Asalaam Aleiykum,
Ameniuliza Muulizaji mbona elimu yako chache ulonayo huifundishi kwa wanafunzi maalum, ikisha na wao wakaifundishe, muulizaji lazima alikua na kitu ndani ya maulizo yake, pengine kuna jambo limemgusa, au kuna kitu kinamtesa kuhusu usomeshaji wangu, kwa sababu angekua anataka kuwamo katika hao wanotaka kufundishwa asingeuliza kwa kubeza, inaonesha ana taaluma za vitabu alizokusanya kupitia vitabu mbali mbali, au kwa Mwalim huyu na yule, hajui hata tafauti ya kufundisha na kusomesha.
Nini Tafauti yake?
Kusomesha nikuchukua (Some information)ukampa mtu mwengine, huko ndio kusomesha, unachukua wanafunzi wasioelewa kitu fulani halafu unawahadithia inakua jinsi kadhaa wa kadhaa, unatoa kwenye kichwa chako unapeleka kwenye kichwa cha wengine. Nini kufundisha? Kufundisha ni (Understanding,Wisdom,Inteligence)ndio tena kinapatikana kitu kinachoitwa(Transformation)ya kujua kutokana na hayo mafundisho, Wapi yanatokea mafundisho(Kutoka kwa Mollah wako)(By Knowing itself through experience)hapo tena ndio inapatikana hiyo kujua.Mfano Gari inasomeshwa, lakini Baskeli inafundishwa, kuogelea Baharini unafundishwa, lakini kukoga tohara unasomeshwa. Vipi leo niweze kufundisha wakati mie mwenyewe sijamaliza kujifunza.
Alipojiwa Mtume s.a.w na Malaika Jibril a.s aliambiwa maneno haya mawili kusomeshwa na kufundishwa, ili tupate kuyajua kwa makini maneno hayo hebu na tuihudhurie aya 1-5 sura ya (Alaq)
"ٱقۡرَأۡ بِٱسۡمِ رَبِّكَ ٱلَّذِى خَلَقَ"
"Soma kwa jina la Mollah wako aliyeumba"
Neno la Mwanzo kaambiwa soma kwa jina la Mollah wako aliyeumba, tizama vipi unaingia katika tafsiri ya maneno haya, namna gani utaishi ndani ya maneno haya matukufu, kwanini kaambiwa soma wakati Mwenye-enzi-Mungu anajua Mtume s.a.w hajui kusoma, vipi leo atasoma, kutokana na tamko hilo kimedumu kitabu hichi kitukufu mpaka hii leo, kimefasiriwa na wanazuoni mbali mbali ulimwenguni, na kinaendelea kusomwa kama kilivo anza kwa tamko la Soma kwa jina la Mollah wako aliyeumba, kwanini ikawa kwa jina la Mollah wako, kwa sababu vyote unavovijua kwenye ulimwengu huu na usivovijua kaviumba yeye, kwa hiyo kama utasoma basi ni kwa jina lake yeye asiyekua na mshirika, kila kitu chanzo chake ni yeye na marejeo yake ni kwake, hakuna kinachotokea (out of nothing). Lakini unapoambiwa soma moja kwa moja unaangukia kwenye(Intellectual)na huo si muradi wa kusudio lake hapo, unaweza kusoma ulichofundishwa, hiyo ndio maana ya hiyo(aya)lakini huwezi kufundishwa ulichosoma vitu viwili tafauti, Kufundishwa ni tukio linalotokea ndani yako(Experience)kama mwanamke hajawahi kuzaa vipi utamfundisha uchungu unakuaje, lakini alokwisha kuzaa anakua kashafundishwa uchungu ukoje anaujua kutokana na uzoefu, na huko kujua ndiko kufundishwa, vipi leo mimi nitaweza kufundisha.
Usije kukimbilia kwa Mwalimu sana analoweza atakupa masomo lakini hawezi kukufundisha, kusoma ni (Theory)ndio maana Bwana Mtume s.a.w akaambiwa "Mollah wako aliyeumba"
"خَلَقَ ٱلۡإِنسَـٰنَ مِنۡ عَلَقٍ"
"Kamuumba mwanaadamu kwa pande la Damu"
Ukimtizama mwanaadamu huoni pande la Damu, hapo imetumika kusoma, lakini ukenda ndani na kuanza kumchambua utakuta kweli ni pande la damu, na huko ndio kufundishwa, umegundua kama ni damu, umepata kufahamu (through understanding).
"ٱقۡرَأۡ وَرَبُّكَ ٱلۡأَكۡرَمُ "
"Soma(Kwa ajili ya)Mollah wako ni Mkarim"
Kakufanyia ihsani kubwa ya kuweza kukupa ufahamu wa kufundishwa, sasa ushayajua maisha, kakufanya Khalifa katika hii Ardhi, kakufundisha jema na baya ili uishi kwa salama, kakupa kila kinachohitajika katika maisha yako, anakuruzuku na kukuponesha maradhi unapoumwa, anakulea mpaka unakamilisha umri wako katika ulimwengu huu basi sasa yasome yote yalokuzunguka ili upate kuujua Ukarim wake.
Endelea part 2
Sunday, April 28, 2013
SINA CHA KUFUNDISHA PART 2
Asalaam Aleiykum,
"ٱلَّذِى عَلَّمَ بِٱلۡقَلَمِ"
"Ambaye amemfundisha Mwanaadamu kwa wasita(Uwezo)wa kalamu(Akili)"Kiungo kinotumika ni hicho hicho mwanzo ni kwa ajili ya kufundishwa, na mwisho wake ni kusomeshwa, mwanzo ni ya kudumu, na ya pili ni ya muda, na zote mbili atakapo Mungu huziondosha elimu hizo kama alivosema katika sura ya an-Nahl aya ya 70 " وَمِنكُم مَّن يُرَدُّ إِلَىٰٓ أَرۡذَلِ ٱلۡعُمُرِ لِكَىۡ لَا يَعۡلَمَ بَعۡدَ عِلۡمٍ۬ شَيۡـًٔاۚ"
"Na miongoni mwenu wako wanorudishwa katika(Umri wa uzee)akawa hajui chochote baada ya ujuzi(alokua nao)"mpaka mwisho wa aya inapomalizikia, inaondoshwa kabisa elimu na kujua, inabakia (Nafs)bila ya taaluma yoyote, mafundisho yashapotea, na sasa umebakia kuwa mzigo kwa wale wenye kujua wakutumikie, na wao wanakutizama hawana uwezo wa kukufundisha tena, kwa hiyo kutoka kwenye kufundishwa kwenda kwenye kusomeshwa halafu kurejea kwenye (Nothingness)ukiyajua hayo, basi toka machozi kwa ajili ya Mollah wako aliye Mkarim, fanya hima kumkumbuka na kunyenyekea kwa ajili ya hisani hii ya kufahamu aliyokujaalia, vipi mimi leo nitakua nina uwezo wa kufundisha.
"عَلَّمَ ٱلۡإِنسَـٰنَ مَا لَمۡ يَعۡلَمۡ"
"Akamfundisha Mwanaadamu (chungu ya )mambo aliyokua hayajui" Kusoma ni (Capacity)ya (Memory)ikiwa akili yako ina kumbukumbu nzuri basi moja kwa moja unakua hodari, kusoma sio (Future)kusoma ni (Past), Lakini kufundishwa ni (Communion)kitu chenye kutokea ndani, pahala pasipojulikana, (Mfano unatengeneza gari ushakwama, hujui ufanye nini uko porini na usiku unaingia simba washaanza kuunguruma, mara inakujia katika Akili yako tia msumari gari itawaka, na kweli ukiweka msumari gari imewaka)huko ndio kufundishwa,(Akamfundisha chungu ya mambo asiyoyajua).
Vipi leo niweze kufundisha wakati mie mwenyewe nafundishwa, Katika Ulimwengu huu kila kitu ni maajabu, kila leo siku ya mafundisho, ulivolala jana, na uliyoyatenda jana yanaweza kuwa masomo, lakini yanotokea leo yote ni mafundisho, jogoo kawika , mtoto kazaliwa, mti umekatwa, fulani kafariki yote hayo ni matukio katika maisha na kila tukio si kusomeshwa bali ni kufundishwa, na ukijaribu kukimbilia kwa Mwalim atakupa masomo lakini sio mafunzo, unaweza kujifunza ukikaa na Sheikh na ukasoma bila ya Sheikh kufungua mdomo, lakini unatakiwa wewe mwanafunzi jee uko tayari kusoma kwa njia hiyo, au ndio unakaa kwa Sheikh unangoja akosee tu upate(kumla nyama), mwanzo lazima upate mafunzo vipi utasoma kutokana na ukimya wa Sheikh, kwa wale wanojua kufundisha basi wanakua hawana haja ya kusomesha, mnaweza kwenda kwa Sheikh au Mwalimu, akasoma aya moja mkakaa masaa matatu mnachambua aya moja na mkiondoka mfano wake mmesoma (Kitab kizima).
