweje Sala yako kila wakati ni vile vile, itizame sana sala yako isije kuwa mazoea au tabia, ifanye kila wakati kama unavotia Udhu na sala yako vile vile iwe nyengine, kumbuka wakati unabadilika basi na wewe fanya sala yako ibadilike, kama ulikwenda na maombi ya dhiki basi wakati mwengine pia nenda na salamu za shukurani. Usije ukawa kama wale walotajwa katika sura ya (Maun) aya ya 4"فَوَيۡلٌ۬ لِّلۡمُصَلِّينَ"
"Wataona wale wenye kusali(Sala za kinafik)unakwenda tu kupachika sala ikisha huyo unatoka mbio,(5)"ٱلَّذِينَ هُمۡ عَن صَلَاتِہِمۡ سَاهُونَ""Ambao wanapuuza sala zao"(Maamrisho yake).(6)
"ٱلَّذِينَ هُمۡ يُرَآءُونَ""Ambao hufanya(Sala na Amali)zao kwa riyaa(ili kuwaonesha watu namie nasali)(7)"وَيَمۡنَعُونَ ٱلۡمَاعُونَ"Na hunyima misaada"(haitakua na faida sala hiyo) ikiwa maamrisho ya Mwenye enzi Mungu huyatekelezi na huku unataraji kurejea kwa Mollah wako, hata ukirejea ni bure, hata huo Udhu hupati kitu kwa sababu inayosamehewa ni Roho si mwili na ikiwa Roho yako ngumu basi jijue na huko kwa Mollah wako hupati kitu, Sala ikipatikana sawa sawa kwako inakua furaha, sala ikipatikana mazito yanakua mepesi, sala ikipatikana mpaka mwenyewe unajua Mollah ana mapenzi na mimi, sala ikipatikana mpaka khofu ya kufa inaondoka na khofu hiyo ikiondoka kwa mara ya mwanzo ndio unaanza kuishi, huogopi tena kufilisika, huogopi tena umaskini, huogopi tena maradhi ukiwa katika hali hiyo jua sala zako zinafika-Mollah atujaalie kabla ya umauti wetu tupate daraja hiyo sisi na familia zetu.Amin
No comments:
Post a Comment