Monday, April 1, 2013

MAKOSA YA MJA MWENYE SHIDA PART 3


Asalaam Aleiykum,

Na kitu cha Nne  ni hichi labda cha kupatwa na Msiba pengine wa mtoto au mume au mke au mtu hashiki uja uzito uone hapo hasira na mayowe na huzuni zinavo tawala, Masikitiko yanakua hayeshi, Uchungu ndio haumaliziki, mtu anaona kaonewa imekuaje au kuna mtu kamfanyia, mbona wengine wanapata yeye kakosa nini, anafikia mtu kuuliza kwanini Mungu kamchukua mwanawe bado mdogo, na wengine wenye kupewa hao watoto, basi wanaletewa mitihani ya kuja kwa watoto hao mpaka huyu Mzee anafikia kusema hee Mollah wangu umenipia nini shetani huyu, jana nilikua polisi leo niko Hospital ananila unga wa Roho Mtoto huyu, na kama huujui unga wa Roho mtizame Mzee mwenye mtoto nunda utaujua.
Halafu linamalizikia la Matunda, sababu wanaadamu ni wenye kupenda matunda, ni wenye kujua Ladha nyingi za Matunda kwa hiyo hili ni kama lile la chakula nalo linakatwa ili mpate kutizamwa mtakua katika hali gani. Inamalizikia aya kwa kutajwa wabashirie wenye kusubiri.
Nini Subira? Soma uzuri hapa na kwa makini kabisa ili upate faida sasa ya kuepukana na huo Mtihani, Jifundishe kupata jawabu la huo Mtihani, Nini Subira?, Subira katika Ulimwengu wa Lugha ina Maana nyingi tu, kama vile si Tayari, haijesha, inakuja labda itatokea na tafsiri nyingi tu ya kutumika neno la subira kwa ufundi wa Lugha, lakini leo nakujulisha katika Ulimwengu wa Pili haitumiki Lugha ila inatumika (Picha) ndio maana ukiota huoti lugha unaota mifano, sasa katika Lugha ya huko Ulimwengu wa Pili Subira ina asili moja na kutizama(Ndio maana hukuti-Mawalii kutumia neno la Sabira na Basira)sababu wamegundua linafanya kazi shughuli moja. Sasa tupate mfano wa neno hilo hapa Ulimwenguni kwetu, Mwanamke akishika mimba mnakua mshagundua kama ni mja mzito, mnajua kuna kiumbe kinakua ndani ya tumbo, halafu baada ya kukua kitazaliwa(sasa tizama kwa lugha unasubiri)lakini kwa matendo unatazama au kuangalia mpaka mtoto atakapozaliwa, huna la kufanya huwezi kulazimsha mtoto akue haraka haraka, unasubiri au kutizama kadara ya Mwenye-enzi-Mungu itimie, na wewe hapo umeridhia, na hiyo ndio Subira, hilo ndio kusudio la subira, unatakiwa uridhie mtihani wa Mollah wako, akikuletea Mtihani wa hofu, wewe utizame(Be Aware)basi hakuwekei sana Mollah wako ila hofu itapotea, (Nisiseme hivi tena ikawa mwizi anavunja ukasema Shk Baja kasema mtizame tu, laa piga kelele) naam ukiwa na njaa usimsahau Mollah wako jua anakujaribu itizame njaa yako, fanya jitihada kwa njia alizokuonesha Mollah wako na yeye atakupa Riziki yako, lakini usishindane na njaa ndipo unaanza kuzua mabalaa chungu nzima, Umekosa Matunda ridhia jana ulipata leo hujapata, una kazi ya utopasi shukuru hivi ndivo alivonipangia Mollah wangu nenda kazini huku umefurahi, ukiwa karani ridhika na kile ulichopewa kwani mitihani yote inaanza na kuto ridhika kwako, umepewa mali au umenyimwa shukuru sema mimi nipo naitizama kudra yako Mollah wangu na wala siyumbi kwani nimeshagundua mambo haya matano yapo kama vilivyo vidole vyangu vya miguuni na mikononi, na kama ninavyo vitizama vidole vyangu na sasa nitayaangalia mambo haya matano hayani shughulishi tena, nini kinatokea ikiwa utasubiri na kupata huo muono wa subira ulokusudiwa, hapo hiyo subira inakurusha katika jambo jengine kabisa unachupa moja kwa moja mpaka katika Aya ya 156 Endelea Part 4

No comments:

Post a Comment