Kufundishwa yatakiwa uende mwenyewe katika barabara ya maisha ndio kidogo kidogo utaanza kujua hili shimo, lile bonde, huyu ngamia, huu mlima, hili jabali, zile nyota, hapo hutaki kusomeshwa, hapo unataka kufundishwa na mfundishaji ni mwenyewe Subhanna, na anakujulisha moja baada ya jengine katika ufalme wake, vipi mimi leo nitakua na uwezo wa kufundisha,
Tizama mtoto mchanga anavofundishwa akiwa kwenye maji, sio kwa sababu mwepesi au anajua kuogelea bali anafata sheria ya maji,inasemaje, utakapoingia basi usipaparike, usishtuke, haina haja ya kufanya chochote utaelea, lakini ngoja sasa upewe (Swimming lesson)uone mambo, angalia unakuaje au muangalie yule anofahamishwa anakua vipi,watu wanatia masomo katika akili yake , hofu inamuingia ndani ya akili, anahisi sasa hivi ndio nazama, nitakufa mie, lakini baada ya muda akiwa peke yake akafanya hivi na vile mara anapata maarifa anajiona anaelea, kashajua siri ya kukaa kwenye maji bila ya kuzama, hapo mafundisho yashamteremkia.Na kama memsahau mfundishaji ni nani basi endelea part 3

SINA CHA KUFUNDISHA PART 3
Asalaam Aleiykum,
Ikiwa mtu kakudanganya yeye anafundisha, yeye anajua yasojulikana basi irejee Quraan sura ya Baqarah aya ya 31uone inasemaje."
"وَعَلَّمَ ءَادَمَ ٱلۡأَسۡمَآءَ كُلَّهَا ثُمَّ عَرَضَہُمۡ عَلَى ٱلۡمَلَـٰٓٮِٕكَةِ فَقَالَ أَنۢبِـُٔونِى بِأَسۡمَآءِ هَـٰٓؤُلَآءِ إِن كُنتُمۡ صَـٰدِقِينَ "
"Na akamfundisha (Nabii Adam a.s)majina ya vitu vyote, ikisha akaviweka mbele ya Malaika, na akasema (Kuwaambia)Niambieni majina ya vitu hivi ikiwa mnasema kweli" hivo ndio kufundishwa, ukishajua sasa unaambiwa waambie (wasomeshe majina ya vitu hivi)Vipi kufundishwa, inayofundishwa ni Roho na inayosomeshwa ni akili, vipi inakua, mchukue mtoto mdogo halafu muoneshe embe atajua hiki ni kitu, atakua yeye na kitu anakiona lakini hajui ni kitu gani(Nambieni ikiwa mnasema kweli)mtoto hawezi kusema atakaa ana shangaa halafu atakuuliza hichi nini? Ukimjibu hii inaitwa Embe hapo inakua ushamsomesha, ushambadilisha akili yake, ushatia jina na sasa kila akiona Embe atakua anaikumbuka kwenye (Memory)yake, akiiona tu anaijua (Embe dodo hiyo)Vipi leo mimi nitakua na kitu cha kufundisha.
Sasa ikiwa na wewe unataka kugundua vipi unafundishwa na Mollah wako, kuwa mtulivu, kaa kimya,kaa itikafu, sikiliza ujumbe gani unakuja katika nafsi yako, fanya Ibada za usiku kwa wingi, ghafla utaanza kufungukiwa na elimu ya kujua, najua unajiuliza nitajuaje, hapo itakua Akili ishaingilia kati, na Akili ikiingia ndio unaambiwa sasa soma kwa Jina la Mollah wako alo Mkarim, kwani unajuaje sasa nyanyua mguu, vipi unatambua sasa toa sauti, nenda kalale, kule kuna hatari, kisu kinakata, hii chai ya moto, lile jua hayo ndio machache katika kufundishwa ama kusoma ni (Faculty) ya Akili, kusoma ni kilele cha kufundishwa, kufundishwa ni (Knowing) na kusoma ni (Knowledge) ndio utaona viwili hivi vikikutana utasikia mwanafunzi huyu hodari, na vipi asiwe hodari na yeye kapewa vitu viwili kwa wakati mmoja, na vikikutana viwili hivi ndio anapatikana Sheikh, au Mwalimu, anapatika Mwenye (Degree) au (Professor) na kama hujapata vyote utakua na kimoja chake, ima msomi bila ya hekima, au utakua na hekima bila ya kusoma, namie nawependa wote na nawahimiza sana watu wasome kwani hekima unakua nayo lakini usomi unatafutwa, na mie nawapenda wasomi wanopata vyeti vyao wakapata Riziki zao za halali na kuleta maendeleo katika jamii zao, hiyo ndio maana ya Elimu, kutolewa kwenye giza lolote kupelekwa kwenye Nuru, na hiyo ndio maana ya aya hii." وَوَجَدَكَ ضَآلاًّ۬ فَهَدَىٰ" "akakukuta umepotea akakuongoa"
Yaa Aalim tupe elimu ya kukufahamu weye na Ufalme wako ulotuzunguka, Tuongoze katika Nuru, ututoe kwenye giza.Amin.

Sunday, April 21, 2013
MWANAFUNZI WA KASUKU PART 1
Asalaam Aleiykum,
Darsa yetu ya leo inaanza na kisa cha kasuku aliyekuwa anamilikiwa na mabibi wawili katika mji wa Kiislam, Kama ilivyo desturi ya Miji yetu dini nzima inakua mikononi mwa Sheikh, Dhana yetu inatupa yeye ndiye anayejua na yeye pekee ndie mteule wa kutukamatia mfumo mzima wa dini, na anachosema yeye hakina makosa ndani yake, vipi itakua na makosa wakati yeye kasoma vitabu, anajua hadith na akiisema hadith moja ndio inakua muongozo mzima wa dini unategemea hadith hiyo, hiyo ndio hali tulo nayo hivi sasa. Kumbuka hii ni hadith ya Kasuku na kama ilivyo hadith yaweza kuwa ya ukweli imetokea au ya uongo imetungwa, lakini upo kwenye darsa usizuke ukaanza kubaki kwenye hadith ukakosa mafundisho ndani ya hadith hiyo, kama yanafaa chukua na kama hayafai yaache ndani ya hadith hiyo, na ukifanya hivyo haitokudhuru chochote hadith hii.
Naam, Kama ilivyo Desturi ya sisi Masheikh tunapenda kufanyiwa Takrima za Ugeni, tunapenda (Mahanjumati)mialiko ndio maradhi yetu, sasa katika mji huu kulikuwa na hawa Mabibi wawili maskini wakipenda sana mambo ya dini na wakitaka kufanya japo machache yenye kheri wakaamua kumualika Sheikh wao, wakamuandalia hapa ndizi mbivu, machapati, sambusa ziko hapo , pale kuna mikate ya ufuta nk, takriban walijitahidi ili mgeni wao apate kufurahi, alipohudhuria yule Sheikh akawa anazunguka kwenye sahani zote ziloandaliwa na chakula kilikua kitamu mno, baada ya kumaliza akaomba dua na kuwaambia wale mabibi nimefurahi sana na chakula chenu na Insha Allah nitakua mwenye kuja kila Alkhamis kutia baraka kwenye nyumba hii. Ikawa ada ya Sheikh yule miezi nenda miezi rudi, na dua yake hiyo hiyo moja, Mungu akujaalieni afya, mzidi kupika vyakula vizuri zaidi.
Mwanaadamu ndio mwanaadamu wale Mabibi wakachoka na hali ile, na Mja akichoka ana aina mbili katika machaguzi ama atafanya visa, au atasimanga, wale mabibi wakaamua kusimanga miezi nenda miezi rudi, washamchoka Sheikh, akitoka wanatukana matusi yaso idadi, Sheikh gani, mroho mkubwa, anatupa dhiki, hatuna uwezo, dua yenyewe moja tu kama kameza keseti, na hivi na vile wakati wanasema haya Kasuku kakaa kimya anawasikiliza, walipogundua Kasuku atawakashifu wakafanya ada Sheikh kabla ya kuingia wanamfunika Kasuku. Siku moja ikatokezea Sheikh kasahau kitabu chake kinachoitwa (Mwenye kuyajua yalofichikana)ikabidi kabla ya kwenda Msikitini apite kwa wale mabibi ili akachukue kitabu chake, alipogonga Mlango, wale Mabibi moja kwa moja wakaufungua ikawa mbele yao kasimama Sheikh, wakawa hawana budi kumkaribisha ndani, alipoingia ndani baada ya kutoa salamu, Kasuku akasikia sauti ya Sheikh na mambo yakaanzia hapo, Kasuku akaanza kusema kila alokua anasikia, Mroho mkubwa, kazi kufakamia makatlesi na sambusa,Alkhamis haijafika umekuja tena, si Sheikh chochote, kusikia matusi ya kasuku yanazidi ikabidi kwa aibu wale mabibi wakimbilie jikoni, Sheikh kainamia chini, Kasuku akasema yote mpaka alipomaliza yale yalotiwa katika kichwani mwake kasuku akanyamaza, aliponyamaza Sheikh akachukua kitabu chake akatoka, waliposikia mlango umefungwa wale Mabibi wakatoka jikoni wakaja ukumbini, ikawa macho yao wao na kasuku wanatizamana, Kasuku akasema sasa nifunikeni.
Na hivi ndivo kila mmoja wetu anavoendelea na maisha yake, ama anajifunika mwenyewe au anaomba sasa nifunikeni, Usikubali ukawa maisha yako kama kasuku, Kasuku anasema alosikia, ndio maana wengine ukiwagusa (Hususan Wasomi) wanahamaki sana maana yake anajijua yeye ni Kasuku, kakusanya taaluma fulani ya kupatia maisha, baada ya hiyo taaluma ananyamaza kimya kama kasuku, na mimi nafanya hivi ili kuondosha kiburi, huwezi kuwa Mcha Mungu kama una kiburi, kwa hiyo napagusa kwenye hicho kisomo chako ili nikushushe tuwe sawa, nikutoe kwenye (Tundu la Kasuku)kwa hiyo usichukie ukafanya (Personal)ukasusa natumia nyezo katika nyenzo zangu nyingi za kuvunja (Viburi)Naam usikubali mwalimu wako akawa kasuku utakua hasarani, Usiishi maisha yako kama Kasuku ikawa wewe muigizaji, umeona watu wamefanya na wewe umefanya, mpaka dua zako zitizame unataka pesa lakini unasoma sura ya (Zilzal)unashida nyengine lakini unatumia Dua ilotungwa miaka 100 ilopita, basi wewe huna hata uwezo wakutunga dua yako ya kuomba, mpaka uwe kama Kasuku.
