Asalaam Aleiykum,
"ٱلَّذِى عَلَّمَ بِٱلۡقَلَمِ"
"Ambaye amemfundisha Mwanaadamu kwa wasita(Uwezo)wa kalamu(Akili)"Kiungo kinotumika ni hicho hicho mwanzo ni kwa ajili ya kufundishwa, na mwisho wake ni kusomeshwa, mwanzo ni ya kudumu, na ya pili ni ya muda, na zote mbili atakapo Mungu huziondosha elimu hizo kama alivosema katika sura ya an-Nahl aya ya 70 " وَمِنكُم مَّن يُرَدُّ إِلَىٰٓ أَرۡذَلِ ٱلۡعُمُرِ لِكَىۡ لَا يَعۡلَمَ بَعۡدَ عِلۡمٍ۬ شَيۡـًٔاۚ"
"Na miongoni mwenu wako wanorudishwa katika(Umri wa uzee)akawa hajui chochote baada ya ujuzi(alokua nao)"mpaka mwisho wa aya inapomalizikia, inaondoshwa kabisa elimu na kujua, inabakia (Nafs)bila ya taaluma yoyote, mafundisho yashapotea, na sasa umebakia kuwa mzigo kwa wale wenye kujua wakutumikie, na wao wanakutizama hawana uwezo wa kukufundisha tena, kwa hiyo kutoka kwenye kufundishwa kwenda kwenye kusomeshwa halafu kurejea kwenye (Nothingness)ukiyajua hayo, basi toka machozi kwa ajili ya Mollah wako aliye Mkarim, fanya hima kumkumbuka na kunyenyekea kwa ajili ya hisani hii ya kufahamu aliyokujaalia, vipi mimi leo nitakua nina uwezo wa kufundisha.
"عَلَّمَ ٱلۡإِنسَـٰنَ مَا لَمۡ يَعۡلَمۡ"
"Akamfundisha Mwanaadamu (chungu ya )mambo aliyokua hayajui" Kusoma ni (Capacity)ya (Memory)ikiwa akili yako ina kumbukumbu nzuri basi moja kwa moja unakua hodari, kusoma sio (Future)kusoma ni (Past), Lakini kufundishwa ni (Communion)kitu chenye kutokea ndani, pahala pasipojulikana, (Mfano unatengeneza gari ushakwama, hujui ufanye nini uko porini na usiku unaingia simba washaanza kuunguruma, mara inakujia katika Akili yako tia msumari gari itawaka, na kweli ukiweka msumari gari imewaka)huko ndio kufundishwa,(Akamfundisha chungu ya mambo asiyoyajua).
Vipi leo niweze kufundisha wakati mie mwenyewe nafundishwa, Katika Ulimwengu huu kila kitu ni maajabu, kila leo siku ya mafundisho, ulivolala jana, na uliyoyatenda jana yanaweza kuwa masomo, lakini yanotokea leo yote ni mafundisho, jogoo kawika , mtoto kazaliwa, mti umekatwa, fulani kafariki yote hayo ni matukio katika maisha na kila tukio si kusomeshwa bali ni kufundishwa, na ukijaribu kukimbilia kwa Mwalim atakupa masomo lakini sio mafunzo, unaweza kujifunza ukikaa na Sheikh na ukasoma bila ya Sheikh kufungua mdomo, lakini unatakiwa wewe mwanafunzi jee uko tayari kusoma kwa njia hiyo, au ndio unakaa kwa Sheikh unangoja akosee tu upate(kumla nyama), mwanzo lazima upate mafunzo vipi utasoma kutokana na ukimya wa Sheikh, kwa wale wanojua kufundisha basi wanakua hawana haja ya kusomesha, mnaweza kwenda kwa Sheikh au Mwalimu, akasoma aya moja mkakaa masaa matatu mnachambua aya moja na mkiondoka mfano wake mmesoma (Kitab kizima).
Kufundishwa yatakiwa uende mwenyewe katika barabara ya maisha ndio kidogo kidogo utaanza kujua hili shimo, lile bonde, huyu ngamia, huu mlima, hili jabali, zile nyota, hapo hutaki kusomeshwa, hapo unataka kufundishwa na mfundishaji ni mwenyewe Subhanna, na anakujulisha moja baada ya jengine katika ufalme wake, vipi mimi leo nitakua na uwezo wa kufundisha,
Tizama mtoto mchanga anavofundishwa akiwa kwenye maji, sio kwa sababu mwepesi au anajua kuogelea bali anafata sheria ya maji,inasemaje, utakapoingia basi usipaparike, usishtuke, haina haja ya kufanya chochote utaelea, lakini ngoja sasa upewe (Swimming lesson)uone mambo, angalia unakuaje au muangalie yule anofahamishwa anakua vipi,watu wanatia masomo katika akili yake , hofu inamuingia ndani ya akili, anahisi sasa hivi ndio nazama, nitakufa mie, lakini baada ya muda akiwa peke yake akafanya hivi na vile mara anapata maarifa anajiona anaelea, kashajua siri ya kukaa kwenye maji bila ya kuzama, hapo mafundisho yashamteremkia.Na kama memsahau mfundishaji ni nani basi endelea part 3
No comments:
Post a Comment