Sunday, April 14, 2013

UKOMBOZI WA NAFSI PART 3

Asalaam Aleiykum,

Sasa ikiwa unataka ukate hiyo minyororo shuruti lake ubadilike, na kubadilika kwenyewe uchague kipi cha mwanzo utakibadilisha, wewe una vitu vingi, mimi leo nakuchagulia cha mwanzo kilicho katika ukumbi wa maonesho nacho ni huo mwendo wako na mtazamo wako, kwanini vikatajwa hivyo, kwa sababu hizo ni alama za kiburi, na alama hizo zinatokea ndani kwenye Nafsi yako, na ukibadilika nje na ndani haiwezi kukaa desturi hiyo tena, angalia Luqman aya ya 18.
" وَلَا تُصَعِّرۡ خَدَّكَ لِلنَّاسِ وَلَا تَمۡشِ فِى ٱلۡأَرۡضِ مَرَحًا‌ۖ إِنَّ ٱللَّهَ لَا يُحِبُّ كُلَّ مُخۡتَالٍ۬ فَخُورٍ۬"
"Wala usiwatizame watu kwa upande moja wa uso, wala usende katika nchi (Ardhi)kwa maringo, hakika Mwenye-enzi-Mungu hampendi kila ajivunae, anojifaharisha"
Usipite ukayatangaza maisha yako, utakua umo khasarani, utafukuzwa kwenye ufalme wa Mwenye-enzi-Mungu, itakua umejishughulisha na wanaadamu wenzio na umemsahau Mollah wako, sasa ufanye nini? Mollah wako anataka ubadilike uwe katika waja wake alowataja katika sura ya Furqan aya ya 63,
"وَعِبَادُ ٱلرَّحۡمَـٰنِ ٱلَّذِينَ يَمۡشُونَ عَلَى ٱلۡأَرۡضِ هَوۡنً۬ا وَإِذَا خَاطَبَهُمُ ٱلۡجَـٰهِلُونَ قَالُواْ سَلَـٰمً۬ا"
Na (hao)waja wa Mwenye-enzi-Mungu ni wale wanaokwenda (Ardhini)Ulimwenguni kwa unyenyekevu, Na wajinga(wakikutana nao)wakisema nao (kwa ubaya)huwajibu(kwa)salama. kukoje huko kwenda kwa unyenyekevu, ni mwendo wa taratibu, kuwa na tahadhari yakwamba katika ardhi hii Mollah wangu kaumba viumbe wengine sina haja mie ya kuviangamiza, nikikutana na wenzangu na nyenyekea kwa heshima na huku namsalimia kila mtu, awe mbaya au mzuri wote nawaamkia kwa maamkizi ya amani ya Mwenye-enzi-Mungu iwe juu yao.ukisha kuyaweza hayo mawili ya mwanzo sasa ushaanza kuupata huo Ukombozi ulokusudiwa, ushaanza kubadilika, na ukibadilika tu unatakiwa uanze kwa haraka kujipendekeza kwa Mollah wako kama isemavyo aya katika sura ya Alam nashirah aya ya 8 "وَإِلَىٰ رَبِّكَ فَٱرۡغَب" Na kwa Mollah wako jipendekeze"
Vipi utajipendekeza kwa Mollah wako na wewe humjui, umeshapewa madawa yote ya kukutibu ili umjue Mollah wako lakini dawa hazifai, umejaribiwa kwa Habat-muluki, umenyeshwa shubiri dohani lakini zote hazijafanya kazi, basi wacha nikupe dawa hii labda itakusaidia katika huko kujipendekeza, ikiwa ushagundua umepata ukombozi sasa anza kufanya tendo hili ambalo kama utalifanya kwa uhakika na kudumisha hali hiyo basi utajikuta ghafla umetokezea na unaishi katika kundi la Mawalii, Ufanye nini kuwa mwenye kutia udhu masaa 24, kaa na udhu kila wakati,mpaka ukitaka kulala tia udhu, nini kitatokea baada ya mwezi mmoja au miwili ukiweza kukaa na udhu bila ya kuvunja ada hiyo, huku unakumbuka wakati wote mimi nina udhu, utahama katika udhu na utakua unamkumbuka Mollah wako, na ukipata kumkumbuka Mollah wako kama ulivo ukumbuka udhu hapo unakua ushafanikiwa na hali hiyo ya kukumbuka haiondoki tena mpaka uhai wako unamalizika katika Ulimwengu huu, na huko uendako unakua katika walofuzu, na kumbuka Mollah wako akiwa katika  fikra zako kila wakati hutendi tena dhambi, na hata ukitaka kutenda basi hufanikiwi. Namuomba Mollah wangu atukomboe tutoke katika maisha ya ufakhari na kujionesha, atukirim mwenendo wa kumkumbuka yeye mpaka mwisho wa Umri wetu. Amin.


No comments:

Post a Comment