Sasa unajiuliza mimi niwe vipi, ukitaka kujua uwe vipi Endelea Part 2

MWANAFUNZI WA KASUKU PART 2
Asalaam Aleiykum,
Sasa uwe vipi, kuwa kama ndege (Hud Hud)yeye alikuwaje, itabidi tumuulize Nabii Suleiman a.s katika kisa cha Quraan alikuwaje (hud hud)Sura ya Naml aya ya 20,21,22,23,24
" وَتَفَقَّدَ ٱلطَّيۡرَ فَقَالَ مَا لِىَ لَآ أَرَى ٱلۡهُدۡهُدَ أَمۡ ڪَانَ مِنَ ٱلۡغَآٮِٕبِينَ"
Akawakagua Ndege(ikawa hudhud hayupo)Akasema imekuaje mbona simuoni Hud Hud, au amekuwa miongoni mwa wasiokuwepo hapa.
" لَأُعَذِّبَنَّهُ ۥ عَذَابً۬ا شَدِيدًا أَوۡ لَأَاْذۡبَحَنَّهُ ۥۤ أَوۡ لَيَأۡتِيَنِّى بِسُلۡطَـٰنٍ۬ مُّبِينٍ۬"
Kwa yakini nitamuadhibu adhabu kali, au nitamchinja au ataniletea hoja iliyo wazi.
" فَمَكَثَ غَيۡرَ بَعِيدٍ۬ فَقَالَ أَحَطتُ بِمَا لَمۡ تُحِطۡ بِهِۦ وَجِئۡتُكَ مِن سَبَإِۭ بِنَبَإٍ۬ يَقِينٍ"
Basi hakukaa sana mara (Hud Hud akatokea)akasema, Nimegundua usilogundua, na ninakujia kutoka (Mji unaoitwa)Sabaa na (Nakupa)habari yenye yakini.
Naam:usiwe kama Kasuku, hivi ndivo inavotakiwa uwe kama Hud Hud hakuogopa kuadhibiwa au hata kuchinjwa kenda huku na huko(Na hii ndio ile maana ya katafuteni elimu mpaka Uchina)pita hapa na pale usiogope, soma kwa huyu na yule, usisubiri mpaka Sheikh au Mwalimu akupe ruhusa, Hud Hud hakutaka hata ruhusa kenda kugundua ambayo Nabii Suleiman a.s bado hajagundua na elimu yote aliyopewa, na wewe katafute ugundue mji wa elimu ili uje kutupa habari za yakini, sio mambo ya (copy)Sheikh fulani kasema, iwe ndio sawa tu, haiwezekani, usije ukaganda pahala pamoja utafungika kama Kasuku kwenye tundu lake na watu wakufunike, chuma hapa na pale ili maisha yako yapate kubadilika kwani elimu ndio njia pekee itakayo kutoa kwenye Giza kukupeleka kwenye Nuru, Soma ugundue jambo jipya kama Hud Hud, na kama hujagundua au kuendelea basi jijue wewe Kasuku wala usione haya kasuku pia ndege.
Naam nini kagundua Hud Hud, na habari gani hiyo yenye yakini,
" إِنِّى وَجَدتُّ ٱمۡرَأَةً۬ تَمۡلِڪُهُمۡ وَأُوتِيَتۡ مِن ڪُلِّ شَىۡءٍ۬ وَلَهَا عَرۡشٌ عَظِيمٌ۬"
Hakika nimekuta mwanamke anatawala, naye amepewa kila kitu, na anacho kiti cha enzi kikubwa.
Kapewa Mali na uzuri, na nchi yake ya Sabaa ilikua nzuri, na kiti alichokua akikalia kilikua cha aina ya pekee, na kikubwa cha kutawala Malkia.
"وَجَدتُّهَا وَقَوۡمَهَا يَسۡجُدُونَ لِلشَّمۡسِ مِن دُونِ ٱللَّهِ وَزَيَّنَ لَهُمُ ٱلشَّيۡطَـٰنُ أَعۡمَـٰلَهُمۡ فَصَدَّهُمۡ عَنِ ٱلسَّبِيلِ فَهُمۡ لَا يَهۡتَدُونَ "
Nimemkuta yeye na watu wake wanalisujudia jua badala ya Mwenye-enzi-Mungu, na Shetani amewapambia vitendo vyao na akawazuilia njia(Za Kheri)kwa hivyo hawakuongoka.
Hebu na wewe jaribu kuwa Hud Hud utuletee habari leo kama utakua Hud Hud utagundua miji ilivochafuka, si kwamba watu wanasujudia Jua tu, bali sasa wamezidisha zaidi wanaabudu mashetani, wanawaamini Waganga na Mizimu na mambo yote ya Shirk ndio yalokumbatiwa, Shetani kayapamba mambo yetu mpaka sasa hakuna hata anayeogopa Akhera mpaka asikie fulani kafariki ndio kidogo anashituka, Shetani ndio anapamba (Ma-Stage)yetu ya mambo machafu, hayo ndio tunayapa umuhimu, jitizame wewe unavotoka mbio ukisikia mduara au pana chakacha, jiangalie nafsi yako inakua vipi ukiambiwa kuna harusi nini inakua hali yako, au usikie kuna Mpira tena (Live)na ikisha rejea nafsi yako mtu akikupa taarifa kuna (Mawaidha)unamtizama usoni unamwambia nifunike kama yule (Kasuku). Nani katawala maisha yako Shetani au Mollah wako, siri hiyo utaijua mwenyewe kama unapoteza siku nzima kwenye TV au katika Darsa, kama kwenye Sala au Nyumba ya Muziki, utatambua mwenyewe dakika ngapi unamkumbuka Mollah wako na masaa mangapi unamkumbuka Mwalimu wako (Kasuku)kama vile nyimbo za Tarab, hayo ndio aloyaona Hud Hud, kwamba Shetani kakupambia mambo ya kidunia anakuzuilia kuujua Ulimwengu na Walimwengu, kakufunga pahala pamoja katika Tundu lako na wala hutaki kufunguliwa ukawa huru, ukaweza kuruka huku na kule, ukaona jipya na la zamani, Kurupuka usingizini ili upate kujifunza katika Ulimwengu huu mambo yapo mengi ya kujifunza na kusoma, na wala usidhani utayamaliza kwani kila siku utakua unasoma mambo mepya, labda ubakie kuwa mwanafunzi wa Kasuku ili ubakie kufunikwa Milele.
Namuomba Mollah atulinde na Ukasuku, tusije kudanganywa na Shetani, atupe uweza wa kugundua kama alivogundua Ndege Hud Hud. Amin

Sunday, April 14, 2013
UKOMBOZI WA NAFSI PART 1
Asalaam Aleiykum,
Nini Mapinduzi? Mapinduzi ni kitu chochote kilogeuzwa, kinaweza kuwa kiti au meza, yaweza kuwa sufuria au Nchi, lakini kuwa na hakika chochote kile chenye kupinduliwa hakitokaa sawa mpaka kirejeshwe katika hali yake ya mwanzo au kama kilivokua, kinyume na hilo hakuna mategemeo ya kukaa sawa daima, na mifano iko mingi ya nchi na mengineyo wenyewe mtachunguza.
Nini Ukombozi?
Ukombozi ni tendo la kutolewa katika hali ya ulazimishwaji, iwe kulazimishwa huko kwa udanganyifu au mbinu ya hila za nguvu, au hadaa ya hiyari ilokupelekea mpaka ukakubali kutawaliwa na jambo husika lenye madhara na wewe, kama vile kutekwa nyara na ukawa huna uwezo wa kujikomboa. Mimi nina uhakika yakwamba kila mmoja wetu ni mahabusu(Mfungwa)wa ima Shetani au Mwanaadamu mwenzio, lazima katika wawili hao mmoja kakuteka nyara, Ikiwa sio mahabusu wa Shetani basi itakua Mwanaadamu mwenzio kakumiliki katika sehemu zote au chache zilobakia, kwa ajili hiyo sasa imekujia darsa hii ya Ukombozi ili upate kuokolewa katika hicho kifungo chako cha khiyari, ili utoke katika (Jela)hii inatakikana mbinu imara za kuifungua minyororo ilo kuzunguka kwenye kila kiungo chako.
Sasa kwanini unatakikana Ukombozi huu wa Nafsi? Sababu kubwa kabisa ya kwanza inayo kufanya uhitaji ukombozi huu ni ile ilokufanya Umsahau Mollah wako, Ambaye kwa Mapenzi yake yasopimika kakupa uhai huu unaoufanyia mzaha kwa wakati huu, Na ukiitizama Nafsi yako imetawaliwa na Maonesho matupu, katika maisha yako imekua kila kitu chako ni lazima kiwe cha shirika, sasa virejee vitendo ntakavo vitaja hapa halafu kwa ukweli wa nafsi yako jiulize mimi ninazo tabia hizi au ni porojo tu.
Umeingia wewe katika (Showing off)hii kuanzia kwenye nguo mpaka chakula, mpaka mazungumzo yako ukijisikiliza utajua nimekusudia nini, Imefunikwa Nafsi yako kiasi ambacho huwezi hata kukumbuka kujiridhisha wewe Mwenyewe au Mollah wako.
Ukisali kwa ajili ya watu, ukitoa Sadaka kwa ajili ya watu wajue unatoa, ukimsaidia mtu kama hutaki kulipwa lakini unailazimisha Nafsi ya huyo ulomsaidia akunyenyekee au akukumbuke daima kwamba ulimsaidia, ukijenga Nyumba kwa ajili ya watu, ukinunua gari lazima watu watambue, imezungukwa Nafsi yako na (Khofu) ya watu mpaka inakua kutwa nzima maisha yako ni kuridhisha watu, na watu ndio watu, kama hujawaridhisha wanageuka kuwa mahasimu zako, hapo unakuanza ugonjwa wa wasiwasi,(Unasema Kichwani kwako kutwa) sijui kaniona, ama kafanya kusudi, Mbona anatenda dhambi, yule anakwenda motoni umejitahidi mpaka umechukua cheti cha Uhakimu sasa, umejibebesha mzigo wa mateso ambayo yanaweza kuepukika kirahisi kabisa na tena bila ya ugumu wowote.
Kwa hali hiyo wewe sasa unahitaji Ukombozi ambao utakutana nao Part 2

UKOMBOZI WA NAFSI PART 2
Asalaam Aleiykum,
Umefika wakati unahitaji ukombozi wa nafsi yako ili yasije Mauti yakakukuta katika hali hiyo, ili upate kuokolewa kutoka katika makucha ya Shetani na Wanaadamu wenzio, nini cha kufanya ili uokoke, lakini huwezi kujiokoa kama hujui matatizo yako, wacha tuzidi kupata mfano ili iwe fundisho kwetu na kwa wengine, itizame Nafsi yako ilivofunikwa na wimbi la maonesho, Jitizame kama wewe Imam vipi inakua hali yako katika kusalisha, unaanza na Sala nia yako ipo kwenye sauti sijui nzuri, inapendeza, nimetia shada, pale nimevuta, sijui mguu nimeweka sawa, ukiwa katika kufunikwa na hali kama hiyo jua hiyo si Sala, kwenye Sala, yule anosali anapotea kabisa na anabakia Mwenye-enzi-Mungu, ukijiona unachunguza Sala za wenzio mguu umekaa vipi, na hivi na vile basi jijue unahitaji ukombolewe kwani Nafsi yako haitaki kujitupa kwa ukamilifu kwa Mollah wako.
Itizame Nafsi yako ilivozama kwenye maonesho ukiwa na Elimu basi lazima matabu yajae nyumbani kwako, watu watajuaje,Umezidi maonesho mpaka ukinunua soksi lazima watu wajue, ukinunua saa au nguo mpya na ikawa watu hawajatambua basi unaweza kuumwa kwanini watu hawajajua, sijui mbaya au wamenidharau, ukihifadhi aya tatu kwenye Quraan mji mzima unataka uelewe wewe shekhe, ukihifadhi hadith mbili tatu unataka uonekane umeshika dini, na ukija kutafakari zaidi utaona unajitangaza mpaka kwenye maasi, jana nilifanya jinsi kadhaa wa kadhaa, hata ukija zinduka wapi Ibilis kakuzunguka kila pembe hutoki tena na huku watu wanazidi kukupigia makofi endelea tutakua pamoja (Motoni). Ukiangalia Mwanaadamu wewe hufanyi chochote kwa ajili ya Mollah wako, kumbuka kipi unachofanya kwa ajili ya yule Alokuumba, kawaida yako imekua hivi mazuri yote unayatangaza, na yale mabaya yote unamkusanyia Mwenye-enzi-Mungu na huku ukisema nisitiri wasijue, nivue usiniadhibu, nilinde nisiadhirike, naomba nisidhurike. hiyo ndio Nafsi yako ilivyo mpaka wakati huu, hayo ndio machache niliyo yataja, lakini kuna mengi ambayo Nafsi inayajua.
Sasa ufanyeje ili ujifungue katika hicho kifungo cha nje, hakuna jengine ila kurejea katika Nafsi yako uanze kufuta mavumbi ili upate kuwa safi, ungare.
Muulize Mollah wako anasemaje katika kadhia hii ya Ukombozi, ufanye nini ili uwe safi na kujiepusha kabisa na maonesho hayo ambayo umeishi nayo miaka yote mpaka kufikia hivi sasa. Anasema Mollah wako usi ishi Maisha ya kujionesha,kwani ukifanya hivyo utashughulika zaidi na wanaadamu wenzio na kumsahau moja kwa moja yeye Muumba, Ila umepewa Ruhusa ya (Kuhadithia)kumbuka kujionesha na kuhadithia ni vitu viwili tafauti, na Ruhusa yenyewe imo katika sura ya Dhuha aya ya 11
"وَأَمَّا بِنِعۡمَةِ رَبِّكَ فَحَدِّثۡ"
"Na Neema ya Mollah wako Ihadithie"
Vipi Utahadithia Neema za Mollah wako zipo nyingi sana, basi ziseme japo hizo chache, Nilikua nimepotea Mollah wangu kaniongoza, nilikua si Sali sasa na Sali, Nilikua simkumbuki haijambo nimeanza kidogo kidogo kumkumbuka, Nilikua nalewa sasa nimeacha, nilikua nazini lakini sifanyi tena, nilikua nikisema watu nimeacha,mambo yote ya haram najiepusha nayo. Akanikuta Mollah wangu maskini lakini nashukuru sasa kidogo mambo mazuri, riziki yangu sasa napata kwa wepesi, hivi sasa najiweza japokua Mollah wangu hajanipa utajiri lakini pia siombi, na mtu akija kuniomba simfukuzi nafanya bidii kuhakikisha naitatua shida yake,Nilikua mgonjwa sasa sijambo na kwa ajili hiyo naona Nafsi yangu nyepesi kwa hivi sasa, na mimi nimejifunga kuyaelekeza maisha yangu kwa ajili ya Mollah wangu pekee.Endelea part 3

UKOMBOZI WA NAFSI PART 3
Asalaam Aleiykum,
Sasa ikiwa unataka ukate hiyo minyororo shuruti lake ubadilike, na kubadilika kwenyewe uchague kipi cha mwanzo utakibadilisha, wewe una vitu vingi, mimi leo nakuchagulia cha mwanzo kilicho katika ukumbi wa maonesho nacho ni huo mwendo wako na mtazamo wako, kwanini vikatajwa hivyo, kwa sababu hizo ni alama za kiburi, na alama hizo zinatokea ndani kwenye Nafsi yako, na ukibadilika nje na ndani haiwezi kukaa desturi hiyo tena, angalia Luqman aya ya 18.
" وَلَا تُصَعِّرۡ خَدَّكَ لِلنَّاسِ وَلَا تَمۡشِ فِى ٱلۡأَرۡضِ مَرَحًاۖ إِنَّ ٱللَّهَ لَا يُحِبُّ كُلَّ مُخۡتَالٍ۬ فَخُورٍ۬"
"Wala usiwatizame watu kwa upande moja wa uso, wala usende katika nchi (Ardhi)kwa maringo, hakika Mwenye-enzi-Mungu hampendi kila ajivunae, anojifaharisha"
Usipite ukayatangaza maisha yako, utakua umo khasarani, utafukuzwa kwenye ufalme wa Mwenye-enzi-Mungu, itakua umejishughulisha na wanaadamu wenzio na umemsahau Mollah wako, sasa ufanye nini? Mollah wako anataka ubadilike uwe katika waja wake alowataja katika sura ya Furqan aya ya 63,
"وَعِبَادُ ٱلرَّحۡمَـٰنِ ٱلَّذِينَ يَمۡشُونَ عَلَى ٱلۡأَرۡضِ هَوۡنً۬ا وَإِذَا خَاطَبَهُمُ ٱلۡجَـٰهِلُونَ قَالُواْ سَلَـٰمً۬ا"
Na (hao)waja wa Mwenye-enzi-Mungu ni wale wanaokwenda (Ardhini)Ulimwenguni kwa unyenyekevu, Na wajinga(wakikutana nao)wakisema nao (kwa ubaya)huwajibu(kwa)salama. kukoje huko kwenda kwa unyenyekevu, ni mwendo wa taratibu, kuwa na tahadhari yakwamba katika ardhi hii Mollah wangu kaumba viumbe wengine sina haja mie ya kuviangamiza, nikikutana na wenzangu na nyenyekea kwa heshima na huku namsalimia kila mtu, awe mbaya au mzuri wote nawaamkia kwa maamkizi ya amani ya Mwenye-enzi-Mungu iwe juu yao.ukisha kuyaweza hayo mawili ya mwanzo sasa ushaanza kuupata huo Ukombozi ulokusudiwa, ushaanza kubadilika, na ukibadilika tu unatakiwa uanze kwa haraka kujipendekeza kwa Mollah wako kama isemavyo aya katika sura ya Alam nashirah aya ya 8 "وَإِلَىٰ رَبِّكَ فَٱرۡغَب" Na kwa Mollah wako jipendekeze"
Vipi utajipendekeza kwa Mollah wako na wewe humjui, umeshapewa madawa yote ya kukutibu ili umjue Mollah wako lakini dawa hazifai, umejaribiwa kwa Habat-muluki, umenyeshwa shubiri dohani lakini zote hazijafanya kazi, basi wacha nikupe dawa hii labda itakusaidia katika huko kujipendekeza, ikiwa ushagundua umepata ukombozi sasa anza kufanya tendo hili ambalo kama utalifanya kwa uhakika na kudumisha hali hiyo basi utajikuta ghafla umetokezea na unaishi katika kundi la Mawalii, Ufanye nini kuwa mwenye kutia udhu masaa 24, kaa na udhu kila wakati,mpaka ukitaka kulala tia udhu, nini kitatokea baada ya mwezi mmoja au miwili ukiweza kukaa na udhu bila ya kuvunja ada hiyo, huku unakumbuka wakati wote mimi nina udhu, utahama katika udhu na utakua unamkumbuka Mollah wako, na ukipata kumkumbuka Mollah wako kama ulivo ukumbuka udhu hapo unakua ushafanikiwa na hali hiyo ya kukumbuka haiondoki tena mpaka uhai wako unamalizika katika Ulimwengu huu, na huko uendako unakua katika walofuzu, na kumbuka Mollah wako akiwa katika fikra zako kila wakati hutendi tena dhambi, na hata ukitaka kutenda basi hufanikiwi. Namuomba Mollah wangu atukomboe tutoke katika maisha ya ufakhari na kujionesha, atukirim mwenendo wa kumkumbuka yeye mpaka mwisho wa Umri wetu. Amin.

Sunday, April 7, 2013
SIRI YA UZURI PART 1
Asalaam Aleiykum,
Leo hapa nataka uonje na mimi japo kidogo chakula cha elimu ya Uzuri, ndani ya chakula hichi upate kujua ladha na maana ya neno hili la uzuri,(Mpaka leo wanahangaika wanasayansi)kujua nini uzuri lakini wameshindwa kuitambua siri hii, na usidhani na sisi ndio tumeigundua laa, tunajaribu kupata chakula hichi cha miujiza ili kwa uchache kitukate njaa yetu yakujua nini uzuri. Sasa utajiuliza kwanini nimeliunganisha neno la uzuri na chakula, sababu kubwa ya kutumia neno hili ni kwa kuwa na wewe unalitumia kila mara katika hicho chakula, unalitumia katika kuwahukumu wanaadamu nani mzuri na nani mbaya, lakini cha ajabu hujui maana yake na wapi huo uzuri unatokea, na kwanini ukatokea, na inakuaje unapotokea, na ikiwa unajua basi wewe ni katika wachache walopewa bahati hiyo ya kuelewa, lakini kwa wale wasojua basi hii ndio Darsa yao ya kupata faida mbili tatu ya siri ya uzuri.
NINI UZURI?
Uzuri una desturi ya kuficha tafsiri yake kama ilivyo Afya na Furaha, ukiulizwa nini Afya unakua huna jawabu, lakini waweza kujibu nini Maradhi ukayaeleza haya ya Sukari, haya ya Figo, haya ya tumbo nk. Na furaha vilevile unaweza kutaja sababu ya Furaha lakini ukashindwa kueleza furaha yenyewe ni nini, na Uzuri hali kadhalika huwezi kuuchambua ila unajua tu hichi kizuri, huyu mzuri , kwa uchache vyote hivyo ni vitendo vya kuhisi(Experience) lazima uishi ndani yake ndio ujue sasa umo katika hali hiyo. Anaweza kusema Mtu kwanini asitaje kuona, Naam kuona unaona kila siku lakini jee unaona mazuri, ndio nikakwambia darsa hii nataka nikufahamishe vipi utizame vizuri au (Uzuri)wa kila kitu ili upate faida.
Tumepewa Fadhila kubwa na Mollah wetu katika neema hii ya (Kuona) nini kinatokea katika kuona(Elewa nazungumza haya kupitia elimu ya dini na sio ya sayansi)Nini kinatokea mpaka tunaona, Unapotizama kitu kwa kutumia macho unakua unatoa (Energy) au nguvu fulani kwenda nje kwenye hicho kitu, na hicho kitu kinatoa (Energy)inayokuja kwako kwenda ndani ya akili na kufanyiwa uchambuzi ili kipatikane kujulikana ni kitu gani, na kikisha julikana inapatikana hiyo yenye kuitwa (Knowledge) au (Known) kwa ufupi. Kwa maana hiyo kila kitu katika Ulimwengu huu ni (Matter) na hiyo (Matter) ni (Energy) na hiyo (Energy)tuwaachie wana (Physics)watatuchambulia zaidi.
Leo katika Darsa hii nitagusa (Lip-stick) Rangi ya mdomo, (Eye-Shadow) nitapita katika utowaji wa nyusi na mengineyo lakini kabla ya kwenda huko wacha nikutembezeni kwenye hii Bustani ya (Known)kujua ili mchume matunda ya fahamu ili mkitoka katika bustani hii na nyie muwe katika kundi la wenye kuelewa. Ndani ya bustani hii tunakutana na kitabu cha wageni, kitabu kikarim Quraan sura ya Mulk aya ya tatu mpaka ya tano. Endelea part 2

SIRI YA UZURI PART 2
Asalaam Aleiykum,
"ٱلَّذِى خَلَقَ سَبۡعَ سَمَـٰوَٲتٍ۬ طِبَاقً۬اۖ مَّا تَرَىٰ فِى خَلۡقِ ٱلرَّحۡمَـٰنِ مِن تَفَـٰوُتٍ۬ۖ فَٱرۡجِعِ ٱلۡبَصَرَ هَلۡ تَرَىٰ مِن فُطُورٍ۬ ٣) ثُمَّ ٱرۡجِعِ ٱلۡبَصَرَ كَرَّتَيۡنِ يَنقَلِبۡ إِلَيۡكَ ٱلۡبَصَرُ خَاسِئً۬ا وَهُوَ حَسِيرٌ۬ (٤) وَلَقَدۡ زَيَّنَّا ٱلسَّمَآءَ ٱلدُّنۡيَا بِمَصَـٰبِيحَ وَجَعَلۡنَـٰهَا رُجُومً۬ا لِّلشَّيَـٰطِينِۖ وَأَعۡتَدۡنَا لَهُمۡ عَذَابَ ٱلسَّعِيرِ "
"Ambaye ameumba mbingu saba zenye Tabaka,(Moja baada ya nyengine)huoni tafauti katika uumbaji wa mwingi wa Rehma, ikisha rejesha macho, je unaona kosa(Lolote)(3).
ikisha rejesha tena macho (yako)mara nyingi zaidi, litarudi jicho lako hali yakua limehizika na kuwa chovu (Kuchoka)(4) Na hakika tumeipamba mbingu ( hii ya)Dunia kwa mataa, na tumeyafanya(Majinga ya Moto)kuwapigia mashetani, na tumewaekea adhabu ya moto uwakao (kwa nguvu)"
Naam hiyo ndio hali ya huko juu na hapa chini huwezi kuona tafauti, hakuna makosa katika uumbaji wa Mwenye-enzi-Mungu huwezi kukuta chochote chenye kukosewa ndio maana ukatakiwa angalia sana, rejea kuangalia mara nyingi, na kweli ukiangalia sana mbingu jaribu nusu saa tu uitizame mbingu basi utaona macho yamejaa lepe lepe la usingizi(jaribu utaona)jicho linavo choka. Aya ikaendelea kusema tukaipamba mbingu kwa mataa, kumbuka Mwenye-enzi-Mungu anatwambia tazameni mapambo ya mbingu, yaonesha binaadamu tunaishi katika Ulimwengu huu hatuyaoni mambo mazuri yalotuzunguka, na vipi wewe utaona uzuri wa Mbingu ikiwa Mkeo huwezi kumuangalia Uzuri wake, ikiwa huoni cha karibu vipi utakiona cha mbali na kama unabisha hayo kama wewe huoni mazuri wacha tuangalie mfano huu, halafu utajua wewe unayaona mazuri au uzuri wa Ulimwengu huu au kinyume chake huoni kabisa.
Mambo mazuri katika Ulimwengu huu yapo mengi na yametuzunguka lakini masikini tumekua vipofu hatuoni chochote, katika ulimwengu huu mpaka ndege wana rangi nzuri, nyota zina uzuri wake, kipepeo ana uzuri wake, njiwa ana uzuri wake, tausi kapambwa kivyake,maua yana uzuri wake kila jambo lina uzuri wake tumezungukwa na mambo mazuri, tunaishi katika ulimwengu mzuri, kila kilichomo kizuri, mpaka maisha yako mazuri, wewe mwenyewe mzuri, lakini matatizo yetu wanaadamu hatuyaoni kabisa mazuri haya, na siyo hatuyaoni bali hata kuyajua hatuyajui kabisa, na mfano kama kilivyo kichwa, bila ya kichwa kuumwa unajua kama una kichwa si mpaka kiume, hiyo ndio hali ya uzuri ilivyo tunaishi ndani ya Uzuri lakini maskini Roho zetu zina ukungu hatuoni uzuri wowote uliomo katika Ulimwengu huu, Na kama unakaidi hilo jiulize wewe mwenyewe kwa siku unayaona mazuri mangapi, hebu kumbuka japo leo mazuri mangapi umepishana nayo na hujayagundua.
Vipi wewe utayagundua mazuri wakati huwezi hata kumgundua mke kavaa(Dish Dasha)la Rangi gani, Jitizame sasa hali yako ukirejea nyumbani unakuwaje, ukifunguliwa mlango swali lako la mwanzo unauliza hamjalala, alaa anolala anafungua mlango, unakuta nyumba ina harufu nzuri za udi unauliza mbona kunanukia, sasa wacha uwekewe chakula uone vipi umelala, hupo kabisa, hata mkeo humtizami usoni, eti wewe ndio unaona haya, una jambo gani wewe hata huoni uzuri wa mkeo, sasa ngoja uwekewe chakula uone nini kinatokea, pengine kuna Biriani na ndizi mbivu, au zimewekwa katlesi na venginevyo, basi unaweza kuishika Biriani (Wallahi)huku unafikiri kisambu cha hawara, unakamata katlesi unafikiri sijui yule kimada kawatia wale samaki kwenye friji, au utafikiri mpira au mambo ya barazani mpaka mkeo akuonee huruma tena anakuamsha chunvi iko sawa ndio unakuruka usingizini, sawa, unashindwa hata kusema chakula kitamu, vipi leo utaona mazuri, utajuaje nini kizuri, wakati kizuri kiko mbele yako hukioni anakwambia Mollah wako katika sura ya Tin aya ya nne.
" لَقَدۡ خَلَقۡنَا ٱلۡإِنسَـٰنَ فِىٓ أَحۡسَنِ تَقۡوِيمٍ۬" Tumemuumba mwanaadamu kwa umbo lilo bora kabisa" vipi leo huwezi kugundua uzuri uliopo katika mambo yote yalokuzunguka, na kwanini hutaki kujua sababu za kutokuona kwako, lazima kuna pahala unafanya makosa fulani ndio maana umenyimwa neema hii ya kuona mazuri katika Ulimwengu huu. Sasa kama nilivyo ahidi nitarejea kwa dada zetu ikisha nijulishe wapi uzuri unatokea na ufanye nini ili upate kuona vizuri. Endelea part 3

SIRI YA UZURI PART 3
Asalaam Aleiykum,
Sasa wacha niwaguse dada zangu na hii shughuli ya kioo na udanganyifu wake, hakuna kioo chochote utacho jitizama kikakwambia wewe mzuri, uzuri hautokei kwenye kioo, kioo ni chenye kukutengeneza tu, sifa zote za uzuri unategemea wanaadamu wenzio wakujulishe au wakusifu wengine wakutamani hapo ndipo unapata kufurahi Roho yako yakuwa kumbe mimi mzuri, kutokana na hali hiyo unahitaji visaidizi kwa sababu wale walo kutizama hawakuona uzuri, wao wenyewe hawaujui uzuri, nini wameona, wameona mapambo ya kuvutia kama vile (Lip-stick) kuchongwa kwa nyusi, vipini vya pua na mapambo mengine ndio maana mkaambiwa (Haram)kuonesha vivutio hivyo, sasa kwanini unafanya hivyo, unafanya hivyo kwa sababu hujaridhika, japokua aya ishakwambia hakuna makosa katika uumbaji wa Mollah wako lakini huridhiki, labda unaona hawataki nijipambe, na bila ya kujipamba siwi mzuri, wakati ukipishana na kiumbe huyo Sokoni na (Natural)yake alomuumbia Mollah wake utaona anameremeta kwa uzuri utokao kwa Mollah wake, kapendeza hana chochote katika sura yake lakini wacha itangazwe harusi ukakutane na mtu huyo huyo, unaweza kukimbia, pengine utamkuta baada ya kupendeza anatisha kwa (Foundation) na podari debe zima, anadhani uzuri unatokezea hapo, kumbe anajiharibu anauficha na kuharibu uzuri wake, na kama mtu atabisha haya ajaribu kwenda harusini (Simple)aweke vitu vyake lakini kwa njia ya (Moderation) na ataona tafauti ikoje na wenzie walopaka poda mwiko mzima na kufanya shughuli za kuuziba uzuri wao, kwanini ujibadilishe siku hii ya harusi wakati siku zote wewe mzuri.
Sasa Uzuri unatokea wapi kwa mwanaadamu?
utizame kwa makini uzuri unapotokea, fanya bidii upajue hapo,
Kwa hilo itabidi tuhudhurie Quraan sura ya Yussuf aya ya 22
"وَلَمَّا بَلَغَ أَشُدَّهُ ۥۤ ءَاتَيۡنَـٰهُ حُكۡمً۬ا وَعِلۡمً۬اۚ وَكَذَٲلِكَ نَجۡزِى ٱلۡمُحۡسِنِينَ "
"Na(Nabii Yusuf)alipo baleghe tulimpa Hikima na elimu, na kama hivi (ndivo)tunawalipa wanaotenda mema"
Hapa aya inatukumbusha kitu muhimu sana, inatuonesha tafauti ya vitu viwili hivi, (Inteligence)na(Education) Unaweza kumkuta mtu ana Degree au Phd lakini maskini kakosa (Inteligence)hekima, hata mazungumzo yake haya maana, kwanini ikawa hivyo kwa sababu yeye ana kipande cha karatasi cha kumjulisha kenda University lakini katika maisha yake anaishi kama mnyama, hana uzuri wowote wa maisha hajui chochote kizuri katika nafsi yake wala ya binaadamu wenzake hana hekima, lakini (Inteligence)hekima ni kitu chengine kabisa na utaona mfano wake kwa watoto maswali wanayouliza kutaka kujua maana ya kitu, watoto wanauliza kutumia (Inteligence) na sisi tunawajibu kutumia (Education) na kwa sababu hatutumii hekima katika majibu yetu, tuna haribu kabisa hekima ya watoto, sasa kwanini nikasema hayo, sababu kubwa watizame watoto utapata tabu sana kumuona mtoto mbaya(Ugly Baby)watoto wote wanazaliwa wazuri(Beautiful)na hekima zao(Hawana dhambi ni wasafi), sasa ngojea wewe wafike umri wa miaka kumi na nne uone sasa ufisadi gani unaingia kuharibu mwenendo, tabia na hekima zote zilizo nzuri, utamkuta mtoto wa kike keshafundishwa kupakwa chokaa, kesha tobolewa pua, tayari anajua kunyoa nyusi, inakua fujo tupu na yule wakiume naye keshaona mapambo hajiwezi tena wanakwenda waja hawa hata wakifikia miaka 30 uzuri wote ushapotea, nuru imezimika kabisa(ndio unasikia mtu anakuuliza unaweza kukisia mie miaka mingapi).
"Sasa tumrejee Nabii Yusuf a.s" Alipofika Baleghe alipewa vyote viwili Hekima na Elimu, hekima kuulinda uzuri wake, kujua mabaya na kujiepusha nayo, kujiweka katika hali ya Tohara(Pure)Nafsi yake isigubikwe na ufisadi wowote ule na hii ndio siri ya uzuri kaa makini uifahamu vizuri(Kama Nafsi itajiepusha na kila mabaya, itakua haina mambo ya kipuuzi imejitupa kwa Mollah wake)basi inatokea kwa hakika (Glowing:To shine brightly and steadily, especially
without a flame)Unangara nafsi yako ina meremeta(Pure Being)kila kiungo chako kizuri, watu wanakushangaa ndio maana katika Aya ya 31 ya sura hiyo hiyo ikasema,
"فَلَمَّا سَمِعَتۡ بِمَكۡرِهِنَّ أَرۡسَلَتۡ إِلَيۡہِنَّ وَأَعۡتَدَتۡ لَهُنَّ مُتَّكَـًٔ۬ا وَءَاتَتۡ كُلَّ وَٲحِدَةٍ۬ مِّنۡہُنَّ سِكِّينً۬ا وَقَالَتِ ٱخۡرُجۡ عَلَيۡہِنَّۖ فَلَمَّا رَأَيۡنَهُ ۥۤ أَكۡبَرۡنَهُ ۥ وَقَطَّعۡنَ أَيۡدِيَہُنَّ وَقُلۡنَ حَـٰشَ لِلَّهِ مَا هَـٰذَا بَشَرًا إِنۡ هَـٰذَآ إِلَّا مَلَكٌ۬ كَرِيمٌ۬ "
"Basi (yule mke)aliposikia msemo wao aliwaita(Waje kumuona Yusuf a.s kwa uzuri wake)na akawafanyia karamu na akampa kila mmoja katika wao kisu na akamwambia (Yusuf a.s)Tokeza mbele yao, basi walipomuona waliona ni kitu kikubwa kabisa na wakakata mikono yao(Kwa visu)na wakasema "hassha lillahi" huyu si mwanaadamu, hakuwa huyu ila ni Malaika Mtukufu"
Hapo utaona kimetokezea kitu kwa ghafla kinameremeta, nuru inawaka, hao wanawake hawamjui Malaika, lakini kwa kuwa kitu kilotokezea kimewashangaza wakadhani labda Malaika, hakujipamba Nabii Yusuf a.s, hakuvaa chochote chenye mvutio, katokeza na nafsi yake tu yenye kungara na wote walokuwepo wakajikata vidole(hata wewe jua likikupiga ghafla machoni wakati unaendesha gari si unapata ajali)huo ndio uzuri unatokezea katika roho yako, sio kwenye mwili wala kwenye mapambo, safisha roho yako, ifanyie tohara daima utakua mzuri mpaka kufa kwako.
"Na hiyo elimu aliyopewa Nabii Yusuf a.s" ndio hiyo ya kujua mambo ya ndoto nk.
"Sasa nini kuhusu wewe" Nafsi ishazimika kwa mambo yalojaa Rohoni (Switch)haionekani tena na wewe bado unataka kuonekana mzuri, hakuna la kufanya ili uwache kujipamba, zidisha Ibada, Muweke Mwenye-enzi-Mungu katika mawazo yako, mkumbuke kila mara, zoea kusoma Quraan sana, baada ya miezi mitatu utaanza kuona dalili za uzuri zinakurejea, taa inaanza kuwaka tena, sasa unaweza kwenda harusini bila ya kujipamba na watu wote wakaanza kukutizama wewe, kwanini ikawa hivyo, kwa sababu utaanza kutoa nuru fulani katika macho yako, na hapo inapotokea hiyo nuru ndipo unapokaa uzuri, na kama unataka kuyajua hayo mtizame yoyote unayedhani ni mzuri kwako wewe utaona mtazamo wako wote unaishia kwenye macho, na hayo macho ni dirisha la uzuri, namalizia kwa kusema uzuri unakaa ndani sio nje kama mnavodhani ndio maana wazungu wakasema(The Beauty is in the eyes of the Beholder)Nakuomba Mollah wangu utupe fahamu hii ya uzuri, tufahamu uzuri wa vitendo vyetu, uzuri wa Nafsi zetu, na mwisho Uzuri wa huu Uhai wetu ulo Tukirim katika hizi Roho zetu.
Amin.

Monday, April 1, 2013
MAKOSA YA MJA MWENYE SHIDA-PART-1
Asalaam Aleiykum,
Kwa wale wanodhani mimi ni mtowaji mawaidha nawaomba wabadilishe dhana zao, na ukisoma Darsa zangu ukadhani ni mawaidha utakua mwenye kukosa faida na mafundisho yaliyomo katika darsa hizi. Mawaidha wajibu wake ni kitu cha kusikiliza, na kusikiliza kuna hiyari ama utasikia maneno au sauti, ukisikia maneno kidogo yatakushitua, yatakugusa japo kwa mbali, lakini ukisikia sauti ndio itakua mtoa mawaidha kasema kitu chengine na wewe unakuja na tafsiri ya kitu chengine kabisa. Sasa nini kazi yangu mimi katika darsa hizi, Nia yangu ni kukupa nyenzo ya kuweza kukubadilisha na ukifahamu darsa hizi unakua mtu mwengine kabisa, Uislam wako na ufatiliaji wako wa mambo ya kidini unabadilika na kuwa wa vitendo sio wa maneno.
Basi leo pata faida ya Mja mwenye shida yaweza kuwa wewe au nikawa mie, Sote tuna shida na kwa vyovyote sote ni wenye kuhitaji, sasa nini kinacho tusib mpaka tukawa tunaingia matesoni, kipi kinacho tujulisha sasa tumeshazama matesoni, cha mwanzo kabisa kuondoka ni hiyo Imani ya uchache iliyomo kwenye mioyo yetu kupotea, na Imani ikipotea unakua umekitupa kitu kikubwa sana chenye thamani na wewe. Ndio maana utaona hata kitendo cha Sala zetu zimejaa maombi matupu, japokua hiyo Sala ni maombi lakini kusudio lake sio kila ukenda kwa Mollah wako unasahau hata kumuabudu ila wewe mwenye kuomba cheo, au utajiri, labda mwanao apasi mtihani au jirani afilisike, hiyo ndio Sala yetu unaomba hiki unataka kile umesahau hata dhumuni la hiyo sala na umekwenda kwa Mollah wako kwa ajili ya kitu gani, unajisahau kabisa inakua unamaliza sala nzima imejaa pesa au fulani adhurike, na kama unakaidi haya wewe yachunguze maombi yako na utagundua kama haya nisemayo ni kweli, na ukishagundua kama haya nisemayo ni kweli basi piga kelele unusuriwe sababu umo hasarani.
Angalia vipi mtu anakua akiambiwa Sali sala za usiku utafanikiwa anakuaje, Unaweza wewe ulomwambia ukatoka mbio, anaweza Mja huyo akasali miezi sita sababu ya Shida yake itekelezwe, lakini Ole wake iwapo Mwenye-enzi-Mungu hajampa matakwa yake, subiri utizame manyago yatotendeka hapo, nini kinatokezea kama hakufanikiwa, machafuko gani Mja huyu anayafanya mpaka Malaika wanaogopa, hatari kubwa, anabadilika Mja huyu kwanza anakwenda kwa Masheikh labda wana miujiza au dua walizo zificha, na kama hapo haiwezekani sasa Mja huyu ndio anaanza vitimbi mara kalala na kisu au kafutika ndimu, safari za kwa waganga ndio zinakua nyingi kuliko hata Msikitini, hata akimbiwa anyoe kope za macho zinatolewa mara moja, ajifunge kitanzi alale nacho pia yuko tayari, Maskini Mja anakua kashaingia hasarani na kuendelea kutenda makosa makubwa kwa Mollah wake, hapo hata Usali na Sijida lichune uso unakua Muflis. Wewe ni mwenye kumshirikisha Mollah wako, na Mollah wako hayuko Radhi na wewe na unaendelea kuishi katika shida na wala hazitatuki.
Sasa kwanini yanatokezea haya, kwa sababu kila mmoja wetu jambo la kwanza anahitaji Utajiri, kila mmoja wetu anahitaji kilichozidi, kile alichopewa hakitoshi, kila mtu anapigana Jihad hii mpaka tunakwenda katika Makaburi yetu hakuna mapumziko na hakuna hata mmoja alofanikiwa, na katika kuyatenda hayo yote tunakua tushajidhuru nafsi zetu kwa madhara chungu nzima ya Ufisadi na Husda, Dhuluma na kumkera Mwenye-enzi-Mungu na viumbe wenzetu na huku hatujui kwanini tunateseka. Kinacho tutesa kikubwa cha kwanza ni kusahau au kutokujua Maumbile ya Ulimwengu huu na Maandiko yake au (Sheria), Na cha pili ni kuondokwa na Imani. Hapa itabidi mnipe nafasi nilizungumze moja baada ya jengine ili upate muangaza au uzinduzi wa fahamu ili usiteseke tena, upate kujua sheria ya mambo ya Ulimwengu huu au mpangilio wake. Kwanza kabisa napenda kukumbusha katika Ulimwengu huu hayo matatizo ndio Mtihani wenyewe, kwa kuwa umesahau ndio maana unaanza kupigana na hayo matatizo, napenda uelewe wewe huwezi kuyashinda matatizo, daima matatizo yatakuzidi nguvu na kukushinda, kwanini ikawa hivyo?.
Mwenye-enzi-Mungu anatwambia katika kitabu chake kitukufu maneno yaliyomo kwenye sura ya Baqarah aya ya 155.
"وَلَنَبۡلُوَنَّكُم بِشَىۡءٍ۬ مِّنَ ٱلۡخَوۡفِ وَٱلۡجُوعِ وَنَقۡصٍ۬ مِّنَ ٱلۡأَمۡوَٲلِ وَٱلۡأَنفُسِ وَٱلثَّمَرَٲتِۗ وَبَشِّرِ ٱلصَّـٰبِرِينَ "
"Tutakutieni katika misukosuko ya (Maisha nayo) Hofu na Njaa na Upungufu wa Mali na Watu na wa Matunda, (basi) na Wapashe habari njema wanaosubiri". Kutaka kujua vipi unadanganyika mpaka unaishia kutenda makosa ya dhanbi kubwa, na ikisha upate (Method-Trick) au njia ya kufanya ili utokane na mtihani huu Endelea-Part 2

MAKOSA YA MJA MWENYE SHIDA-PART-2
Asalaam Aleiykum,
Sasa ikiwa ushapata uhakika yakuwa Mwenyewe Alokuumba kasha kwambia atakutia katika Mtihani vipi leo unashindwa kuwa makini katika kujibu mtihani huo kwa ridhaa na maridhio ya kukubali, Mwanzo kabisa kwenye aya imetajwa nitakupa matatizo ya (Hofu) Nini hofu? Hofu ni lugha nyengine inayo tafsirika sambamba na Mauti, Ukiwa na hofu ikisha ukaidekeza hiyo hofu, ukaitilia mbolea na maji unakua unaishi kama vile Mfu(Zombie) Unakua huipati Sala, wala Mapenzi, hupati furaha vyote hivyo vinatoweka kwako sababu ya hiyo hofu, inatawaliwa Akili na hofu na kujazwa Maradhi mpaka ina haribika, nini maharibiko ya Akili, maharibiko ya Akili ni kutoka kabisa katika njia ya maamrisho ya Mollah wako , ndipo hofu inakuchukua na inakupeleka sasa katika mambo haya,
Unahitaji Mali na umri ndio unakatika, unaanza mapigano ya kuitafuta mali, unataka Nyumba hofu inakufanya utaipata lini, unahitaji mwanamke au mwanamme, ukiwashwa na Tumbo kidogo mbona limewasha, ukitizamwa kidogo tu kwanini kanitizama kakusudia nini kunitizama vile, itakuaje akijua, mbona kifua hakiponi, Shetani kasema nitadhurika, daktari kanipa mwezi mmoja tu wakuishi, watoto sijui wataishi vipi bila ya mimi, mbona hajatusalimia, kapandishwa cheo yeye nimeachwa mie, leo tutakula nini, fulani mbona jeuri na mengi mengineo kwa sasa utakua ushaanza kujijua kumbe loo na mimi ninayo Hofu. Ndio maana aya Mwanzo ikaanza na Hofu, na ukiichunguza kwa makini hiyo hofu yenyewe si kitu chenye Uhai kabisa, ni wewe mwenyewe ndie mwenye kukiunda ukakipa Uhai, ndio maana nikasema hofu ni ndugu wa Mauti. Na ukianza kuifufua nayo inafufuka na kuanza kuishi, na hapo unaanza kuonja upungufu wa kweli kweli katika nafsi yako.
Na Nafsi ikianza kuwa na upungufu ndipo maradhi yote yanazaliwa kwa sababu usharuhusu hofu iishi ndani ya mwili wako,Pia napenda ukumbuke Hofu ni chanzo cha yote yanofatia, Na maradhi yakiingia unaanza kupigana nayo na hapo ndipo zinaanza (Ngumi) za Njaa,(Neno la pili aya limeitaja njaa)Hapa linatajwa hilo litakalo tupeleka wengi Motoni, hichi chakula ndio fitna kubwa ya mwanaadamu, kwanini ikawa hivyo, Chakula ni Jumba la Roho, chakula ndicho kinacho kufanya uwepo Duniani kwa njia ya kuonekana, na kama utakikosa kwa muda wa miezi mitatu tu huna uhai(Utakufa)huwezi kuishi, hichi chakula ndicho chenye kusababisha Maafa yote, Mtu atadanganya, atakopa, ataiba, atadhulumu, atapokea Rushwa lazima tonge iende kinywani, na kila ukitenda matendo hayo yote elewa umefeli Mtihani na marejeo yako ni sehemu (Mbaya huko Akhera) Imekua jambo la hatari kubwa katika kuitatua dhiki ya njaa, sababu kila mmoja wetu anataka aokoke na balaa hili ili mauti yasimkute, na kama nani anopenda mauti yamkute, na hilo jambo la njaa ndilo linatupelekea kumsahau Mollah wetu kabisa, njaa ndio inayotufanya mtu hataki mambo ya dini, njaa inaturudisha katika kundi la wanyama kikamilifu japokua sisi tumepewa fahamu ya kuondoka katika hali hiyo. Tafauti yako na mnyama ni hivi, Mnyama anaruzukiwa hana fahamu, wakati wewe unaruzukiwa ukiwa na fahamu kamili, na umepewa ulimi wenye kuhisi au (Test) ya ladha zipatazo laki tatu, lakini mtizame Farasi au Ngombe ana ladha moja au mbili tu ya majani, hasikitiki , halalamiki karidhika wala hapati shida yoyote, hana haja ya kuweka akiba, lakini jitizame wewe ulopewa fahamu unakuaje, kwanza unataka chakula cha leo, ikisha cha kesho, halafu tena cha Akiba na kile cha ziada cha kuwatesea Binaadamu wenzio wasiokua nacho hicho cha kula. Lakini Mnyama akisha kula huyo anakwenda zake hashughuliki mpaka njaa imshike tena, kama ndege ndio anasowera angani anaimba akimsabahi Mollah wake na furaha tele ya Shukurani.
Jambo la tatu nalo ni hilo la upungufu wa Mali, hakuna yoyote mwenye kukubali kupungukiwa na Mali seuze ukawa huna kabisa, vita vinaanza hapo sasa, mbona natumia tu hazirudi, mbona siku hizi sipati faida, au umejenga jumba la Ghorofa unaona ukuta mmoja hautoshi zungusha na wapili, weka na walinzi tunaweza kudhurika, Mwenye-enzi-Mungu anakutia mtihani mali inapungua taratibu huku wewe moyoni unatetemeka na hapo tena ndio unaingia makosani kwa kumwita Mganga aje kusafisha nyota au aulizwe Jini mbona mambo simazuri kuna nini.
Enedelea Part 3

MAKOSA YA MJA MWENYE SHIDA PART 3
Asalaam Aleiykum,
Na kitu cha Nne ni hichi labda cha kupatwa na Msiba pengine wa mtoto au mume au mke au mtu hashiki uja uzito uone hapo hasira na mayowe na huzuni zinavo tawala, Masikitiko yanakua hayeshi, Uchungu ndio haumaliziki, mtu anaona kaonewa imekuaje au kuna mtu kamfanyia, mbona wengine wanapata yeye kakosa nini, anafikia mtu kuuliza kwanini Mungu kamchukua mwanawe bado mdogo, na wengine wenye kupewa hao watoto, basi wanaletewa mitihani ya kuja kwa watoto hao mpaka huyu Mzee anafikia kusema hee Mollah wangu umenipia nini shetani huyu, jana nilikua polisi leo niko Hospital ananila unga wa Roho Mtoto huyu, na kama huujui unga wa Roho mtizame Mzee mwenye mtoto nunda utaujua.
Halafu linamalizikia la Matunda, sababu wanaadamu ni wenye kupenda matunda, ni wenye kujua Ladha nyingi za Matunda kwa hiyo hili ni kama lile la chakula nalo linakatwa ili mpate kutizamwa mtakua katika hali gani. Inamalizikia aya kwa kutajwa wabashirie wenye kusubiri.
Nini Subira? Soma uzuri hapa na kwa makini kabisa ili upate faida sasa ya kuepukana na huo Mtihani, Jifundishe kupata jawabu la huo Mtihani, Nini Subira?, Subira katika Ulimwengu wa Lugha ina Maana nyingi tu, kama vile si Tayari, haijesha, inakuja labda itatokea na tafsiri nyingi tu ya kutumika neno la subira kwa ufundi wa Lugha, lakini leo nakujulisha katika Ulimwengu wa Pili haitumiki Lugha ila inatumika (Picha) ndio maana ukiota huoti lugha unaota mifano, sasa katika Lugha ya huko Ulimwengu wa Pili Subira ina asili moja na kutizama(Ndio maana hukuti-Mawalii kutumia neno la Sabira na Basira)sababu wamegundua linafanya kazi shughuli moja. Sasa tupate mfano wa neno hilo hapa Ulimwenguni kwetu, Mwanamke akishika mimba mnakua mshagundua kama ni mja mzito, mnajua kuna kiumbe kinakua ndani ya tumbo, halafu baada ya kukua kitazaliwa(sasa tizama kwa lugha unasubiri)lakini kwa matendo unatazama au kuangalia mpaka mtoto atakapozaliwa, huna la kufanya huwezi kulazimsha mtoto akue haraka haraka, unasubiri au kutizama kadara ya Mwenye-enzi-Mungu itimie, na wewe hapo umeridhia, na hiyo ndio Subira, hilo ndio kusudio la subira, unatakiwa uridhie mtihani wa Mollah wako, akikuletea Mtihani wa hofu, wewe utizame(Be Aware)basi hakuwekei sana Mollah wako ila hofu itapotea, (Nisiseme hivi tena ikawa mwizi anavunja ukasema Shk Baja kasema mtizame tu, laa piga kelele) naam ukiwa na njaa usimsahau Mollah wako jua anakujaribu itizame njaa yako, fanya jitihada kwa njia alizokuonesha Mollah wako na yeye atakupa Riziki yako, lakini usishindane na njaa ndipo unaanza kuzua mabalaa chungu nzima, Umekosa Matunda ridhia jana ulipata leo hujapata, una kazi ya utopasi shukuru hivi ndivo alivonipangia Mollah wangu nenda kazini huku umefurahi, ukiwa karani ridhika na kile ulichopewa kwani mitihani yote inaanza na kuto ridhika kwako, umepewa mali au umenyimwa shukuru sema mimi nipo naitizama kudra yako Mollah wangu na wala siyumbi kwani nimeshagundua mambo haya matano yapo kama vilivyo vidole vyangu vya miguuni na mikononi, na kama ninavyo vitizama vidole vyangu na sasa nitayaangalia mambo haya matano hayani shughulishi tena, nini kinatokea ikiwa utasubiri na kupata huo muono wa subira ulokusudiwa, hapo hiyo subira inakurusha katika jambo jengine kabisa unachupa moja kwa moja mpaka katika Aya ya 156 Endelea Part 4
MAKOSA YA MJA MWENYE SHIDA-PART-4
Asalaam Aleiykum,
Unakuja kufungua macho kwa uwazi katika aya ya 156 sura ya Baqarah, "ٱلَّذِينَ إِذَآ أَصَـٰبَتۡهُم مُّصِيبَةٌ۬ قَالُوٓاْ إِنَّا لِلَّهِ وَإِنَّآ إِلَيۡهِ رَٲجِعُونَ "
"Ambao uwapatapo msiba husema hakika sisi ni(Waja) wa Mwenye-enzi-Mungu, na kwake yeye tutarejea"
Ikiwa huko mwanzoni umeshaambiwa hiyo yote ni mitihani, sasa hofu inakuondoka unakubali matokeo yote kumbe ni kazi ya Mwenye-Enzi-Mungu na wewe huwezi kushindana na Molla wako, ilobaki ufanye nini?, uridhike, na ukiridhika ndipo kikitokea kifo japo una huzuni lakini unakua mwepesi wa kuridhika na kukubali kuwa mwenyewe ndie aliyeleta na sasa kakichukua, ukiwa huna mali unajua Mollah ndie Mjuzi anajua sababu ya mimi kutokunipa mali, Ukifilisika pia unaelewa yeye ndie alonipa na sasa kachukua, Ukiwa na njaa, sasa unajua kwa subira yako kama anaweza kuniponesha na maradhi hashindwi kunipa njia ya kupata riziki ya chakula, ukishapata zawadi hii ya subira ukawa unajua kila kitu anapanga Mollah wangu, na mimi sasa sitaki kushindana na dunia hii, Nimeridhika nataka niishi kama njiwa vile hana wasiwasi basi unapata Ridhaa ya Mollah wako na unaingia katika aya ya 157 ya sura hiyo hiyo inayosema,
" أُوْلَـٰٓٮِٕكَ عَلَيۡہِمۡ صَلَوَٲتٌ۬ مِّن رَّبِّهِمۡ وَرَحۡمَةٌ۬ۖ وَأُوْلَـٰٓٮِٕكَ هُمُ ٱلۡمُهۡتَدُونَ "
"Hao juu yao zitakuwa baraka zitokazo kwa Mollah wao na Rehma, na ndio wenye kuongoka"
Ukishatimiza masharti ya Subira ukajifunga kweli kweli kuikabili mitihani alokupa Mollah wako na kufuzu, basi zinamiminika Baraka kutoka kwa Mollah wako(Blessing) watu wanakua wakisema aa usishindane naye yule kabarikiwa, na Rehma za kila aina zinakushukia unakua mwenye kufanikiwa katika mambo yako pasi hata kuomba, utaona mtu kakuletea zawadi bure, mara hichi mara kile, watu wanakutamania, na baraka za Mollah wako ni nyingi huwezi kuzipokea zote ukawa umezuia utaanza kuwapa na wenzio, utakua ukitoa kwa furaha, na ukipata hali kama hiyo wewe tena unakua umeshaongoka, umefuzu mtihani, umefanikiwa kutizama bila ya kutumia Macho(Ndio Maana ya Subira). Mollah wetu Tujaalie tupate hekima hii ya subira iwe kila mtihani wako ukija tunauona mpaka unaondoka, tujaalie kheri ndani ya mtihani huo tusikusahau daima, tupe moyo wa subira tudumu katika kuhifadhi yale ya kheri uliyotuamrisha ili tupate Baraka na Rehma zako kama ulivo ahidi. Amin.

Subscribe to:
Posts (Atom)